Waliouziwa nyumba za Serikali matatani

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
IMG_20190213_074634.jpg

===========

WATUMISHI wa serikali walioshindwa kukamilisha malipo ya nyumba za serikali walizouziwa mwaka 2002, wapo hatarini kunyang’anywa nyumba hizo. Mwaka 2002 Serikali ya Awamu ya Tatu ilitangaza kuuza nyumba zake kwa watumishi wa umma sehemu mbalimbali nchini, ambako ilitoa muda wa miaka 10 wawe wameshakamilisha malipo hayo huku wakizuiliwa kubadilisha matumizi hadi miaka 25 ipite.

Hivyo muda wa kuwa wamemaliza kulipa fedha hizo umeshapita, ambao ni mwaka 2012 huku ule wa kuanza kubadilisha matumizi ni mwaka 2027. Lakini, hata hivyo, gazeti hili limebaini kuwa baadhi ya waliokuwa watumishi wa umma na wengine bado wanaendelea na utumishi wa umma, waliouziwa nyumba hizo, hawajamalizia kulipa fedha na wamekiuka mkataba wa mauziano kwa kubadilisha matumizi ya nyumba hizo.

Wapo ambao miaka 10 imepita hawajamaliza kulipa gharama na wameshabadilisha matumizi ya nyumba hizo, kwa kujenga nyumba za kisasa za kupangisha (apartments), kuingia ubia na kujenga maduka makubwa, ofisi na hata baa au kumbi za burudani na wengine wameziuza.

Hayo yamefanyika hasa kwenye maeneo waliyokuwa wakiishi watumishi wa ngazi za juu serikalini kama vile Oysterbay, Masaki, Upanga na Mikocheni, Dar es Salaam. Katika kupata uhalisia wa ni idadi ya nyumba ngapi za aina hiyo, ambazo hazijamaliziwa kulipiwa gharama zake na kiasi gani cha fedha, ambazo serikali ingetakiwa kupata kama zingelipwa kwa wakati, gazeti hili lilifanya mahojiano maalumu na Kaimu Meneja wa Sehemu ya Miliki na Huduma za Nyumba wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Erasmi Tarimo.

Mahojiano hayo yaliyochukua takribani dakika 45 yalifanyika kwenye ofisi ya Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Daudi Kondoro, ambaye pia alikuwa akifuatilia majibu ya kina kutoka kwa Tarimo.

Tarimo alifafanua kuwa kwa waliomaliza kulipia gharama zote za nyumba, hawakupewa kibali na TBA cha kubadilisha matumizi, kwa kuwa wakishamaliza kulipa gharama, nyumba zinakuwa mali zao, ila sasa kama wakipewa kibali na halmashauri za manispaa waliopo, hilo linakuwa sio tena suala la TBA.

Alisema kwa waliobadilisha matumizi huku wakiwa hawamaliza hata kulipa fedha za serikali, TBA ina uwezo wa kuwanyang’anya. Kuhusu idadi kamili za wadaiwa hao na fedha wanazodaiwa kwa ujumla, gazeti hili linaendelea kusubiri takwimu halisi kutokea TBA, ambapo Kondoro licha ya kuagizwa kutolewa kwa takwimu hizo, agizo lililotekelezwa na Tarimo kwa muda wa siku saba sasa gazeti hili linangojea taarifa rasmi kutoka TBA.

Hiyo ni kutokana gazeti hili kutakiwa kuwasilisha barua rasmi ya kuomba takwimu hizo, hitaji ambalo Jumatatu ya wiki iliyopita iliwasilisha ombi rasmi la kupewa takwimu hizo, lakini hadi jana taarifa hizo hazijajibiwa.

Tangu kuingia madarakani, Rais John Magufuli amekuwa mstari wa mbele katika kufuatilia ukusanyaji wa fedha za serikali kutokea kwenye miradi yake mbalimbali. Hakusita kutoa neno kuhusu uuzwaji wa nyumba hizo za serikali na kutaka ufuatiliwe, ili wababaishaji wa aina hiyo ambao hawajalipa, wachukuliwe hatua.

Waliouziwa nyumba hizo, waliuziwa bila ya kuwapo kwa nyongeza ya asilimia yoyote kwa maana ya fedha ya faida, ila licha ya kuwa nyingi zilikuwa kwenye maeneo muhimu ya kibiashara.

Hata hivyo, wapo hao ambao hawajamalizia kuzilipa. Mkataba kwa waliouziwa nyumba hizo, hawakutakiwa pia hata kufanya matengenezo makubwa; na kama kulikuwa na haja ya kufanya matengenezo makubwa ya nyumba hizo, walikuwa wakitakiwa kupewa kibali kutokea TBA.

Kwa mujibu wa Tarimo, TBA inao uwezo wa kumnyang’anya nyumba mtu aliyekiuka mkataba huo. Gazeti hili litaendelea kufuatilia kwa kina takwimu hizo kutokea TBA ili kuwabainisha ambao hawajalipa fedha hizo na kukiuka masharti ya kubadilisha matumizi. Katika mitaa mbalimbali hasa jijini Dar es Salaam kama vile Oysterbay, Masaki na Upanga, kuna maghorofa mengi ya kisasa ambayo yamepangishwa kwa shughuli za kiofisi, huku mengine yakitumiwa kama makazi ya kuishi kwa wageni na hata Watanzania, pia huku kwa asilimia kubwa kodi yake inatozwa kwa Dola ya Marekani.


===========
Nina wasiwasi kama zoezi hili litafanikiwa.

Kama ni hivyo basi tuanze na wale waliojigawia nyumba kwa bei karibu na bure miaka ya 90.

IMG_20190213_081158.jpg
 
Mimi hapa ndio huwa nashindwa kuelewa, serikali inajenga nyumba kisha zinapotea.
 
Ila kwa kweli uuzaji wa nyumba za serikali uliumiza sana wananchi. maeneo kama oysterbay yalikuwa ni vema kwa viongozi wa serikali. hata ukijenga leo uta jenga mbagala. Wengine waliouziwa wameshatangulia mbele za haki na waliorithi hawakuwahi hata kuwa watumishi. Ila awe Magufuli au nani kuna siku ataingia kiongozi hizi nyumba zitarudishwa. wale walionunua wasifikiri wako salama.
 
Na aliyeziuza je? yuko salama....?
Kwa hili, japo huwa namkosoa Magufuli, hana hatia. Magufuli aliuza nyumba za serikali kwa kufuata maagizo ya Mkapa. Mkapa nae alijiuzia baadhi ya nyumba.

Magufuli kama waziri - na rafiki yake Mkapa, asingepinga agizo la raisi Mkapa. Alichofanya Magufuli ni kutumia madaraka yake kama waziri husika kuuzia nyumba watu wawili au watatu wa karibu yake, kutia ndani mdogo wake. Hiyo ni kama marupurupu ya uwaziri ambayo ndugu zako mara nyingine wanafaidi. Hakupokea rushwa toka kwa hawa watu wake - walilipa nyumba kihalali. Alifanya kutumia "loophole" iliyokuwapo kujinufaisha.

Kama kuna mtu wa kumlaumu na kumnyang'anya nyumba, basi wa kwanza ni Mkapa. Mkapa huyo huyo ndio alijiuzia mradi wa serikali wa Kiwira Coal Mine kwa bei poa.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom