Waliotumia jina la Mama Magufuli kutapeli wadhibitiwa

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imefungia akaunti ya facebook na tovuti ya www.focusvikoba. wapka.mobi, iliyoanzishwa na matapeli wa mtandao wakidai ni ya Mke wa Rais, Mama Janet Magufuli na kuomba wananchi kutuma fedha za kiingilio kwa Vicoba ili wapate mikopo.

Taarifa ya TCRA iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa uchunguzi wa mamlaka hiyo, umeonesha kwamba Mama Magufuli hana akaunti ya Facebook wala tovuti inayohamasisha watu kuomba mikopo ya vikundi vya Vicoba.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Ally Simba amesema katika taarifa hiyo kwamba akaunti hiyo ya Facebook iliyodaiwa kuwa ni ya Mama Janet, ilianzishwa na matapeli wa mtandao.

Dk Simba alisema ingawa kumekuwepo na maendeleo na mabadiliko makubwa katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania, kuongezeka kwa idadi ya watoa huduma za mawasiliano, idadi ya watumiaji na aina ya huduma zinazotolewa, lakini kuna wachache wanaotumia huduma hivyo kutenda uhalifu.

Kwa mujibu wa Dk Simba, wahalifu hao hutumia simu za mkononi na kwenye intaneti kuanzisha tovuti za kihalifu na kupitia mitandao ya kijamii kama vile Facebook. Alisema hivi karibuni kumekuwa na matukio ya wahalifu wa mtandao kuanzisha tovuti na blogu na pia kurasa za facebook kwa kutumia majina ya viongozi wakuu wa nchi, wabunge na watu wengine maarufu.

Wahalifu hao kwa mujibu wa taarifa hiyo, hudanganya wananchi kwamba kuna fursa za kupata mikopo au misaada kupitia vikundi vya kusaidiana, maarufu kama Vicoba na kuwataka wananchi watume fedha za kujiunga na huduma hizo kwa njia za simu za mkononi.

Alisema pamoja na kuzifungia akaunti hizo za facebook na tovuti, Mamlaka inashirikiana na Polisi kuchunguza matukio hayo na tayari hatua kubwa imefikiwa katika kuwakamata na kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kwa mujibu wa kifungu cha 15 (1) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015, mtu yeyote haruhusiwi, kwa kutumia kompyuta, kujifanya yeye ni mtu mwingine.

Adhabu kwa kutenda kosa hili kwa mujibu wa Dk Simba, imeainishwa kwenye kifungu cha 15 (2) ambacho kinasema mtu akipatikana na hatia anaweza kutozwa faini isiyopungua Sh milioni 5 au mara tatu ya thamani ya kile alichopata kupitia ulaghai huo, au kiasi ambacho ni kikubwa kati ya faini na mara tatu ya alichokipata.
 
Hii habari ingetolewa Na Msemaji wa TCRA siyo Bosi mwenyewe what does delegation of power means ?? Huko Zanzibari sijui itakua under military personnel mpaka lini ?
 
TCRA mna account humu JF,kila siku tunawakumbusha kuwa kwanini Azam Tv inakata mikondo ya luninga za nyumbani kama ITV,Star TV,Channel 5 na Channel 10....tunaomba channel hizi zirudishwe kwa watumiaji wa Azam Tv
 
Back
Top Bottom