Waliotoka kwenye mashirika ya kimataifa ni wezi 'papa' wametudhalilisha!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
10,578
2,000
Mkapa aliwaleta Daud Balali kuwa gavana wa BoT na Andrew Chenge kuwa mwanasheria mkuu wa serikali kutoka umoja wa mataifa walikokuwa wakitumikia.Hawa wote wameishia kulitia taifa la Tanzania hasara ya mabilioni ya fedha na kulichafua mbele ya taswira ya kimataifa. Mbali zaidi wakaishia kujichotea mabilioni ya fedha kutokana na nafasi zao nyeti na zenye maamuzi.

Kikwete akatuletea maprofesa wawili; Muhongo na Anna Tibaijuka kutoka umoja wa mataifa walikokuwa wakitumikia.Badala yake wamelitia
tena taifa hasara na kuishia kujichotea mabilioni kutokana na nafasi zao nyeti walizo kuwa nazo.

Kutokana na mwenendo huu ni lazima tuwatazame kwa makini watu wa aina hii. Pengine wamezoea kupata fedha nyingi huko hivyo wakirudi nchini wanajiona wataishia kuwa masikini kutokana na 'vimshahara vya uwaziri, ugavana na uanasheria huku vikiwa havina mapochopocho' ya kando. Au pengine wamezoea kuiba bila kutiliwa shaka kutokana na kulundikana mapesa huko walikokuwa wakifanya kazi hivyo kutokugundulika kirahisi.

Kwa kweli wanatia shaka na wamekirhiri kwa wizi na fisadi kubwa kubwa bila hata ya woga na hofu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom