Waliouawa na polisi maandamano Chadema Arusha watajwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliouawa na polisi maandamano Chadema Arusha watajwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 7, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  POLISI mkoani Arusha imewataja watu wawili waliouawa na askari wake kwa risasi za moto katika vurugu zilizotokana na maandamano yaliyofanyika juzi mkoani hapa.

  Mbali na watu hao, Denis Maiko na George Mwita Waitara wote wakazi wa Sakina jijini hapa, watu wengine wanane wakiwemo askari watatu walijeruhiwa katika vurugu hizo huku wengine 49 wakishikiliwa na polisi.

  Kutokana na ufinyu wa nafasi katika kituo cha Polisi, wafuasi 49 wa Chadema waliokamatwa walilazimika kulala ndani ya karandinga usiku kucha hadi jana walipoachiwa baada ya kupewa dhamana na Mahakama.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye amethibitisha hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa majeruhi hao wanane wamesambazwa katika hospitali mbalimbali kwa matibabu zaidi.

  Mbali na vifo na majeruhi hao, pia mali mbalimbali ziliharibiwa kutokana na kurushiwa mawe na raia wakati walipokuwa wakirejea kutoka mkutanoni.

  Mali zilizoharibiwa kwa mawe ni pamoja na magari ya Polisi, jengo la CCM Mkoa pamoja na magari yaliyokuwemo ndani ya jengo hilo na jengo la mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Salum Ally lililopo mtaa wa Bondeni.

  Polisi wanaendelea kufanya tathmini ya hasara na uharibifu uliotokana na vurugu hizo za juzi ambapo jana walionekana katika jengo la CCM wakichukua picha za video kwa ajili ya ushahidi wa hasara.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hasara hiyo mbona nadhani ni ndogo? Inatakiwa kuwe na hasara kubwa kiasi cha kutisha. Mi sijaona hasara yoyote.
   
 3. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hasara kubwa ni kupoteza maisha ya watu waio na hatia
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sure,hope hlo litamsumbua kila mmoja aliye kwenye system,kumwaga damu bila hatia ni risk n cost!wale wameacha watu wanaowategemea,itakuaje?JINAMIZI HILO LITAWASUMBUA SANA,TENA SANA!
   
 5. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Nawaomba waJFwenye wenye taarifa sahihi kwa maana ya majina au watu waliokufa au kujeruiwa tuweke wazi majina ya wahanga hao hapa JF.

  Waliouwawa....
  Denis Shirima - huyu ni fundi magari
  George Mwita Waitara
  ........
  ........


  Majeruhi
  ........
  ........
   
Loading...