Waliotorosha makontena 329 yasiyo na kibali bandarini wafungwa miaka mitatu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imewahukumu kifungo cha miaka mitatu jela washtakiwa wawili na mmoja kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kutorosha makontena bandarini.

Kesi hiyo ya uhujumu uchumi inahusiana uondoaji wa makontena 329 katika bandari kavu ya Azam (AICD) bila kulipiwa kodi.

Washtakiwa hao wamehukumiwa adhabu hiyo leo na Jaji Winfrida Korosso aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo baada ya kuwatia hatiani katika mashtaka 107 kati ya 110 yaliyokuwa yakiwakabili.

Waliohukumiwa adhabu hiyo ni Raymond Adolf Louis aliyekuwa meneja wa oparesheni za usalama na ulinzi Azam ICD, Khalid Yusuph Hassan na Benson Vitalis Malembo.

Louis na Hassan wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu kila mmoja kwa kila shtaka katika mashtaka 104 ya kughushi na kifungo cha miaka miwili kila mmoja katika shtaka moja la kuisababishia Mamlaka ya Mapato (TRA) hasara ya Sh12.5 bilioni.

Akitoa adhabu hiyo, Jaji Korosso amesema adhabu zote hizo zinakwenda kwa pamoja.

Mbali na adhabu hiyo ya kifungo, pia Jaji Korosso ameamuru washtakiwa baada ya kumaliza kifungo chao kuilipa TRA fidia ya nusu ya hasara waliyoisababishia, yaani zaidi ya Sh6 bilioni wote kwa pamoja.

Malembo amehukumiwa kutumia adhabu ya miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia katika shtaka moja la kuisababishia TRA hasara hiyo ya Sh12.5 bilioni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
▶Walio choma kituo cha polisi kifungo cha maisha jela.

▶Walio isababishia serikali hasara ya Mabilion Ya Pesa Miaka Mitatu Jela.

◀▶Hizi Sheria zetu kuna Umuhimu Wa Kuzifanyia Marekebisho.
 
watumishi wote wa TRA waliokamtwa waliachiwa eti DPP hana nia ya kuendelea na Kesi ..................... huu mfupa ulikuwa mgumu sana kwa Baba Jesca, Tetesi zinadai maji yaliwafika shingoni wakaamua kuwaachia watuhumiwa wa awali.
Naanza kuona ukweli upo wapi!
 
Kila nikiandika coment naifuta hii ni mara ya tisa,maana kila nikitaka ku-send nakua kama nawaona vile kesho ukipost bring back our TEAB VIBAJAJ
 
Si chadema huwa wanasema hawaoni mahakama ya Mafisadi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Funika ujinga wako angalau kwa dakika tano uinusuru heshima yako! Kwa kifupi upo uchi ubongoni mwako!
Eti mahakama ya ufisadi! Mbona inatenda kwa kiwango cha chini kuliko mahakama ya mwanzo? Hulioni hilo kwani akilini kumefunikwa na sifa za kijinga!
 
Nimeandika nikafuta, nikaandika nikafuta, nikaandika nikafuta tena. Na sasa hivi nimeandika nikafuta.

Kontena 329 miaka mi tatu.
Kuku watano miaka mitatu
 
Kwa hali hii hiyo vita dhidi ya ufisadi haiwezi kuja kufanikiwa hadi pale tutakapokuja kuamua kuwa na sheria kali kama China ambazo haziangalii sura au tabaka la mtu.
 
Back
Top Bottom