Waliotimuliwa BoT 1993 waibwaga tena BoT Mahakamani


K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Messages
1,691
Likes
2,210
Points
280
K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2013
1,691 2,210 280

Dar es Salaam. Jaribio la kupinga hukumu ya kuwarejesha kazini wafanyakazi 31 waliopunguzwa mwaka 1993, limekwama tena baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali maombi ya Benki Kuu Tanzania (BoT) ya kuongezewa muda wa kukata rufaa.

Nje ya Mahakama jana, wakili wa BoT, Sereni Mponda alisema anakusudia kuwasilisha rufaa kwa kutumia kipengele kingine akitaka mahakama ikubaliane na maombi yao ya kukata rufaa nje ya muda, akisema BoT ina nafasi kubwa ya kushinda kwa kuwa kuna suala aliloliita zito la kisheria linalohitaji mwongozo wa Mahakama ya Rufani.

Alidai Mahakama Kuu ilikosea kwa kuamini kuwa mkataba wa hiari uliotumika kuwapunguza wafanyakazi wote ulikuwa batili kwa sababu haukusajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Ajira.

Oktoba 2, Mahakama ya Rufani ilitupilia mbali maombi ya BoT ya kuongezewa muda wa kukata rufaa kupinga uamuzi wa kuwarejesha kazini wafanyakazi hao ambao shauri lao limedumu kortini kwa miaka 22.

Lakini taasisi hiyo kuu ya fedha nchini ikaomba Mahakama ya Rufani irejee hukumu yake ya kutupa maombi yao ya kuongezewa muda wa kukata rufaa, ambayo jana yaligonga mwamba tena.

Watu hao 31 ni miongoni mwa wafanyakazi waliopunguzwa kazi na BoT mwaka 1993 wakati Serikali ikirekebisha uchumi, kwa kupunguza matumizi kulikoambatana na kupunguza watumishi, kazi ambayo Mahakama ilibaini ilifanywa bila ya kuzingatia sheria.

Akisikiliza maombi hayo jana, Jaji Semistodes Kaijage alitaka kufahamu kama kipengele cha 10 cha Kanuni za Mahakama ya Rufaa ya 2000 kilichotumika kuyawasilisha kilikuwa kinaruhusu mahakama hiyo kusikiliza ombi hilo, lakini baada ya majadiliano na pande mbili, Wakili Mponda alikiri kuwa shauri hilo halifai kusikilizwa chini ya kifungu hicho.

Jaji Kaijage alisema ni lazima Mponda amridhishe kama kipengele cha sheria alichotumia kinawezesha mahakama kusikiliza ombi la kuongezewa muda ili BoT iweze kuwasilisha ombi la kuongezewa muda kuwasilisha taarifa ya kukata rufaa.

Wakili wa wafanyakazi 31 wa BoT, Barnaba Luguwa alimweleza Jaji Kaijage kuwa tatizo la upande wa BoT ni kung’ang’ania kanuni ya 10 badala ya kuangalia vipengele vingine vya sheria vinavyoweza kusaidia kumaliza mgogoro baina ya wateja wake na benki hiyo.

Chanzo: Mwananchi


=====

Mytake: Hivi serikali haiogopi Laana? Maana wazee wengi wanaoidai lazima waende kwanza mahakamani ndipo haki yao ipatikane, kupatikana ni kwa mbide.
Kwa maoni yangu huku ni kukosa shukrani, kama mtu anadai haki yake mpeni!
 
I

Islam005

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2008
Messages
2,635
Likes
1,116
Points
280
I

Islam005

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2008
2,635 1,116 280
Serikali ipo busy kununua bombadia nyingine, we tulia.
 
Mavipunda

Mavipunda

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Messages
5,138
Likes
4,035
Points
280
Mavipunda

Mavipunda

JF-Expert Member
Joined Jun 27, 2012
5,138 4,035 280
mahakama ni chombo cha kutoa haki
 
K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Messages
1,691
Likes
2,210
Points
280
K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2013
1,691 2,210 280
mahakama ni chombo cha kutoa haki
Sasa si kesi imeshaamuliwa na mahakama, kama vipi wapewe chao au warudishwe kazini.
Unakumbuka ishu ya wazee wa East Africa Community?
 
Blood of Jesus

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Messages
640
Likes
1,073
Points
180
Age
48
Blood of Jesus

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2016
640 1,073 180
Tanzania bhana!
 
B

Babati

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
31,760
Likes
25,214
Points
280
Age
33
B

Babati

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
31,760 25,214 280
Mawakili wababaishaji kama hawa wanaisababishia hasara kubwa sana serikali, kuna tatizo gani kuwarudisha watanzania wenzako? badala ya kutoa ushauri mzuri kwenye menejimenti unakaa unapoteza muda pamoja na fedha za umma.
 
B

Babati

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
31,760
Likes
25,214
Points
280
Age
33
B

Babati

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
31,760 25,214 280
Serikali imebana OC sasa mawakili wamebuni njia nyingine ya kupata posho.
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
24,268
Likes
55,196
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
24,268 55,196 280
Wakae na hao watumishi wawalipe fidia yaishe
 
Pakawa

Pakawa

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
4,848
Likes
5,755
Points
280
Pakawa

Pakawa

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
4,848 5,755 280
Wakae na hao watumishi wawalipe fidia yaishe
Mkuu hili haliwezi kutokea. Watazungushwa miaka itazidi songa hawataambulia kitu. Kumbuka wafanyakazi wa East Africa Community. Utakuwa mchezo wa mahakamani tuuuuuuu!!
 
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
58,032
Likes
55,324
Points
280
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
58,032 55,324 280
Jaribio la kupinga hukumu ya kuwarejesha kazini wafanyakazi 31 waliopunguzwa kazi mwaka 1993 , limekwama tena baada ya mahakama ya rufani kutupilia mbali maombi ya BOT ya kuongezewa muda wa kukata rufani .

Chanzo - Mwananchi

Mytake - Hakuna haja ya BOT kupoteza muda , waamue moja , kuwalipa wahusika stahili zao au wawarejeshe kazini kama ilivyoamriwa na Mahakama .

Mnatesa raia wenu makusudi kwa faida ya nani ?
 
Mwanga Lutila

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2016
Messages
2,863
Likes
7,082
Points
280
Mwanga Lutila

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2016
2,863 7,082 280
Kuwarejesha kazini haitawezekana, wawape tu stahiki zao.
 
M

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2013
Messages
8,090
Likes
18,535
Points
280
M

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2013
8,090 18,535 280
Hili suala BOT litazidi kuwadhalilisha.
 
B

blessings

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Messages
5,764
Likes
3,543
Points
280
B

blessings

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2012
5,764 3,543 280
Huto tuzee tuchawiii
 

Forum statistics

Threads 1,273,525
Members 490,428
Posts 30,484,172