Waliotemwa CCM wazawadiwa magari; aina ya V8; Siri ya Mukama kumrithi Makamba yabainika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliotemwa CCM wazawadiwa magari; aina ya V8; Siri ya Mukama kumrithi Makamba yabainika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 20, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tanzania Daima  KATIBU Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Luteni Yusuf Makamba na Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho, Philip Mangula, wamezawadiwa mashangingi mapya, aina ya V8, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

  Habari ambazo gazeti hili imezipata, zimesema kuwa magari hayo yametolewa na chama kwa watendaji hao wastaafu ili kuuenzi mchango wao.

  Wakati Makamba akiwa ameachiwa gari jipya alilokuwa akilitumia, Mangula amepewa gari jipya kabisa.

  Mbali ya Mangula na Makamba, Makatibu wa NEC kwenye sekretarieti nao wamepewa mashangingi mapya aina ya V8.

  Habari zinasema kuwa mashangingi hayo ndiyo yaliyotumika wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
  Mbali ya Katibu Mkuu, Willison Mkama na Naibu wake, John Chiligati, wengine waliopewa magari hayo kwa ajili ya shughuli zao za kuimarisha chama ni Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi), Januari Makamba (Siasa na Mambo ya Nje) na Lameck Mwigullu Mchemba (Uchumi na Fedha).
  Akizungumzia hali hiyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida kwa chama kuwaenzi watendaji wake.

  “Ni utararibu wa kawaida wa chama. Hata Mangula alipoondoka, gari alilokuwa akilitumia alikabidhiwa, lakini sasa limeharibika na chama kimeamua kumpa lingine, Makamba naye ameachiwa gari alilokuwa akilitunia,” alisema Nape.

  Mangula ambaye alienguliwa kwenye nafasi ya ukatibu mkuu, alitumikia nafasi hiyo kwa muda wa miaka kumi chini ya mwenyekiti wake, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa.

  Nafasi ya Mangula ilichukuliwa na Luteni Makamba ambaye ameitumikia nafasi hiyo kwa miaka sita hadi wiki iliyopita nafasi yake ilipochukuliwa na Mukama.

  Wakati huohuo, siri ya Rais Jakaya Kikwete kumteua Mukama kurithi mikoba ya Makamba, imebainika.

  Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa Mukama amepewa nafasi hiyo kwani ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa tume iliyoundwa kwa siri na Rais Kikwete kufanya tathmini ya Uchaguzi Mkuu na sababu za chama kupoteza umaarufu.

  Ripoti ya Mukama ambayo ilisheheni wanazuoni, ndiyo iliyopendekeza mabadiliko makubwa ya kujivua gamba kwa kuwavua baadhi ya viongozi kwenye nafasi zao na kupendekeza watuhumiwa wa ufisadi waliokifikisha chama mahala kilipo sasa, wajiondoe au wang’olewe baada ya miezi mitatu.

  “Mukama ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa tume hiyo na imekuja na mapendekezo mengi, hivyo Rais Kikwete ameamua ampe nafasi hiyo Mukama ili apate nafasi ya kuyatekeleza aliyoyapendekeza kwenye tume yake,” kilisema chanzo chetu cha habari.

  Mbali ya kupendekeza fumua fumua na kutaka mafisadi wang’olewe, mapendekezo mengine ya tume ya Mukama ni kutaka wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) wachaguliwe kutoka kwenye wilaya zao badala ya mkutano mkuu ili kukiweka chama karibu na wananchi. Pia kimependekeza utaratibu na vigezo vya kumpata mgombea wa kiti cha urais ambavyo ni tofauti na utaratibu wa zamani wa chama hicho.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  This is sickening; how CCM has all that money to provide services to their former Secretary General and V8 transportation?
   
 3. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  With V8 how are (especially Mangula and Makamba) they going to manage them? Very high fuel consumption, nothwithstanding maintenance costs. This can explain why ccm is the home of rich guys and not normal peasants and workers as it used to be in the past.
   
