Waliosoma Political Science wana mchango gani kwenye siasa za nchini mwetu?

Mchango wao ni mkubwa ukitamburika pamoja nakutumika lkn inabidi ujuwe kuwa hapa bongo makaburasha hayatumiki sana hasa watawala wetu hawathamini usomi na tafiti za hawa tunabaki kuwasikiliza kwenye BBC,VOA,DW etc. Hila kitu ambacho twaweza sema wamewazalisha walimu wa Civics and GS wanafundisha shule za kata.
 
ningekuwa na madaraka ningepunguza kabisa idadi ya wanafunzi
wa baadhi ya hizi taaluma,hasa hiii ya political science......

ni mzigo na kuongeza wapiga porojo nchini......
 
tatizo la 3rd world ni kua maamuzi muhimu yanafanywa kisiasa na sio kisayansi. sijui hiyo political science ina science kiasi gani ndani yake. lakini ni wazi haitumiki ipasavyo. the boss, kama watu waliosoma agricultural engineering wanahesabu noti bank, acha vijana wajisomee ili walau wapige porojo za maana kidogo. niliwahi kuserviwa juice kwenye ndege na mtu aliyesoma veterinary medicine,nilichoka kabisa! namuuliza kulikoni,ananiambia inalipa! nchi inachosha hii!
 
Hakuna tofauti kati ya political science na Bussineess admin/Bcom..... nchi za wenzetu, political science ni degree very hot!! mashirika mengi hupendelea watu wenye political science degree, Polisci is not blah blah, we kaangalie prospectus halafu fananisha na Bcomm(mgt).
 
Political science haipatikani kwenye chuo chochote nje, tena wala haiana faida yoyote kwa taifa letu. Usikubali mwanao asome kozi za kijinga kama hizi
 
kwani huyu mh zitto kabwe alisomea nini pale ud na huyu mh john mnyika..
sio hicho unacho uliza..
 
Mkuu kwenye nchi yetu hata mainjinia, madaktari et al hawana umuhimu wowote, waamuzi wakuu wa kila jambo ni wanasiasa wenyewe. Taaluma iko nyuma ya siasa Tanzania.. Labda unifafanulie mchango unaohitaji kuuona wa political scientists ni upi haswa? Wanazuoni wa siasa nchini mwetu aidha hufariki ktk mazingira ya kutatanisha (H. Othman, S. Chachage,) au hutengwa na Serikali (M.Baregu) au hupuuzwa tu kila wanachosema...

kutokana na mikataba feki tuliyowahi kuingia kama nchi inabidi tuanze kuhoji mchango wa Wanasheria wetu? Kuporomoka kwa thamani ya Tsh tuhoji mchango wa wanauchumi wetu? Vifo vinavyoepukika mahospitalini tuhoji mchango wa madaktari wetu? Mgao wa umeme na barabara zisizopitika, tuhoji mchango wa wahandisi wetu?
 
ningekuwa na madaraka ningepunguza kabisa idadi ya wanafunzi
wa baadhi ya hizi taaluma,hasa hiii ya political science......

ni mzigo na kuongeza wapiga porojo nchini......

PS sio polojo, ni uchambuzi wa siasa za nchi na mafanikio yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Umhimu wao ni mkubwa hasa kwa wale wanaopenda kuutumia na iwapo wenye nguvu gvt wameridhia kuchukua mapendekezo yao. Tatizo hapa kwetu huwa tunapuuza mawazo ya political analysit, lakini tukiwaheshimu tunaweza kuwa na taifa ambalo ni zuri zaidi ya hili tulilonalo.

hapo kwako kwenye bolded kijani, sio kweli nadhani unachanganya kati ya mwanasiasa na mtaalamu wa masuala ya kisiasa. hawa ni watu wawili tofauti. Inawezekana kuwa mwanasiasa bila kuwa mtaalamu wa masuala ya kisiasa na mtaalamu wa masuala ya kisiasa akiwa mwanasiasa na akatumia weledi wake na akapewa support na wengine, atatupeleka mbele zaid
 
