Waliouwawa Zanzibar na Bara kwenye Uchaguzi mwaka jana haki zao wanapataje?

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Yaani bado kabisa tuna safari ndefu mno Zanzibar walivunjwa miguu na kuuwawa na Utawala wa Magufuli

Watu kwa maelfu wamewekewa vilema vijana kwa wazee.

Haki za hawa watu ukiunganisha na Wa huku bala waliouwawa kama Akwilina,Azory Gwanda, Ben Saanane na Tundu Lissu wanapataje haki zao?

Samia bado sana ana kazi ya kufanya.
 
mkuu mbona mambo haya yapo tangu chaguzi za huko nyuma, je, huko nyuma walilipwa? kama walilipa tunayo haki kumlaum rais bt ka hawakulipwa anapaswa alitazame jambo hili kwa jicho la pekee kwa lengo la kuponya taifa.
 
Wambie waende mahakamani. Ni kama upande ule Chacha wangwe aliuwawa baada ya kuutaka uenyekiti haki yake atapataje? Dr Slaa alivunjwa mkono wakati wa kukipigania chama ila cha kushangaza mwaka 2015 mzee wa chelete mfukoni akaja kupewa nafasi ya juu kugombania uraisi bila jasho, je dr Slaa mpaka leo haki yake anaipataje?
 
Siasa za kiafrika ni vurugu mechi siku zote. Walipouwawa watendaji wa serikali za mitaa kuliko Kibiti na Mkuranga ilionekana sio habari ya kustahili kupewa kipaumbele, walipoanza kuuwawa wauwaji wa watendaji ikageuka kuwa habari kwamba serikali inaua raia wake!!.

Wanaofanya ukatili wakiufanya ni sawa tu ila kibao kikiwageukia inakuwa ni habari ya kuandikwa kwa herufi kubwa tena ukurasa wa kwanza.
 
Back
Top Bottom