 4. MrNSSF

  MrNSSF Senior Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  chama kimeshita hatamu
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Balllliiin!!!!
   
 6. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mtashangaa sana, kina Mukama wakistaafu wataachiwa chopa. na kila mtoto wa kigogo CCM atapewa jet. Buzwag moja tu inalipia mafuta ya shangini mia plus kwa mwaka bila tabu
   
 7. C

  Chogo matata Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Chama cha majambazi hicho!
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwasababu wana vyanzo vya mapato... whether legitimate or not, whether legal or illegal hayo ni mambo mengine
   
 9. CHIMPANZEE

  CHIMPANZEE Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ni haki yao kuzawadiwa, wacha wafaidi matunda yetu sisi wanachama wao.
   
 10. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280

  Mangula yuko kwenye list ya Mafisadi already, hivyo hatuna haja ya kumjadili baada ya deal la EPA na uchaguzi. Ila Makamba kwa vile hajatajwa usifikiri hana kitu. CCM wote ni mafisadi. Sasa kama Kingunge mwenyewe kahusishwa kwenye madeal ya ufisadi unategemea nini kwa waliobaki??

  Kinachonishangaza mimi, ni January Makamba. Huyu bwana si tayari ana gari la ubunge na posho zote pamoja na za kamati. Sasa hilo shangingi jingine atalifanyia nini?? Kweli mwenye nacho huongezewa.
   
 11. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wanamuenzi Makamba kwa kuwa gamba!!!!!
  Ama kweli ukistaajabu ya Musa......!!!
   
 12. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acha kumtusi bibi yangu kuleee kijijini
   
 13. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  big no my brother. They are not that bad if you compare with the previous model. With 1vd- ftv v8 engine twin turbo the fuel consumption is 10.3 kms per liter. Ni kama rav 4 wakati zile za zamani ni 6 or 7 kms kwa lt. . And the service is cheaper if u compare to the old model. 9 lts of engine oil badala ya 10 lts kwa zile za zamani. So, they are cheaper to run than the old momel. Nawasilisha.
   
 14. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Makamba Family, Mungu awape nini tena?
   
 15. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ivi gamba unaweza liongezeya? damu ili liendelee kuishi
   
 16. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,412
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  ndio maana nape tangu amechaguliwa hajaufumba mdomo.utafikiri sie yeye aliekuwa akikemea ufisadi nafikiri alichokua akikitafuta kakipata
   
 17. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  hiiiiiiii balaaaaaaaaaaaaa.Ngoja nikadake kumbikumbi naona wanaruka kweli hapa bukoba mjini
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Baada ya kupita kipindi cha kama miezi 6 hivi JF itabidi tuangalia jinsi gani CCM kilivyo tofauti tangu Mukama amrithi Makamba ukatibu mkuu mwaka huu.
   
 19. D

  DENYO JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko ccm -magamba kuwatosa magamba wenzao
  nape, chiligati, na mkulu siku ile walitoka kwa mbwembwe sasa wananywea wenyewe hivi hawakujua kwamba mapacha watatu ndio walioshikiria ccm na ndio wanoendesha serikali ya kimtandao? Tofauti na chadema na slaa hakuna mtu mwingine mwenye ubavu wa kumtosa chenge anajua madudu mengi ten years as ag. Tofauti na chadema na slaa dr wa ukweli hakuna mwingine anaweza kumtosa mzee wmenye mvi amekamata kila kona ya ccm watavua wapi waache wapi? Amekamata hadi spika -kila konaaaaaaa ni mjanja huyu isipokuwa kwa chadema tu na dr slaa ndio maana alisema ccm iangalie sana arusha, tofauti na chadema na dr slaa nani anaweza kumnyoshea roast ni gwiji la magamba anajua kila kila kona akiguswa tu anafungulia -nape ajifunze sasa ataanza kuchukua chake mapema na kuanza kuwapamba. Kifo cha ccm hicho mbele pachungu nyuma pachungu waende wapi??????? Let them dissolve the party.
   
 20. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  naona kimeshika utamu
   
Loading...