Waliosahaulika miongoni mwa wanaostahili kuwajibishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliosahaulika miongoni mwa wanaostahili kuwajibishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, May 5, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,965
  Likes Received: 37,515
  Trophy Points: 280
  Wafuatao nao wanastahili kuwajibika ama kwa uzembe au kwa kushiriki ufisadi huu:-

  (1)Mkurugenzi mkuu wa usalama wa Taifa
  Huyu anasimamia usalama gani kama nchi inaporwa na yeye yupo ofisini. Hivi kweli hakujua kinachoendelea na kama ndio mbona alikaa kimya? Tutafakari

  (2)Mkurugenzi mkuu TAKUKURU
  Hii kashifa ina harufu kali ya Rushwa ambapo ni wazi viongozi hawa(mawaziri) inawezekana walihongwa kwa mfano ugawaji wa vitalu vya kuwindia,utroshaji wanyamapori n.k.Lakini TAKUKURU imeshindwa kabisa kuzuia na hata kuchukua hatua baada ya wizi huu kufanyika na badala yake siku zote husubiri mambo yaibuke bungeni ndio waanzishe uchunguzi feki wa kutuzuga.

  (3)Mkuu wa jeshi la polisi nchin(IGP)
  Huyu bwana ni maarufu sana na intelijinsia ya maandamano ya kisiasa lakini nashangaa hiyo intelijinsia haipo kwenye ufisadi wa nchii hii.Hapa kuna kitu na si bure.Tujiulize hivi huko barabarani walikopitishwa hawa wanyama hakukuwa na trafiki polisi na kama ndio mbona walikaa kimya?Kuna something behind.

  Watanzania tusipoamka kama wenzetu wa Misri,Libya na kwingineko nchii hii itauzwa.
   
 2. m

  mangwela Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh inapendeza sana hasa tunapoanza kufikiri mbali zaidi ya hawa watanzania wenzetu ambao wamo kwenye kadhia hii.

  Ni wakati sasa kwa waandishi wa habari wa Tanzania kulifikiria taifa la Tanzania kwa mapana zaidi, waandishi andikeni zaidi ya taarifa ya CAG kwani kuna mengi yanayo endana sambamba na uozo wakwenye wizara zetu zaidi ya wimbo ambao wanasiasa wanataka tuuimbe pamoja nao.

  Naomba niende mbali zaidi kwani mpaka leo mkuu bado anaamini tatizo ni FITINA wizarani wakati kunajinai ya wazi imetendeka na inatakiwa watanzania kwa umoja wetu tumuwajibishe mkuu wa kaya na wala si kumng'ang'ania PINDA kama ambavyo tunaaminishwa japo kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae imekuwa ni kama catalyst mpaka kufika hapa tulipo.
   
 3. U

  Userne JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 895
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa itabidi wawajibike au wawajibishwe! Sababu; "Kama waliwajibika kwa kutoa taarifa kwa ngazi husika na hiyo ngazi haikuchukua hatua, ilikuwa wao wajiuzulu! kutojiuzulu kwao ina maana wameshiriki au kazi waliopewa hawaimudu!"
   
 4. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  naunga mkono hoja nzuri..
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wakuwajibishwa ni bosi wao(jei kei) maana yeye ndio aliyewachagua hao!!
   
 6. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapa umeona mbali sana mkuu. WATU hao uliowataja walipaswa kuwa wa kwanza kuwajibishwa. Upotevu na utumiaji mbaya wa resources zetu unatokana na kupwaya kwa taasisi hizo ulizozitaja.
   
Loading...