Waliotumwa kumuua Dr. Ulimboka wapata PIGO Afrika Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliotumwa kumuua Dr. Ulimboka wapata PIGO Afrika Kusini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TAMKO, Jul 7, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. TAMKO

  TAMKO JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Serikali ijiandae

  Tumefurahishwa na taarifa ya Pigo la ajali lililomkuta mmoja wa Kikosi kilichotumwa Huko AK kumwangamiza Dr Ulimboka. Ajali hiyo ambayo mpaka sasa ni Siri ya Kikosi haijulikani ilimpata wapi na kwa nini lakini kikosi kimeonekana kujitosa kumtibia mwenzao ambaye alitapakaa damu na kupoteza nyuzi kadhaa walizoziandaa juu ya kutafuta wapi alipo Dr. Ulimboka.

  Kikosi Hicho ambacho kinalalamika kukosa ushirikiano na wenzao wenye makazi ya Kudumu AK, kinakiri mpaka sasa Madaktari wamekuwa werevu zaidi wa kuchezesha shilingi hii kuliko wao. Kikosi hiki ambacho kama nilivyoeleza kinaundwa na Askari wa majeshi yetu yote, wale ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakishiriki vitendo haram ndani ya jamii kama ujambazi na operation za kuua kwa malipo, hawawezi kwa lolote kuacha kutimiza lengo lao kwa kuwa kama wakiasi majeshi haya basi wako hatarini kushtakiwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha kwa kuwa sasa kifungu cha kitanza kimeshalegezwa.

  Napenda kuitahadhalisha Familia ya Dr. Ulimboka na wazee waliotumwa kumpoza Dr. Ulimboka kwamba akae kimya au atafutiwe kazi nje ya nchi asirudi Tz, au asingiziwe amekufa ili jamii Imsahau, wakifanya kitendo kama hicho watakuwa tayari wameshahalalisha serikali kummaliza Mtu huyo haraka. Kama nilivyosema Dr. Ulimboka anawafaham Fika waliomtendea Kitendo hicho na miongoni mwao ni Ndugu zake waliomo kwenye "system".. HILO LIKO WAZI KABISAA

  Wazingatie ushauri wa wananchi wengi kwamba anatakiwa arudi TZ kwa siri kubwa na aibukie kwenye vyombo vyote vya habari LIVE na aelezee sakata lake mwanzo mwisho na hapo ndipo serikali itashindwa kumuua kwa maana macho ya jumuia zote yatakuwa Hapo. Zaidi ya hapo atabakia kuwa historia kama Balali..
   
 2. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Ahsante kwa taarifa..
   
 3. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,866
  Trophy Points: 280
  Mmh! Ngoja nikapate zangu :beer: maana nahisi kama akili yangu ina kizunguzungu.., Mungu tusaidie waja wako
   
 4. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Silly government. Endelea kutujuza. Huruma sana serikali ya majambazi.
   
 5. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ngoja nitengeze juice ya bamia nisipate kichaaa nitarudi tena mungu wangu.
   
 6. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nyakati hizi ni vigumu sana kuficha ukweli! ... time n space ...issue ya Ballali itakuwa hadharani kabla ya 2015...
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Endelea kutujuza mkuu! Serikali dhaifu ndio anguko lake hilo
   
 8. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,646
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Inasikitisha sana kama hapa ndipo tulipofikia kama nchi.
   
 9. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kumbe kuna mkakati tena wa kumuua huko huko RSA? God please we berge for your help please, thank you God for causing thae said Accident otherwise these people could kill un innocent man?
  Ningependa sana waendlee kuumbuka na kudhalilika!
   
 10. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Rubbish na umbilikimo wa kufikiri na kupima - lete data intelijensia kamili nani huyo alikwenda vipi sio umbeya na taarifa kutoka katika vikao vya chai maharage
   
 11. m

  mpigilie JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mungu akubariki uendelee kutupa uozo wa hii tunayoiita serikali yetu
   
 12. H

  Hute JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,045
  Likes Received: 3,916
  Trophy Points: 280
  waliomteka ulimboka hawakuwa na nia ya kumuua, kama wangekuwa na nia hiyo asingeachwa hai. kwani walikuwa na bunduki, pia wangeweza hata kumvunja shingo au hata kumnyonga akafa, kinachoonekana kwa wale wana intelijensia wataelewa, hakukua na nia ya kumuua, bali walikuwa na nia ya kumuadibisha tu kwa njia ya mateso alafu aachwe hai.

