Waliosoma Political Science wana mchango gani kwenye siasa za nchini mwetu?

hiyo kozi kwa hapa Tanzania ndiyo Jembe hasa wale walioipata pale UDSM
ndani yake kuna vitu adimu na lukuki. nawashauri wanafunzi waisome sana hawatadanganyika kabisa
ndani ya political science unasoma...
  • democracy and economy
  • planning
  • local gment
  • human rights
  • public policy
usichezee kabisa hao watu ndio wanaowazunguka mawaziri, maraisi hata hizo kauli mbiu za vyama vya siasa wanatengeneza wao. hata propaganda wanapanga wao kaka. kama unajipanga kugombea mtafute unamweleza unataka kugombea wapi atakuelekeza mbinu. waulize waliowahi kugombea watakueleza makali yao. wao wanajua umwage sera ipi na wapi.
yaani hwa jamaa ni noooooooma
 
tatizo la 3rd world ni kua maamuzi muhimu yanafanywa kisiasa na sio kisayansi. sijui hiyo political science ina science kiasi gani ndani yake. lakini ni wazi haitumiki ipasavyo. the boss, kama watu waliosoma agricultural engineering wanahesabu noti bank, acha vijana wajisomee ili walau wapige porojo za maana kidogo. niliwahi kuserviwa juice kwenye ndege na mtu aliyesoma veterinary medicine,nilichoka kabisa! namuuliza kulikoni,ananiambia inalipa! nchi inachosha hii!

Umesema kweli King'asti wangu maana hii nchi lazima uwe mwendazimu kukabiliana na hizi hali jojo
 
jambo la kujihoji wanachofundisha ni rel au wanasoma tu historia za akina maxweber na mambo ya zaman ambayo kuyafanya kwasasa ni ngumu halafu democracy na multpartism hawapewi nafasi hawa watu
 
political science sio politics, politics inafanywa na wanasiasa na raia yeyote yule.
Umetokea wapi na wewe!! www ndo unayefanya mchango wa tuliosoma hii kozi pale kigamboni uonekane hauna maana
 
Mbona mnaongelea phdz na prof.Vipi undergraduate wao?Mimi ninawaona kuwa wanasaidia kufundisha uraia na gs mashuleni ili tuwe na raia wema....A.othuman alisoma ps wapi?r.i.p jamaa kasoma Law na DS tu.
 
Halafu unakuta mwanafunz a political science atapata mkopo 100% wakati wa engineering au daktari ananyimwa.
 
hakuna namna utaiepuka political science kwenye nchi yoyote ile duniani. yenyewe ni nini hasa? ni somo linalohusiana na dola, nchi, taifa, serikali, utawala, sera, asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi na taasisi kwa ujumla. ni somo linalojikita kwenye mifumo (structures).

wanafanya shughuli gani?
-utawala serikalini na sekta binafsi
-ushauri wa kitaalamu serikalini, watu binafsi mf wanasiasa na kwenye mashirika (consultancy)
-kujikita kwenye siasa wao wenyewe
- asasi za kiraia (civil society organizations)
- kwakuwa ps ni sehemu ya social sciences, usishangae ukawakuta benki, shuleni hata mahospitalini wakifanya kazi
-utawala wa rasilimali watu, hasa serikalini
nb. watu wa social sciences na law wana msingi mmoja, hivyo usishangae kuona Kabudi, mukandala na rwaitama wote wakichambua siasa ingawa wanatokea kwenye specialization tofauti
 
Hii kozi ilibidi kufutwa kabisa katika vyuo vikuu hapa nchini mbaya zaidi ina maprofesa wa kumwaga yaani kila mtu ni professa hapo UDSM
 
Mkuu kwenye nchi yetu hata mainjinia, madaktari et al hawana umuhimu wowote, waamuzi wakuu wa kila jambo ni wanasiasa wenyewe. Taaluma iko nyuma ya siasa Tanzania.. Labda unifafanulie mchango unaohitaji kuuona wa political scientists ni upi haswa? Wanazuoni wa siasa nchini mwetu aidha hufariki ktk mazingira ya kutatanisha (H. Othman, S. Chachage,) au hutengwa na Serikali (M.Baregu) au hupuuzwa tu kila wanachosema...

kutokana na mikataba feki tuliyowahi kuingia kama nchi inabidi tuanze kuhoji mchango wa Wanasheria wetu? Kuporomoka kwa thamani ya Tsh tuhoji mchango wa wanauchumi wetu? Vifo vinavyoepukika mahospitalini tuhoji mchango wa madaktari wetu? Mgao wa umeme na barabara zisizopitika, tuhoji mchango wa wahandisi wetu?

umetoa hoja ya msing sana kama watakuelewa.BIG UP
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom