Kuna mtu anakumbukumbu na hii sheria kuwa ilishapata baraka za bunge kweri? Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.
1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.
2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.
Walisimamie kulipinga hili kwa nguvu zote,wafanyakazi wote tuwaunge mkono...lakini wap vyama vya wafanyakazi? Hawajalijua hili?Sijaona mtu akifariki inakuwaje au naye anasubiri 55 years? What a shame. Huu uwe mtaji kwa chadema kupata kura zaidi za wafanyakazi
Bila kuwa na sheria ya Unemployment Benefits (au inayofanana na hiyo) hili sio wazo zuri hata kidogo.
Ripoti ya CAG ilisema wazi Serikali imeshindwa kulipa mabilio ya pesa ilokopa kutoka NSSF au pale ilipodhamini mikopo kutoka NSSF. Ni NSSF wamejenga Udom, wamekopesha Gen Tyre, Daraja la Kigamboni nk.Mi nashaang'aa hii nchi inavyoendeshwa...
Hapa itakuwa hawa jamaa wa serikari wamechota hela kwenye hizo fund wakashindwa kurudisha wkt watu wanadai hela zao ndo wakaona waitungie sheria.
Du!ama kweli hii nchi!
Miaka michache iliopita niliamua kufanya maamuzi magumu. Nilichukua balance yangu NSSF nikakuta nina 8m, riba wameweka elfu 8! Yaani interst hairudishi hata kushuka thamani kwa shilingi! Baada ya 2yrs nikaacha kazi nikazoa milioni zangu nikaziwekeza mahali ambapo napata laki 8 kila mwezi, si haba.Huu ni wizi wa mchana kweupee!!Yaani nikiacha kazi kabla ya miaka 55 hela mnayonikata kila mwezi mnaichukua nyie?Au labda sijaelewa vizuri?
Zito kabwe, mnyika, nchemba, kingwangala etc najua mpo humu? Hili mlipitisha? Tunaomba majibu?
Na wengine mnaoingia kwa hidden ID's kweli haya ndo mambo mlipisha huko???
If yes it could be fair and balanced that you as well wait till that decaying age to rip the benefits associated with the expiry of tenure...........
Sadist's era.....................!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!?????????????????????
Huu utakuwa ni ujinga. Unaacha kazi kwa kutegemea 20% ya contributions zako ndio uendelezee kampuni!!!hili nipigo kwangu na kwajamii kwa ujumla nilipanga kuacha kazi za kuajiriwa mwisho mwa mwaka huu ili vijisenti vyangu viniwezeshe kuendeleza kijikampuni changu..daah wabunge hili mlilipitisha kweli
Sheria tayari imeshaanza kutumika. Wasubiri tu mpaka wafike 55 yrs voluntary au 60 yrs compulsary!Jana kumetokea mtafaruku mkubwa sana Mgodini Nzega. Kwani wafanyakazi wa Kampuni ya Caspian woote waliamua kuachakazi, kwa kuandika resignation ya 24hrs, wakarudisha mashine toka site na kurudi ofisini kumkabidhi mkuu wao hizo barua. Hii yote imetokana na taarifa hizi za SSRA, imesababisha Management ichanganyikiwe na Production ilisimama kwa masaa 3 hivi, na sasa Kampuni ya Resolute na Caspian zimetuma wawakilishi Dar ili Kupata ukweli juu ya hali halisi.
Nasikia huko Nzega taarifa zinasema eti SSRA, itaanza kuitumia sheria hii kuanzia tarehe 1 Oktoba 2012 ndo maana wafanyakazi huko Mgodini wameamua kuacha kazi sasa na kwenda kuchukua mafao yao kabla ya Oktoba Mosi.
Huu utakuwa ni ujinga. Unaacha kazi kwa kutegemea 20% ya contributions zako ndio uendelezee kampuni!!!
Hii sheria ya SSRA nimeipenda. Itasaidia sustainability ya mifuko yetu na pia wanaweza kuplan vizuri especially kwenye long term investmennts.