  Kwa wale wenye akili watakubaliana na mimi kuwa, kiongozi wa mgomo kuuawa si rahisi sana kama wagomaji, kwasababu machafuko yanaweza kutokea mfano wananchi wangeandamana kupinga icho kitendo..hivyo hakukuwa na nia kabisa ya kumuua, kama nia hiyo ilikuwepo, hakika asingekutwa hai, angepiga tu bunduki hata palepale alipotekewa, angefuatwa nyumbani kwake akapigwa kama wale waliomfata Pro. Mwaikusa, angefanyiwa chochote na ingejulikana ni majambazi tu yamefanya hivyo....kama ulimboka ana akili, namshauri akipona aachane na mikumbo, atumie elimu yake ambayo kodi za wananchi watz masikini zilimsomesha ili wananchi hao wasife na pia ajenge maisha yake kabla hajazeeka. labda kama anataka kuwa mfia mgomo ndo aendelee kujilipua.

  pamoja na kwamba ipo strong allengation kwamba serikali yaweza kuwa imehusika, cha ajabu ni kwamba ushahidi haupo. sasa kuituhuumu selikali si sahihi, labda kama serikali itakuwa inatuhumiwa kwa kushindwa kuwalinda raia wake ambapo hata hapo serikali inaonekana haijawa zembe......ulimboka ukipona, kama unanisikia, achana na mikumbo, tafuta maisha yako watoto wako waje waishi vizuri utakapozeeka au ukichukuliwa na Mungu.
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi Amnest suala la kumlinda Ulimboka waligoma?
  Hao jamaa waacheni tuu Mola atawapatiliza apa apa duniani!
  Wameona kuua watetea haki ni sifa na dili!
   
 14. c

  chama JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sera kubwa ya Chadema uongo, majungu na fitina je ikithibitika kuwa serikali haihusiki na kisa hiki utasema nini? Dr. Ulimboka hakuwa nabii kama Yesu subiri uchunguzi ufanyike usitulee porojo

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 15. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu ubarikiwe, naona waovu wanaumbuka
   
 16. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hebu check hapo.

  Join Date : 4th July 2012

  Posts : 2
  Rep Power : 0
  Likes Received3
  Likes Given0
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mwenyenzi Mungu amponye arudi Tanzania, akatueleze sakata lake mwanzo mwisho!
   
 18. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Endelea kusubiria taarifa ya serikali,hakuna aliyekuzuia
   
 19. d

  dguyana JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka upo sawa kimtazamo ila hujadadavua. Walichotaka wale jamaa ni kujua nini na nani yupo nyuma ya huu mgomo. Ndio maana walimchukua na kumtesa kama kufa afe polepole. Na Mungu alivyomkubwa inaonyesha baada ya Uli kuzimia wakajua tayar keshakufa sio haikuwa na ulazima wa kumuua kwa bunduki.

  We unadhani wangekuwa na nia ya kumtesa tu si wangempeleka hospital au wangemtupa pale manzese darajani? Ndio maana hata yule polisi aliepewa kipondo pale Muhimbili siku ile alikuwa anaongea kwa tahamaki kuwa 'Jmaa bado anahema'. Upo kaka?
   
 20. PRISCUS JR

  PRISCUS JR JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Napenda watu wema kama mtoa thread, mola na akupe maisha marefu endelea kutujuza mipango yote wanayopanga, umenikumbusha wakati mzee mengi alipoanika mipango na njia zote ambazo mafisadi walipanga kutumia kumuua wakakosa la kufanya. wito wangu kwa madaktari hasa walio karibu kabisa dr.ulimboka wamlinde vya kutosha wasimwamini hata ndugu labda baba na mama. mola yu pamoja na wenye haki, wadhalimu wataaibika punde. asante mkuu kwa taarifa
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...