Mkuu kwenye nchi yetu hata mainjinia, madaktari et al hawana umuhimu wowote, waamuzi wakuu wa kila jambo ni wanasiasa wenyewe. Taaluma iko nyuma ya siasa Tanzania.. Labda unifafanulie mchango unaohitaji kuuona wa political scientists ni upi haswa? Wanazuoni wa siasa nchini mwetu aidha hufariki ktk mazingira ya kutatanisha (H. Othman, S. Chachage,) au hutengwa na Serikali (M.Baregu) au hupuuzwa tu kila wanachosema...

kutokana na mikataba feki tuliyowahi kuingia kama nchi inabidi tuanze kuhoji mchango wa Wanasheria wetu? Kuporomoka kwa thamani ya Tsh tuhoji mchango wa wanauchumi wetu? Vifo vinavyoepukika mahospitalini tuhoji mchango wa madaktari wetu? Mgao wa umeme na barabara zisizopitika, tuhoji mchango wa wahandisi wetu?

Tanzania hatuna wanasheria, tun watu waliosoma law concepts tu. Ndio maana hawana msaada wowote likija suala la kulinda rasilimali za watanzania.

katiba ya Tanzania, inatamka wazi kwamba, rasilimali za TAIFA, zitatumika tu kwa ajili ya kuwaletea wananchi wake maendeleo. Hali ilivyo ni tofauti. Mikataba ya madini mfano, imehusika katika kuwanyang'anya hata maeneo watu waliyokuwa wanayamiliki tangu enzi bila hata fidia na kupewa akina ROSTAM.

Nenda Geita, Shinyanga, Arusha, Mtwara, Mbeya, Tarime(musoma), Tabora na maeneo mengine uchimbaji madini unakoendelea. Angalia wakazi wamenufaika vipi na uchimbaji huo, utakuta zaidi ya kupata kibarua tena kisicho na bima, hawana lolote, wamegeuka wakimbizi na ombaomba licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa madini.
waliofanikisha dhuluma hii ni wanasiasa wa CCM wakisaidiana na watu waliosoma tu nadharia ya sheria na hivyo hawafai kuitwa wanasheria
 
Hakuna tofauti kati ya political science na Bussineess admin/Bcom..... nchi za wenzetu, political science ni degree very hot!! mashirika mengi hupendelea watu wenye political science degree, Polisci is not blah blah, we kaangalie prospectus halafu fananisha na Bcomm(mgt).

Degree za sheria je? Si ndo hao wapo maofisini field unakuta mtu yuko law school kwa maana keshagrajueti LLB lakini ukimwambia atengeneze mkataba simple tu wa upangishaji wa frame ya duka anachemka
 
kwani huyu mh zitto kabwe alisomea nini pale ud na huyu mh john mnyika..
sio hicho unacho uliza..

Zitto alisoma B.A.Economics ambapo alifanya option ya PS na SO kama sikosei but was well and fully influenced by the LATE Dr. CHACHAGE-The doctor of human brain-Head department ya Sociology and Cultural Anthropology
 
Political science haipatikani kwenye chuo chochote nje, tena wala haiana faida yoyote kwa taifa letu. Usikubali mwanao asome kozi za kijinga kama hizi
Are you serious1!!??
Kwa marekani kwa mfano, before journalism or Law school majority huchukua polisci.
Polisci haina tofauti na Bussiness Administration....we angalia syllabus za hizi degree, they all study the same things.
 
Zito hakuwahi ku opt SO department iliyokuwa chini ya chachage wakati huo, nilikuwa pale simkumbuki kumuona darasani kwetu zaidi ya kuonana nae kwenye siasa za nje na ndani ya chuo.....

Political Science yupo Martine Shigela ambaye ali opt Uchumi pia, huyu ni bosi wa UVCCM na mchango wake TUNAUONA ......
Mwenye macho haambiwi tazama, haihitaji degree kung'amua kuwa TZ ni taifa linalopuuza wasomi na kutukuza saaaana madesa ya wafadhili kuyatendea kazi kwa maendeleo yetu.......tulikuwa na wasomi wazuri ( chachage, prof othman nk) mchango wao tuliouona kwa kuandika vitabu na kwenye midahalo lakini SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA ....HUISHIWA KUPIGIWA MAKOFI NA WASOMI WENZAO, ama kubezwa na WANASIASA......bado tunaowazuri ila nao wanavunjwa moyo na trend y upuuziwaji wa taaluma iliyoko nji hii......wababaishaji WAMEPEWA NAFASI KUBWA hiii inazuia weledi kufanya mambo

mix with yours
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom