Waliosoma na kufanya kazi nje ya Tanzania

Yes, Mkuu! Unajisalimisha tu ER, hakuna atakayekunyima matibabu huko! Hawawezi wakakuacha ukawafia pale, vinginevyo wanajitafutia matatizo!

Na bila ya kusahau Medicare Au Obama care ambazo hospital nyingi tu unatibiwa
 
Jamani acheni mbwe mbwe.Kweni Tesla nini
Hapa Bongo mbona yako magari ya thamani kuliko Tesla.
Tesla model X is $35K model S $72K to $95K
Range Rover $65K to $90K.

Hapo nadhani umeimiss point inayoongelewa kuhusu Tesla! Tatizo sio uthamani wake, ni barabara. Kumbuka hii Tesla inajiendesha yenyewe!
 
Hapo nadhani umeimiss point inayoongelewa kuhusu Tesla! Tatizo sio uthamani wake, ni barabara. Kumbuka hii Tesla inajiendesha yenyewe!

Sawa Mkuu Lakini huyo jamaa mwenye mbwe mbwe Hajasema barabara mbovu ila mshangao wake Eti Tesla Dar!!!
Watu wachache kama hawa ndio wanafanya WaTanzania wanje waonekane waringaji Na dharau
 
Naelewa mtu yeyote akiamua kuishi tokyo,new york etc. Nisichoafiki ni mtu kujaribu kuonesha Tz ni kama jehanamu.
Huko ni zaidi ya JEHANAMU
RC anaweza ita waandishi wa habari,mbele ya makamanda wa Polisi anakutaja kama wewe ni drug dealer
Bila ushahidi hata mmoja!
DC anaweza kukutia mahabusu akiamua tu
DC Hapi wa Kndoni kamuweka jana mtumishi wa UMMA sababu hakupokea simu yake siku ya Jumapili
Lema yupo mahabusu mwezi wa 4 sasa kwa mashtaka ambayo yanaweza sikilizwa Mahakama ya Mwanzo na hukumu ukitiwa na hatia ni faini tu
Watu wapo mahabusu sababu tu walichora katuni ya Rais

Huko ni JEHANAM,huko hawaheshimu haki za msingi za kujieleza!
 
Comments zenu kama hizi ndio zinawafanya baadhi ya watu humu wawaone nyie 'diaspora' mnajisikia ila mtu kama mimi ambae nimeishi huko na nimeona watu kama nyinyi wengi tu huwa sipati shida kuwasikia maneno yenu.

Haya mkuu baki peponi sisi wengine tumezzoea jehanamu yetu.
 
Ukweli ndio huo Rondo!!!
DC akiamua uwe arrested you are fucked up!
Hiyo ni Jehanum tosha.
Leo hii hata tv na magazeti hayapo free kureport fair and balanced news
Imagine Mange ndio tegemeo la the voiceless!
 
Jamani acheni mbwe mbwe.Kweni Tesla nini
Hapa Bongo mbona yako magari ya thamani kuliko Tesla.
Tesla model X is $35K model S $72K to $95K
Range Rover $65K to $90K.
Tatizo kubwa sio jinsi gani miundombinu sio rafiki Tanzania..
 
Mwisho wa siku Tanzania itajengwa na wa-Tanzania. Ni vyema waliosoma nje watumie elimu na maarifa waliyopata kubadilisha hali ya maisha nyumbani. Fanya mabadiliko kutumia exposure uliyopata. Unajenga nyumba usisubiri maji ya DAWASCO, weka utaratibu wa kukinga maji ya mvua na uyahifadhi. Weka umeme wa solar, vitu vidogo vinaleta tofauti kubwa.
 
I wish wangekusikia! Huku ni ubabe tuuu
 
Mkuu naona mnafanya kuwa TZ mtu huwezi kuishi kabisa. Ni kweli barabara,elimu,afya huwezi kulinganisha na first world lakini picha mnayoonesha kupitia comments zenu ni kama jehanamu.

Mbona kuna watu wana uwezo kuliko mamilioni ya watu USA na wanaishi TZ? Tena wengine wana option ya kuamua kuishi USA/UK au Tz ila wameamua kukaa TZ.

Mimi mwenyewe nina option ya kuishi UK au TZ lakini nime opt Tz, kila mtu anamaamuzi yake kuishi atakapo ila kujaribu kuonesha TZ ni kama jehanamu si sawa na inasikitisha kama anaefanya hivyo kazaliwa TZ na ameenda abroad ukubwani, at least kama ulizaliwa huko ukaja Tz mzee.

Bila kuwa offended, naomba unitajie kijiji anachotoka babu yako mzaa baba Tanzania.Ukishakipata jibu maswali yafuatayo. Usiwe mnafki au usidanganye. Yeyote anayehoji kuhusu diaspora kubaki nje maswali haya yanamhusu pia.

  1. Unaishi hicho kijiji sasa hivi? Kwanini hauishi huko?
  2. Sababu gani zinakuzuia kuishi kwenye hicho kijiji?
  3. Unakwenda kwenye hicho kijiji mara ngapi kwa mwaka?ukienda unakaa muda gani?
  4. Kama unakaa chini ya mwezi, kwa nini kijijini kwenu, iliko asili yako hukupendi kiasi cha kukaa muda mfupi kiasi hicho?
  5. Ni sawa nisipokuita mzalendo?kwa sababu tu hukai muda mrefu kijijini kwenu iliko asili yako?
  6. Kazi unayoifanya sasa hivi ukirudi kijijini kwenu utaendelea kuifanya?mshahara unaoupata utaendelea kuupata kwa kiwango hicho hicho ukifanya shughuli nyengine huko kijijini kwa babu zako?watoto wako watakwenda shule zilezile ulizoziacha Dar?watakwenda kwenye recreationals ulizoziacha Dar?
Kama kwenye haya maswali majibu yako mengi ni NO., Basi acha kusakama diaspora kwa nini hawarudi TZ. wana sababu zao binafsi, ambazo zinaweza kufanana kweli kweli na sababu za wewe kung'ang'ania Dar,Dodoma, Arusha, Mwanza etc.

Dar yako ndio NY yetu, Mwanza yako ndio London yetu, Arusha yako ndio Tokyo yetu. tofauti ni majina na umbali, sababu hazitofatiani. Jukumu la kutafutia familia zetu kipato na maisha bora ni swala binafsi. Sio la nchi au serikali, jukumu la kufurahia maisha popote tulipo ni jukumu binafsi pia. Tusichanganye vitu.
 
Kuna watu wanajinasibisha kuwa wazalendo, lakini kuanzia asubuhi hadi wanalala ni kuchukua rushwa tuuuuu.., Uzalendo gani sasa huo? wewe unayenyima watu haki zao siku nzima unajiitaje mzalendo wa nchi yako? Uzalendo sio kuwa stuck sehemu moja miaka nenda rudi. Huko ni kukosa options. Na kwa wachache wenye options,ni uvivu au mazoea, has nothing to do with uzalendo.

Kuna wazalendo wa nchi yetu lakini kutwa wanazurula sehemu mbalimbali duniani.
 
Kimweri hebu nioneshe mahali ambapo nimemsakama mtu arudi au ambae haraki kurudi.

Labda nikwambie tu kifupi msimamo wangu, sijali mtu aishi popote atakapo coz i've been there done that! Ila nashangazwa na mtu aliekwenda Ulaya/US halafu anashinda mitandaoni kutukana na kudharau alipotoka.

Sijalazimisha mtu kurudi coz sio mimi niliekupeleka wala sijui kwanini hutaki kurudi ila kuja humu jf na kuanza kuponda TZ kisa mmefika ulaya/usa nawashangaa tu.

Post yangu ya kwanza niliandika kwanini niliamua kurudi na kuishi Tz ila nyingi zilizofuata zilikuwa ni kwanini watu hawataki kurudi kitu ambacho mleta mada hakuuliza! Kauliza waliorudi walopata courage gani as anajua vizuri kwanino hamrudi.

Na mleta mada alikuwa anataka kusikia mnachokosema nyinyi kuwa TZ is hell hapafai kuishi kabisa.

Ishi unapotaka ila kuja jf kukandia TZ mlikotoka wengine kama mimi tunawashangaa kwasababu tipo hapa tunaishi na tuna enjoy maisha,tena wengine tukitaks kurudi huko tunarudi anytime ni uamuzi tu.
 
Back
Top Bottom