Luqman mohamedy
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 892
- 1,226
Habari wanaJF
Nia ya kuandika uzi huu ni kuondoa fikra mgando kuwa waliosoma enzi za Mwalimu walipata shida kuliko waliosoma enzi za ruksa na kuendelea.
Hizi ndizo sababu za kubeba hoja yangu
(1) Kwa Miaka ya kuanzia 60-80 idadi ya watu ilikuwa kidogo, japo ya uchache wa taasisi za elimu ila kila mmoja mwenye nia na muamko wa kusoma aliweza kupata nafasi. Kilichokuwa kinahitajika ni juhudi binafsi tu na wachache waliokomaa walitoboa.
(2) Kwa miaka ya 60-70 elimu ya juu ilikuwa ikitolewa bure kabisa ukilinganisha na hii miaka ya karibuni elimu imegeuka pesa, kama huna pesa basi elimu utaisikia tu kwahiyo wasomi wengi wamekuwa wakipata misukosuko inayowapa msongo wa mawazo kipindi cha masomo yao na kushindwa kuzingatia masomo yao.
(3) Kwa miaka ya 60-70 ajira baada ya elimu ilikuwa ni uhakika, kwahiyo waliokuwa masomoni kwa kipindi hicho hawakuwa na wasiwasi kabisa wa ajira baada ya masomo, ukilinganisha na miaka ya sasa wasomi wengi wamekuwa wakisoma na stress za wapi wataelekea baada ya masomo yao.
(4) Kwa miaka 60-70 ubora wa elimu uliweza kudhibitiwa sababu ya uchache wa taasisi za elimu, kwahiyo wasomi wengi walitoka wakiwa na ubora mmoja.
Tofauti na sasa ubora wa elimu unategemeana na bajeti ya taasisi utayoenda na kuna taasisi ukizipita elimu yako inadharauliwa.
Hizo ndizo baadhi ya hoja zangu zikipingana na kauli ya wengi wakidai vijana wa sasa wanasoma kwa raha sababu pekee ikiwa ni teknolojia, kazi kurahisishwa na computer.
Kama utapingana nami unaruhusiwa kupinga kwa hoja sio kejeli.
Karibu na hoja yako
Sent using Jamii Forums mobile app