Waliouziwa nyumba za serikali Masaki wanapata zadi ya 200milioni bila kulipa kodi.

rugumye

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
561
178
Ndugu wanajamii nyumba za serikali zilizouzwa zinawaingizia faida kubwa waliozinunua (MASAKI-DAR), mfano nyumba moja hupangishwa kwa $10,000 mpaka $15,000 kwa mwezi sawa na 16mil mpaka 24mil.

Waheshimiwa hawa hawalipi kodi za serikali kwaani baadhi hawana TIN wala hawajasajiliwa VRN. Pia nyumba hizi asilimia kubwa hazina mita za maji (wanalipa flat rate 20,000/= NA 30,000/= kwa mwezi huku zote zikiwa na reserve tanks kuanzia lita 10,000 mpaka 30,000 za ujazo) hivyo huikosesha mapato DAWASCO.

Kumwagilia bustani huku masaki siyo issue kwaani maji ni ya kumwaga hakuna tofauti kati ya masika na kiangazi ni evergreen mwaka mzima. Ukiuliza nyumba hizi ziliuzwa kwa gharama ya shilingi ngapi utacheka, nimeambiwa kuwa nyumba ya bei ya juu iliuzwa 100milion.

HOJA YANGU: Zilirudishwe haraka ili serikali izipangishe ipate mapato zaidi. DAWASCO wafunge mita nyumba zote. kama wanakataa waandishi wa habari wafanye utafiti au waje niwape evidence kwani mimi ninafanya kazi masaki. lakini nina amini DAWASCO wanalijua hili kwaani huwa wanapita.

Je walala hoi wanalipa kiasi gani kwa mwezi?

NAWAKILISHA.
 
nadhani beneficiaries wengi ndio wanaosimamia utendaji wa serikali hii, dont expect anything!!
 
People should not be afraid of their governments, goverments should be afraid of their people.
 
With corrupt leaders, governmental officials, friendship in everything; expect nothing good for the citizens.
 
Mmoja wa makamishna wa TRA ni kati ya wanaomiliki na kupangisha hizo nyumba.
Sasa ailipe TRA ipi?
 
Ni kweli, waache tu wapate hizo faida.... hizi nyumba kote zilikouzwa kinyemela tutazirudisha tu.... na watalipia kila kitu...
 
Wivu tu huo...riziki ya mwenzio usiilalie mlango wazi!

Watu kama nyie ndio kikwazo kikibwa katika maendeleo. Full uswahili na nashangaa kukuta watu wa aina yako kwenye jamvi. Naona aibu kushea jamvi na watu kama nyie. NYAMNBAAAAAAF
 
Serikali ya magamba kila kitu noma.....hii nchi ya waheshimiwa wachache ambao wanamiliki, wanahodhi, wanafanya maamuzi muhimu kwa nchi, wanahukumu lakini mwisho wa siku ndiyo wanafaidika na rasilimali za nchi hii.....tunahitaji mabadiliko

  • :yell:
 
Najua faida y kodi itakusaidia wewe km si mzazi wako au ndugu yako, najua kuna ndugu yako hapa Dar analipa maji DAWASCO zadi ya 50,000 kwa mwezi au ananunua maji dumu 500/=. najua kodi hii itakusaidia ukiwa mgonjwa au kukuelimisha kwaani unahitaji shule zaidi. najua kodi hii itamnunulia dawa mzazi wako km si kmdogo wako. Naheshimu mawazo yako pia kwaani level ya kuelewa na kupambanua mambo inatofautiana. Pole ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom