Waliovua ``Samaki wa Magufuli`` wahukumiwa miaka 21 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliovua ``Samaki wa Magufuli`` wahukumiwa miaka 21

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Feb 25, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,610
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Raia wawili wa Kichina, Hsui Chintai (63), kushoto, na wakala wake, Zhao Hinqui, wakisindikizwa na askari Magereza kwenye Mahakama Kuu Tanzania jana, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kuvua samaki ndani ya eneo la maji ya Tanzania kinyume cha sheria.


  Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, jana ilimhukumu kulipa faini ya Sh. bilioni 21 au kwenda jela miaka 30 nahodha Hsu Chiontai wa meli ya Tawariq 1, baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili, ikiwemo kuingia eneo

  la Uchumi la Bahari Kuu ya Tanzania (EEZ)na kuvua samaki eneo hilo bila kuwa na leseni.
  Kadhalika, mahakama hiyo imemhukumu kulipa faini ya Sh. bilioni moja au miaka 20 wakala, Zhao Hanquin wa meli hiyo

  baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kuingia eneo la EEZ kinyume cha sheria.
  Jaji Augustine Mwarija pia aliamuru meli hiyo kutaifishwa kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya sheria ya uvuvi namba 18 kifungu kidogo cha (1) ambayo ilikuwa kielelezo namba moja kwenye kesi hiyo.

  Washtakiwa watatu waliachiwa huru baada ya ushahidi uliotolewa na pande zote mbili kushindwa kuwatia hatiani ambao ni wakala Hsu Sheng Pao na Cai Dong Li na Chen Rui Hai ambao ni wahandisi wa meli hiyo.

  Jaji Mwarija alisema baada ya hoja zilizotolewa na pande zote mbili mahakama imezingatia hoja hizo na kwamba adhabu zimetolewa kwa mujibu viwango kulingana na sheria ya makosa dhidi ya washtakiwa. Alisema meli hiyo ilitumia majina tofauti ikiwemo Tawariq 1 na Tawariq 2 kiasi kwamba Mahakama imeshindwa kuelewa jina gani ni sahihi hivyo haitambuliki.

  Halikadhalika washtakiwa walikuwa na leseni mbili tofauti za kufanya uvuvi kinyume cha sheria. Wakili Bendera alisema hajaridhika na hukumu iliyotolewa kwa washtakiwa hao wawili na kwamba upande wa utetezi wana nia ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

  Machi 23, 2009, washtakiwa hao na wengine 32 walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu, , wakikabiliwa na mashtaka mawili, shtaka la kwanza ni kuvua samaki bila leseni kinyume na sheria ya Uvuvi wa Samaki katika kina kirefu ya mwaka 2009.

  Shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Machi 8, 2009 washtakiwa walikamatwa wakivua samaki bila leseni. Hata hivyo, washtakiwa 31 waliachiwa huru baada ya mahakama hiyo kuona kuwa hawana kesi ya kujibu.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kwann hamsomi post za wenzenu kabla hujapost yako?
  unarudia kitu walichopost then its meangless
   
Loading...