Waliosoma Jitegemee Secondary School hebu ingieni hapa Tusalimiane

Mtamile

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
2,838
1,266
1782097_705481902815942_1692643582_a.jpg


Salaam kwa wote mliowahi kusoma Shule ya Sekondari ya Jitegemee lengo la uzi huu ni kusalimiana na kukumbushana vitu vizuri na vya kipekee vinavyopatikana/vilivyokuwa vinapatikana shuleni Jitegemee
binafsi nakumbuka sana vitu vifuatavyo
1. Mkungu Tree: Huu ni mti unaotumiwa sana kwa ajili ya kufanyia vikao na School baraza
2. Uwanja wa damu: hapa ndo pale kwata huwa inafanyikia
3. Smart Area: ukifika hapa utake usitake lazima ukimbie
4. Sanga Hall: haa hapa ndo sehemu ya kupatia chakula kwa wanafunzi wa hostel

Watu amabao siwezi kuwasahau ni Pamoja na Ndyamkama, Mbwenge, Afande Tall, Afande Kajimala, Wajadi(huyu kwa
waliokaa Hostel hadi miaka ya 2007 nadhani wanajua habari zake)
unaweza ukaongezea unachokikumbuka zaidi ukiwa Jitegemee Sekondari

311673_270206636340676_973946217_n.jpg


smart area
hapo ni mwendo wa kukimbia kwa kwenda mbele


Matokeo ya Form Four 2013

1507560_644296325637440_280352885_n.jpg


Kwa Kirefu tazama HAPA

Matokeo ya form six 2014

10362625_723118197755252_4964209227340446984_n.jpg
 
Jitegemeee Secondary School I love you
Wajadi, Mama Lyimo, Mwalimu Mnzava wa Biology. Bwenge, Ndyamukama na Head master wakati huo akiwa Massawe bana
Smart Area na kwata la pale uwanjani linafanyika mwezi mzima kwa form one na form five na wahamiaji wote wa ile shule
Ila Jitegemee ilikuwa miaka ya Massawe na akina Bwenge bana
Nyuma ya ofisi kuna sehem ya chips mayai na chips maini kwa watoto wa kishua na wali maharage kwenye mabada ya bati kwa watoto wauswahilini sijui kama bado yale mabanda ya mabati yapo siku hizi
 
Mr Rocky,


Dah mmenikumbusha kitambo nyie raia. Kuna afande mmoja alikua anaitwa Bruno jamaa alinitupiaga stick ya kichwa kisa Mwalimu Mleli kamuambia anishughulikie, nikaona hapa jamaa ataniua nikatoka nduki mbaya smart Area pale nilikipia speed ya hatari kama Hussein Bolt. Ticha Mleli akaanza kupiga kelele kama za mwizi vile maafande wote wakaniungia na stick kama mia nane ivi mikononi.

Nilitoka nduki kufika mbele wakamshtua Kamanda wao wa Mbio anaaitwa Afande Kiimbi (RIP), ebana jamaa anatoka nduki yule sijawahi ona...dakika sifuri niko mikononi mwa maafande...Kilichotokea............Tega sikio Part II. Tehe tehe

Jitegemee Sec.(JIte-Wute )Member 1996-1999
 
mimi nmesoma jkt kipindi mkuu wa shule akiwa ni Mkisi....

Mkisi alikuwa brothermen wa kufa mtu, alikuja akiwa na nyota mbili, akapewa civics form three dah tuliandika maumivu jamani, yaani kila saa misifa tuuu, alikuwa na sister ake hivi sasa ukatae adhabu ya sister ake, Lilikuwa linasema tu Afande waleo jasho hao, kiama mtakiona...

jiteute member 1997-2000
 
Afande Bruno Namkumbuka sana kwenye Kwata daaah wewe acha tu nimesoma pale kuanzia Form one hadi Six ,Nimemaliza form six 2004(EGM) .Nakumbuka sana Mkisi Program daaah alikuwa anatumbonda mbaya ,Nakumbuka siku moja alikuja kutupiga mikwaju class ,mshikaji mmoja anaitwa Gwamaka alipigwa mbaya na Mkisi daaaahhhh wewe acha tu.
 
Wakunyuti,

Ha! Ha! Ha! Mkuu nimecheka balaaa na sibanduki hapa hadi niione hiyi part II.

Huyo afande Bruno alikuja kuwa Patron baada ya Wajadi kuondoka halafu alikuwa ni muoga sana akishajua babaako ni Afande mwenye cheo kikubwa
 
oyaa watu wa jiteutee/jite-wutang niaje?hivi yule mwl checbob na mkongwe ktk kuuza ma pastpaper yupo?.nakumbuka tulikuwa tunamuita ticha madilu cos he was some sort of a madilu system wannabe kuanzia uvaaji mpaka ukataji wa nywele.ila alikuwa mmoja kati ya walimu mwenye urafiki na ukaribu sana na wanafunzi wa from four,five na six.halafu miaka ile ya 2000 kulikuwa na madogo wawili mapacha na watukutu sana,surname yao ni CHACHA.wako wapi sasa hivi.kwa zile hussle zao sitashangaa nikisia ni wamekuwa mapunda au mazungu wa unga.
 
hahaha Wakunyuti hiyo part II hata mimi sibanduki,lazima nijue mwisho wake.
 
Last edited by a moderator:
Member wa Jitegemee kuanzia 1993 mpaka 1996
Mkisi kaanzia siku nyingi kufundisha civics na misifa yake
Wakati tunasoma pale Bwenge alikuwa na binti yake anasoma palepale
 
Kuna huyu afande huwa anajifanya mbabe sana anaitwa Kajimara ukizinguana naye anakutishi kukuwekea bangi sijui bado yupo?
 
Aisee...wapi watoto wa mwakyambiki?!! Hahahaa...waliokuwa wanatoroka after prepo kwenda mwankenja kwa maduu.

Kimbe mbe ni siku ya jumamosi inspection for hostellers...hahahahahahaaa...wenye madem zao viranja sasa!!!
 
Afande Bruno Namkumbuka sana kwenye Kwata daaah wewe acha tu nimesoma pale kuanzia Form one hadi Six ,Nimemaliza form six 2004(EGM) .Nakumbuka sana Mkisi Program daaah alikuwa anatumbonda mbaya ,Nakumbuka siku moja alikuja kutupiga mikwaju class ,mshikaji mmoja anaitwa Gwamaka alipigwa mbaya na Mkisi daaaahhhh wewe acha tu.

Mkisi program umenikumbusha mbali alikuwa anapita class chezea sana kichurachura na kushimva mashimbo ya uchafu
 
By the way, concerts za waitara hall, makuti...hahahahahaa...afande tall na bruno, kajimala...walikuwa wanakaba sasa...vijana wa hostel walikuwa wakipata upenyo wanabambia hadi rege...chezea ugwadu.
 
Aisee...wapi watoto wa mwakyambiki?!! Hahahaa...waliokuwa wanatoroka after prepo kwenda mwankenja kwa maduu.

Kimbe mbe ni siku ya jumamosi inspection for hostellers...hahahahahahaaa...wenye madem zao viranja sasa!!!

Mkuu unakumbuka mwisho wa ukuta karibia na bweni la Makame ndo palikuwa pa kurukia ukuta
 
Hahahaa....kwenye ule mstimu mkabala na ukuta wa salvation...nimekula sana flight hapo...yaani palikuwa kama main gate kwa sie watoto wa hostel miaka hiyo.
 
Alipo rithi mikoba ya Kiswaga akaanza kuja na bodyguard na afande Ismail...na kamsemo kake ka P power five...prior preparations prevents poor performance...
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom