Waliotunga hii sheria "Tovuti zisajiliwe Tanzania" wanaogelea maji wasiyoyajua

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,289
2,000
Nimeshangaa sana hawa watanzania kuogopa ushindani kiasi cha kutungia sheria kila kitu kilicho ktk soko moja na serikali. Tumeona seheria za sukari, sheria ya habari, tovuti, etc. Serikali imeamua kuingia ktk chain isiyo na mwisho ya kuweka mazingira yasiyo sawa kiushindani kati ya serikali na raia wake.

Ktk hili la tovuti naona serikali imeingizwa ktk maji wasiyoweza ogelea. Internet ina mengi sana. Mengiyalianzai duniani kabla ya kufika Tanzania .Na watanzania wengi walijisajili kabla ya sheria, tayari wamejenga kila kitu wanachohitaji ktk hayo mazingira.


Sasa hivi tovuti yenye dot com ndio inayowapa urahisi sana watu wa duniani kukumbuka na ndio ina mvuto.Watanzania lazima wawe na hizo domain.

Mashirika yanayosajili hizo tovuti na huduma zake wana huduma nyingine nyingi sana ambazo watanzania hawawezi pata hapa kwetu kwa bei rahisi km ya nje,na uhakika wa kuwepo hewani muda wote, au linapotokea janga km vita kubwa etc.Sidhani km Tanzania tunaweza pata huduma kwa level ya amazon,microsoft, google,godaddy, etc. Serikali kweka hizi sheria ni kuwanyima watanzania namna ya kuingia ktk biashara kwa kuwazuia wasitumie huduma hizi za bei rahisi.

Zaidi ya hizi domain kuna vitu vingi sana vinavyohusiana na tovuti km technologia za kuzuia mashambulizi ya tovuti.Hizi huduma kwa tanzania hakuna shirika linaloweza toa hii huduma.

Kuna mengi sana ambayo sidhani km watanzania wanajua watayapaje,na urahisi unakuja km watu watapada hizo huduma za ambazo zimewekwa kwa namna ya biashara km daladala kwamba unanunua unachohotaji na ukihitaji hata kikubwa sana kinapatikana.
 

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,289
2,000
Ngoja tuone hiyo ndoto ya ".tz" inatimia vipi kwa ubabe huu unaoendelea. Nchi hii haiwezi kukua kiteknologia kwa kutumia sheria za kibabe.
inaelekea jamaa wanapolazimisha vitu vyao viuzwe,huwa wanakuwa wamesahau maana halisi ya soko huria, na ushindani unaomshaidia mtumiaji kupata huduma bora. Km watu wanakimbia ushindani kupitia huduma bora, wanaamua kuhujumu wengine ni wazi wameshachemsha game hili. Mbaya zaidi mkonga wa Taifa upo hapo hakuna hata business model ya jinsi ya kutoa huduma za ndani kwa bei nzuri,ili wajasiriamali wachangamkie fursa na kuongeza thamani ya watu kutumia huduma za ndani.
 

zinj

JF-Expert Member
Jan 1, 2013
978
1,000
Hatuwez kuwa watumwa....lazma itumike dot.tz na huduma zitapatkana
Mkuu:
Tafadhali fafanua zaidi hizo huduma zitapatikana vipi na kwa gharama ipi,
Hiyo ni changamoto kubwa, na si ya kubeza kwa kuichukulia kirahisi.
 

Nazareti

JF-Expert Member
Apr 1, 2016
413
500
Hatuwez kuwa watumwa....lazma itumike dot.tz na huduma zitapatkana
Huna uwezo wewe, juzi tu hapa kagame kaleta wataalamu toka Rwanda kusaidia mfumo wa tra, au hujui hilo? eti nao walijaribu kuishambulia JF siku ya uchaguzi, naona walifanikiwa kwa masaa 5 tu na baada ya hapo ni mwendo mdundo hadi leo maana iko nje ya tz.com ndo kisa leo wanataka kampuni zote ziwe chini ya tz.com? hamna kitu kabisa
 

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,025
2,000
SHERIA hutungwa na watu kwa malengo fulani.Sheria hujifia yenyewe pale inapozidiwa na mahitaji.Sheria zinazoweza kudumu ni zile za makosa ya kudhuru watu wengine,kudhulumu au kuhatarisha uhai wa binadamu.SHERIA za makatazo na kuzuwia maendeleo ya sayansi na teknolojia hupitwa na wakati kutokana na mahitaji muhimu ya binadamu.
 

kwemanga1

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
835
1,000
Mkuu:
Tafadhali fafanua zaidi hizo huduma zitapatikana vipi na kwa gharama ipi,
Hiyo ni changamoto kubwa, na si ya kubeza kwa kuichukulia kirahisi.
Hao ndivyo walivyo mkuu wanadandia hoja wasizozifahamu achana nao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom