Waliotembeza jeneza lenye bendera ya CCM wapandishwa kizimbani Tunduma

Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,420
Likes
31,651
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,420 31,651 280
Vijana wawili wamepandishwa jana kwenye Mahakama ya mwanzo ya Viwawa wilayani Mbozi kwa kosa la kutembeza jeneza lililofunikwa bendera ya chama cha mapinduzi pamoja na msalaba katika mji mdogo wa Tunduma baada ya kutangazwa ushindi wa kiti cha ubunge kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA jimbo la Mbozi Magharibi.
Waliopandishwa kizimbani ni Selemani Ibrahimu maarufu kama mwarabu na Maneno Halongo wote wakazi wa mji wa Tunduma.
Wakisomewa shitaka lao mbele ya Mh hakimu wa mahakama ya mwanzo Vwawa Ismail Karuta, mwendesha mashitaka wa polisi koplo Pascal Mkondya aliieleza mahakama kuwa mnamo Novemba 2 mwaka huu saa 7 mchana katika mji wa Tunduma watuhumiwa walibeba sanduku mfano wa jeneza na bendera ya CCM wakiimba nyimbo za mazishi kitendo ambacho kilikuwa cha uvunjifu wa amani.
Alisema chini ya sheria ya maadili ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani namba 124 ya 1985 sura ya 342 kifungu kidogo cha 2 d pamoja na tangazo la serikali namba 273 la agosti 2010 ambalo linakataza vitendo vyenye lengo la kudhalilisha ama kukikashifu chama kingine.
Pamoja na kukana shitaka hilo, washitakiwa hao walishindwa kutimiza masharti ya dhamana baada ya hakimu Ismail Karuta kuwataka kudhaminiwa na watu watatu ambao ni watumishi wa serikali pamoja fedha kwa maneno kiasi cha shilingi 500,000/=. Watuhumiwa walipelekwa mahabusu hadi novemba 17 kesi yao itakapoanza kusilikilizwa.
Source : Dannytwevetz Blog
 
mambo yameanza tayari
 
B

Babuyao

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2009
Messages
1,734
Likes
32
Points
145
B

Babuyao

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2009
1,734 32 145
Mbona hayo ni mambo maodgo bana? Uhuru wa kujieleza/kutoa mawazo uko wapi? Ni uonevu tu ccm hawa, aaaa!!
 
M

Msavila

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2007
Messages
403
Likes
21
Points
35
M

Msavila

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2007
403 21 35
Hiyo dhamana ina utata. Mfanya kazi gani wa serikali atakayemdhamini anayeshitakiwa kwa kukikosea adabu cahama tawala. Uchaguzi umekwisha tarehe 31.10 hivyo sheria inayotumika haina nguvu. Waachieni la sivyo mahakamasi huru!!
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,420
Likes
31,651
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,420 31,651 280
Hiyo dhamana ina utata. Mfanya kazi gani wa serikali atakayemdhamini anayeshitakiwa kwa kukikosea adabu cahama tawala. Uchaguzi umekwisha tarehe 31.10 hivyo sheria inayotumika haina nguvu. Waachieni la sivyo mahakamasi huru!!
hakimu unaweza kuta elimu yake nayo ya utata.......UPE
 
Forum statistics

Threads 1,237,927
Members 475,774
Posts 29,306,666