Walioshiriki kampeni walikuwa wengi sana lakini wapiga kura ni kidogo sana

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Ukiangalia takwimu za waliojiandikisha na waliopiga kura tofauti ni kubwa sana na pia ukiangalia waliokuwa wanashiriki katika kampeni na waliopiga kura idadi iko tofauti sana.

Sasa naanza kukumbuka ule utitiri wa watu wakati wa kampeni za mwaka 2015 kwa Dr Maguli na kwa Mh Lowassa yale mafuriko yalikuwa yanatisha sana.

Imekuwaje idadi ya waliopiga kura imekuwa kidogo kiasi hiki?
 
Miaka yote ndivyo ilivyo. Sio watuwote watakao jiandikisha ndio watakao piga kura.
 
Tunaogopa kufa tunafamilia zinatutemea.

Ashinde mnyika ashinde mtulia ashinde mwalimu hakuna anaekuletea ugali mezani.
 
Kwa risasi zilizorindima jana unadhani watu wangekuja kupiga kura leo
 
Kwa risasi zilizorindima jana unadhani watu wangekuja kupiga kura leo
Mbowe kwenye kampeni zake si aliwaambia Polisi kuwa safari hawatakubali na wako tayari kufa....
 
Watanzania walio wengi siasa hazina tija kwao na haziwahusu. Sana sana huwa wajitokeza kwa uchaguzi wa rais kwani huyo ndiye anawahusu. Na ukiwa na siasa za matusi na za vurugu ndiyo sahau kabisa watanzania kukuchagua.
 
ok
 
Back
Top Bottom