Waliosaidia viongozi wastaafu kudukuliwa walipata faida gani?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,571
217,926
Tulishaona na kusikia humu humu JF sauti na video za kutengeneza zilizowahusu viongozi wa sasa na viongozi wastaafu waliodukuliwa huku wakidaiwa kumsengenya Aliyekuwa Rais wa Tanzania, ambaye sasa anaitwa mwendazake.

Wako waliojitokeza kuomba radhi, huku wengine wakitimuliwa kwenye Chama, majina yao yanafahamika na wala hatuna haja ya kuyarudia, Kwa mujibu wa sheria za Tanzania kudukua ni kosa kubwa kisheria, japo wadukuaji hao hawakushitakiwa kwa mjumbe wa nyumba 10, serikali za mitaa ama mahakamani (japo naamini iko siku watadakwa na kushitakiwa).

Sasa swali langu ni hili, wadukuaji hao ambao wanafahamu makosa yao tangu mwanzo je walilipwa nini hadi kukubali kutumika kijinai ? Haya sasa mwenda chini hayupo watakuwa tayari kuomba radhi hadharani kwa makosa yao?

Nakala: Cheusi Mangala
 
Mimi namshangaa sana Kikwete,

Yaani Mkewe au Former First Lady Kwa miaka kumi Kwa Sasa ni Mbunge.

Mwanae wa Kwanza ni Mbunge.

Yeye Kikwete anapokea mshahara wa Rais aliyepo madarakani Kwa asilimia 80%.

Wachana na Ulinzi.

Sasa wakuu tukisema Kikwete ni mbinafsi tutakua tunakosea?
 
Mimi namshangaa sana Kikwete,

Yaani Mkewe au Former First Lady Kwa miaka kumi Kwa Sasa ni Mbunge.
Khaa kwa hiyo ulitaka Ridhiwan asitimize ndoto zake za KISIASA kwa kuwa tu ni mtoto wa RAIS Mstaafu?

Mama Salma Kikwete alimlazimisha hayati Magufuli kumteua Ubunge?

Na kiheshima ulitaka amkatalie Rais asiende kutumika bungeni?

Viongozi wengi watoto wao na ndugu zao ni WANASIASA NA WATENDAJI WAKUBWA TU...Wana haki zote kwani KATIBA YA NCHI haiwazuii.

Mshahara wa 80% haukuwekwa na Rais Kikwete....uko KISHERIA NA KITARATIBU YA WASTAAFU WA NGAZI YAKE.

#KaziIendelee
#NchiKwanza
 
Mkuu,ukichunguza vizuri utagundua mtandao wa voda kwa sasa unapitia wakati mgumu sana kiuchumi. Hii ni kwa sababu ya kujiingiza kwenye mambo ya kijinga Kama hayo ya udukuaji.

Ule msukule uliokua unawapa sapoti haupo Tena. Wamejiondoa kwenye sapoti ya ligi ambayo hii ni dalili ya Kwanza ya kuondoka Tanzania. Time Will tell after all, its the best judge ever!

 
Mimi namshangaa sana Kikwete,

Yaani Mkewe au Former First Lady Kwa miaka kumi Kwa Sasa ni Mbunge.

Mwanae wa Kwanza ni Mbunge,

Yeye Kikwete anapokea mshahara wa Rais aliyepo madarakani Kwa asilimia 80%.

Wachana na Ulinzi.

Sasa wakuu tukisema Kikwete ni mbinafsi tutakua tunakosea???
Kwakua ubunge wao n wa kupambana majimboni mm naona hakuna shida mkuu

Ndio demokrasia yenyewe
 
Kwakua ubunge wao n wa kupambana majimboni mm naona hakuna shida mkuu

Ndio demokrasia yenyewe
Shida ipo kubwa sana mkuu,

Kwanini Hawaigi mfano wa Baba wa Taifa??

Kwani Maria Nyerere alishindwa nae kugombea Ubunge??

Huko kujazana familia nzima kwenye utawala si ndio mwanzo wa kutengeneza matabaka ya watawala na watawaliwa.
 
Shida ipo kubwa sana mkuu,

Kwanini Hawaigi mfano wa Baba wa Taifa??

Kwani Maria Nyerere alishindwa nae kugombea Ubunge??

Huko kujazana familia nzima kwenye utawala si ndio mwanzo wa kutengeneza matabaka ya watawala na watawaliwa.
Katiba inawaruhusu mkuu Kama wangekuwa wamevunja katiba hapo n sawa

Mbona mzee mwinyi mwanae Rais na mwingine mbunge na katiba inawaruhusu
 
Back
Top Bottom