Waliosoma na kufanya kazi nje ya Tanzania

Nashukuru akili ya uzalendo ilinitembelea mapema kabla shughuli ya kutafuta haijanikolea. I could waste good time kwenye uzalendo.
Jamii yetu bado sana tena sana. Kwa uzoefu kidogo nilionao naona tuna shida sio ndogo.

Diaspora hapa wanaongelea mambo ya siasa nzuri sijui huduma na kodi inavyotumika maana yake hawa wenzetu wameshatoka.
Hii dar ambayo haileweki kwa watanzania wengi ni mbingu. Achana na dar huko Tanzania kwenyewe ni balaa. Huko kuwa na shule kijijini bado ni bahati, zahanati yenye mfanyakazi mmoja bado ni bahati. Wanaoishi huko hata kuongelea siasa safi na haki zao na kulipa kodi ni ndoto.

Sasa kwa nini ujitese kuishi na watu ambao hata kuona ambacho wewe unaishi hata kwenye picha bado. Hii dar yenyewe inalazimishwa ifanane lakini watu ndo hao hao bado wanapanga barabarani bidhaa na rais karuhusu. Mkae huko mfurahie maisha sio kila siku kujikarahisha na mambo ambayo wenzio wanaona sawa.
 
Comments zenu kama hizi ndio zinawafanya baadhi ya watu humu wawaone nyie 'diaspora' mnajisikia ila mtu kama mimi ambae nimeishi huko na nimeona watu kama nyinyi wengi tu huwa sipati shida kuwasikia maneno yenu.

Haya mkuu baki peponi sisi wengine tumezzoea jehanamu yetu.

Kipi nimeongea ambacho TZ hakifanyiki?Maisha sio HELA tu bali kuwa na uhakika kama upo huru na hutendewi mabaya sababu tu hupatani na watawala!Leo hii tuna ona RC na DC wanatia hadi watumishi mahabusu!
Mwaka jana nikiwa home Dar niliwahi pelekwa polisi sababu nimekataa kuondoka nje ya geti la home wkt polisi walipo niamuru niingie ndani kwa madai saa nne usiku majambazi huchukua advantages ya watu kuwepo mitaani kufanya uhalifu
Saa nne nalazimishwa na Police niingie ndani,kuwaambia kama kwa sheria ipi raia mwema akatazwe kuwepo nje, wakanibeba kesho yake nikatoka bila hata ya kufikishwa Mahakamani!
Wananiachia wananiambia'hapa sio US,tii polisi'
 
Ndugu mleta uzi/thread, issue ya kurudi ama kutorudi ni mtambuka na haina sababu zinazofanana among individuals na kwa kuwa binadam tuna malengo tofauti, struggles za kufanya tufikie malengo ndo inaweza kuwa sababu ya kuendelea kubaki ugahaibuni or ama kurudi Bongo/tz. Mathalani, umestaafu kazi na hauna permanent residence permit...inabidi urudi Bongo unless otherwise...! kwa upande mwingine tuna wapendwa wetu Bongoland especially wazazi...lazima urudi tu! kuna wengine wanakuwa wamechoka lifestyle za ughaibuni na anatamani arejee Bongo! Nje ya tz ubaguzi is for real. na kuna wengine wanachoka hali hiyo, wanageuza gari kurudi Bongo!
 
Inaelekea wewe hujakatiza mipaka ya tz. Huko nje watu wanaishi kwa shida kuliko hapa kwetu. Nafikiri unawaona wakija huku kutafuta maisha sababu huku maisha sio ghali kama kwao
 
Mm nlikuwa najiapiza toka nipo chuo kuwa nikienda kusoma nje sirudi tz. Sasa nlipata nafasi ya kwenda kusoma nje ndo nikaijua nchi yangu nzuri na ni sehemu nzuri ya kuishi. Hasa nlipobakiwa na mwezi kurudi nlikuwa naona kama mwaka vile
 
Kimweri umesema ninasakama walioamua kuishi nje na kutorudi. Nimekuomba nioneshe post niliolazimisha mtu kurudi au kumsakama alieamua kuishi nje.

Post zangu nyingi ni kuwajibu wanaokandia Tz kama Sheriff na wengine.
 
Kwangu mimi, home is where I make my living! Kwa sasa hivi nyumbani ni hapa nilipo! Nikishastaafu ndio naweza kuamua kurudi, na nina uhakika vipensheni vyangu vinaweza kunifikia popote pale nitakapokuwa katika sayari hii! Haya mambo sijui ya "Home sweet home" wala hayanisumbui kwani nazuka wakati wowote ninaotaka!
 
Hii thread mleta mada alitaka kujua waliorudi ni nini kiliwafanya warudi kwenye nchi yenye shida kama hii ilhali wameweza kuji establish huko walipo lakini cha ajabu wengi wamejibu kwanini hawajarudi na kuleta maelezo meengi as if kuna mtu kawalazimisha warudi.
 
Mwisho wa siku Tanzania itajengwa na wa-Tanzania. Ni vyema waliosoma nje watumie elimu na maarifa waliyopata kubadilisha hali ya maisha nyumbani. Fanya mabadiliko kutumia exposure uliyopata. Unajenga nyumba usisubiri maji ya DAWASCO, weka utaratibu wa kukinga maji ya mvua na uyahifadhi. Weka umeme wa solar, vitu vidogo vinaleta tofauti kubwa.

Mkuu umenena ya maana sana.
Hawa jamaa wa chache wenye mbwe mbwe wanategemea Nani awajengee Tanzania ili iwe kama huko majuu.Wako WaTanzania wengi walikuwa huko majuu ambao wamerudi Na wanajenga nchi kimya kimya.
 
Hii thread mleta mada alitaka kujua waliorudi ni nini kiliwafanya warudi kwenye nchi yenye shida kama hii ilhali wameweza kuji establish huko walipo lakini cha ajabu wengi wamejibu kwanini hawajarudi na kuleta maelezo meengi as if kuna mtu kawalazimisha warudi.
Kwenye huu uzi nimegundua kuwa kuna watu ambao hawapendi shida kabisa na wamezoea kuishi kwenye mazingira ambayo watawala wanafuata haki na wajibu wao ndo hao ambao hawana mpango wa kurudi. Ila wale waliozoea shida na maisha ya kuonewa na kukandamizwa na watawala ndo wamerudi..
 
Ni vizuri kama umegundua hivyo. You are a genius.
 
Mkuu umenena ya maana sana.
Hawa jamaa wa chache wenye mbwe mbwe wanategemea Nani awajengee Tanzania ili iwe kama huko majuu.Wako WaTanzania wengi walikuwa huko majuu ambao wamerudi Na wanajenga nchi kimya kimya.
Wanachekesha hasa mtoa mada ambae anasema waliorudi ni waliozoea shida na kukandamizwa na watawala! Laughable.
 
Kwenye huu uzi nimegundua kuwa kuna watu ambao hawapendi shida kabisa na wamezoea kuishi kwenye mazingira ambayo watawala wanafuata haki na wajibu wao ndo hao ambao hawana mpango wa kurudi. Ila wale waliozoea shida na maisha ya kuonewa na kukandamizwa na watawala ndo wamerudi..

Bora umeliona hilo!
On top of that this Bashite saga is the biggest oxymoron for JPM to deal with.
May God bless him and Tanzania.
 
Back
Top Bottom