Waliosoma enzi za Mwalimu wanaenzi Mema ya Mwl. Nyerere...!!!!??

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Asilimia kubwa ya Viongozi na mawaziri walisomeshwa bure na Mwalimu Nyerere.

Mwalimu aliona umuhimu wa kupigana na adui Ujinga na elimu ndo ukombozi wa kiuchumi na kuleta maendeleo kwa taifa lolote.

Asilimia kubwa ya Wakenya wamesoma na wamepata elimu bora kuliko sisi watanzania. Sasa hivi ki elimu Tanzania inarudi nyuma. Kwa kigezo cha ubora wa elimu ya msingi na secondari. Huwezi kujenga vyuo vikuu vingi wakati msingi wa elimu ni dhaifu, hivyo vijana wengi wanamaliza vyuo vikuu si competitive na hawajiamini, hawana gut ya kuthubutu biashara especially katika soko la East Africa community.

Ila Nashangaa kwa nini serikali inashindwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa Vyuo?? sembuse kuwomesha Burrreee!!!

Kwa nini serikali ya Nyinyiem haitaki kuboresha elimu ya msingi na secondari? Hakuna maabara, hakuna library, vitabu havitoshi, msongamano darasani.

Mbaya zaidi madai ya waalimu hayazingatiwi na hivyo waalimu wamekosa moyo.

Matokeo yake failure darasa la saba na form 4 ni kubwa

Badala yake viongozi Nyinyiem wako bize na michongo ya kupora rasili mali za taifa kama pembe za ndovu Hongkong, wanyama hai Qatar, Madini, Tanzanite, na kupelekwa pesa Uswissiii

Jadililini kama Hii siku ya Uhuru ina manufaa ama maigizo tu.
 
Back
Top Bottom