Waliouziwa nyumba za Serikali matatani

Jiwe alishatutia hasara mara ya kwanza kwa kuziuza kwa bei cheee

Sasa atatutia hasara tena pindi akiwanyang'anya kinguvu maana watatupeleka mahakamani na kulipwa fidia ya mabilioni!
 
Kwa hili, japo huwa namkosoa Magufuli, hana hatia. Magufuli aliuza nyumba za serikali kwa kufuata maagizo ya Mkapa. Mkapa nae alijiuzia baadhi ya nyumba.

Magufuli kama waziri - na rafiki yake Mkapa, asingepinga agizo la raisi Mkapa. Alichofanya Magufuli ni kutumia madaraka yake kama waziri husika kuuzia nyumba watu wawili au watatu wa karibu yake, kutia ndani mdogo wake. Hiyo ni kama marupurupu ya uwaziri ambayo ndugu zako mara nyingine wanafaidi. Hakupokea rushwa toka kwa hawa watu wake - walilipa nyumba kihalali. Alifanya kutumia "loophole" iliyokuwapo kujinufaisha.

Kama kuna mtu wa kumlaumu na kumnyang'anya nyumba, basi wa kwanza ni Mkapa. Mkapa huyo huyo ndio alijiuzia mradi wa serikali wa Kiwira Coal Mine kwa bei poa.

Acha umazwazwa wewe, kama alipewa agizo lisilo na manufaa kwa nchi alipaswa ajiuzulu.
 
Kujiuzulu uwaziri kwa ajili ya kupewa agizo na raisi kuuza nyumba za serikali? Na hujui kwamba inawezekana ulikuwa ni uamuzi wa baraza lote la mawaziri ambao kila mmoja alipata nyumba ya serikali? Unachosema ni kwamba kila baraza la mawaziri likfanya uamuzi ukiwa waziri hukubaliani na huo uamuzi basi ujiuzulu. Na kama wamepiga kura wengi wakashinda? Ni afadhali hatuna wendawazimu kama wewe kama mawaziri. Wewe ungekuwa waziri katika nafasi yake ungejiuzulu, sivyo? Acha unafiki.
 
Yes ndivyo inavyopaswa, baraza la mawaziri likifanya maamuzi yaliyo nje ya maslahi ya Taifa basi mjumbe wa baraza hilo (waziri) ana haki ya kujiuzulu kuserve katika serikali husika!
 
Kwa hili, japo huwa namkosoa Magufuli, hana hatia. Magufuli aliuza nyumba za serikali kwa kufuata maagizo ya Mkapa. Mkapa nae alijiuzia baadhi ya nyumba.

Magufuli kama waziri - na rafiki yake Mkapa, asingepinga agizo la raisi Mkapa. Alichofanya Magufuli ni kutumia madaraka yake kama waziri husika kuuzia nyumba watu wawili au watatu wa karibu yake, kutia ndani mdogo wake. Hiyo ni kama marupurupu ya uwaziri ambayo ndugu zako mara nyingine wanafaidi. Hakupokea rushwa toka kwa hawa watu wake - walilipa nyumba kihalali. Alifanya kutumia "loophole" iliyokuwapo kujinufaisha.

Kama kuna mtu wa kumlaumu na kumnyang'anya nyumba, basi wa kwanza ni Mkapa. Mkapa huyo huyo ndio alijiuzia mradi wa serikali wa Kiwira Coal Mine kwa bei poa.
Kwani hujui kutumia madaraka kwa manufaa binafsi ni kosa.
 
Yes ndivyo inavyopaswa, baraza la mawaziri likifanya maamuzi yaliyo nje ya maslahi ya Taifa basi mjumbe wa baraza hilo (waziri) ana haki ya kujiuzulu kuserve katika serikali husika!
Ajiuzulu, atumbuliwe, aachie ngazi! Hizi nyimbo watu mnaimba kwa wivu tu kwa kuwa nyie sio mawaziri. Mngekuwa kwenye position zao mngekuwa wagumu kujiuzulu zaidi hata ya wao.
 
Kwani hujui kutumia madaraka kwa manufaa binafsi ni kosa.
Hakujiuzia, aliuzia watu wengine. Hayo sio manufaa binafsi kwa kuwa hakufaidika binafsi. Ndio maana nikasema alitumia loophole iliyokuwapo.

Ni sawa na mimi nikiwa Mmakonde kukawa na application za kazi mbili ambazo ziko sawa kwa sifa, Mchaga na Mmakonde mwenzangu. Kwani nikimuajiri Mmakonde mwenzangu nina kosa?
 
Sijaelewa, labda mwandishi kakosea kichwa cha Habari.

Waliouziwa au waliouza???

Swali Ni moja tuu hapa... Muheshimiwa Hakimu je? Kama nyumba hizi zilikua haziuzwi ningenunua????

Nyumba hizi zilikua zinauzwa na nikanunua kwa pesa yangu halali.

Asante.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakujiuzia, aliuzia watu wengine. Hayo sio manufaa binafsi kwa kuwa hakufaidika binafsi. Ndio maana nikasema alitumia loophole iliyokuwapo.

Ni sawa na mimi nikiwa Mmakonde kukawa na application za kazi mbili ambazo ziko sawa kwa sifa, Mchaga na Mmakonde mwenzangu. Kwani nikimuajiri Mmakonde mwenzangu nina kosa?
Hiyo loophole unayosema aliitumia ndiyo kosa lenyewe.
 
habari leo wametumwa kusikilizia kama watu wanakumbukwa mwizi wa nyumba za serikali ni nani
 
Hiyo loophole unayosema aliitumia ndiyo kosa lenyewe.

I say, kutumia loophole sio kosa kisheria - because you are almost out of the law, but just a little bit inside the law!

Kwa mfano, agizo lilisema hizo nyumba wauziwe watumishi wa serikali. Yeye akamuajiri mdogo wake kuwa mtumishi wa serikali na mwezi huo huo akakubali ombi lake la kuuziwa nyumba. Sasa kama agizo halikusema watumishi wa serikali wawe wametumikia serikali kwa muda gani, utamshitaki kwa kosa gani? Kumbuka kwamba agizo haliku-specify muda wa kuwa mtumishi wa serikali ili kutowanyima fursa za kuuziwa nyumba mawaziri ambao waliingia serikalini kupitia ubunge na uwaziri, na kimsingi walikuwa na muda mfupi kama watumishi wa serikali.

Hivi unafikiri alikurupuka kumuuzia nyumba mdogo wake?
 
Agizo lilitoka katika kikao cha baraza la mawazili kwamaanaiyo serikali ilipitisha. Serikali ilizishindwa izo nyumba kwakua ilitakiwa iwe inaweka bajeti ya kuzihudumia marakwamara na ikaonekana ni mzigo mkubwa ukichukulia Nyumba nyingi zimejengwa na wakoloni miaka ya hamsini.Maamuzi yalikua wanaoishi kwenye nyumba izo wapewe kipaumbele na walipe kidogokidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom