waliovamia viwanja Jumuiya ya Wazazi (CCM) watakiwa kuvisalimisha mara moja

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,000
wazazi.gif


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha mapainduzi(CCM),Majura Bulembo akionyesha moja za mikataba kati ya jumuiya hiyo na Mmiliki wa Shule za Green Acres iliyokiukwa jijini Dar es Salaam jana.Kulia ni Katibu wa jumuiya hiyo, Khamis Dadi.Picha na Fidelis Felix

Na Raymond Kaminyoge

JUMUIYA ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeanza kukunjua makucha na kuwatangazia mafisadi waliovamia viwanja vyake kuvisalimisha mara moja vinginevyo watanyang'anywa kwa nguvu.


Uamuzi wa jumuiya hiyo umekuja ikiwa ni takriban mwezi mmoja baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuueleza mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika mjini Dodoma kwamba mali za jumuiya hiyo zikiwemo shule zimeuzwa na kumilikishwa watu binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo alisema kuwa, kamwe mali za umoja huo haziwezi kuendelea kuwa `shamba la bibi.'
Alisema asilimia 85 za rasilimali za jumuiya hiyo zilizovamiwa na watu mbalimbali ziko katika mkoa wa Dar es Salaam.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom