Waliopoteza ndugu hawawezi kuomba ushahidi USA ili wafungue kesi ICC?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,216
Nitangaze wazi kuwa taaluma ya sheria imenipita pembeni.

Ila hilo halinizuii kutaka kuelewa mimi na wale wote ambao wana ndugu zao wamepotea, wamejeruhiwa au kuuawa na hakuna hatua zozote zinazoonekana kuchukuliwa.

Serikali ya Marekani majuzi ilitoa tamko la kumtaja kiongozi mmoja (ambaye hata kabla tetesi zimemtaja) kuhusika na upotevu na uuaji wa watu walio kuwa itikadi tofauti naye.

Kwa vile baada ya tamko hilo ilitakiwa serikali iombe ushahidi huo toka USA kwa ajili kuchukua hatua na haikufanya hivyo, je inawezekana ndugu wa jamaa hao wote waliopotezwa au kushambuliwa (mfano Lissu) kuomba huo ushahidi na kuwapatia Prosecutors wa ICC washughulike na mtuhumiwa anayelindwa na utawala?

Au ni namna gani haki inatafutwa nje kama ndani inazuiwa?

Hili suala siyo la ushabiki wa kisiasa kwani naamini kama mkeo ni chama pinzani na cha kwako huwezi kutetea kama atauawa kwa sababu za aina yeyote kwa vile sio kada/shabiki wa chama chako, bali utataka haki itendeke.

Msaada tafadhali, kuipigania haki ni baraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GONGA LINK hapa>>>
 
MsemajiUkweli, Asante MsemajiUkweli kwa link. Lakini hoja yangu ni wahusika kuomba ushahidi huo kutoka US bila wao US kujali tunautumia wapi. Ukiangalia wao wamekataa kuitambua mahakama hiyo kushughulikia matters concerning citizens of USA sidhani kama kutoa ushahidi kuwapa wengine wautumie huko kama inagomba hiyo mkuu.

Hata hivyo jambo hilo ni la faida kwetu Watanzania na hata kwa huyo kiongozi aliyetajwa kwani kama ushahidi huo ni magumashi basi atakuwa amesafishwa na nchi imesafishwa na tuhuma hizo.
Au nini mawazo yako? Kama nilivyosema pale awali, jambo hili sio la kiitikadi bali ni jinai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani hawaitambui mahakama ya ICC na hawaitaki hata kuisikia na walishaipiga marufuku kufanya shughuli zake Marekani iwe kutafuta ushahidi au chochote marekani
Kama hawaitambui kwa nini wanatoa mchango wa fedha mkubwa kuliko nchi nyingine yeyote kuiendesha hiyo ICC?

Basically wanaitambua ila haina juridiction nchini kwao. Yaani hawawezi kwenda kumkamata George Bush kwa mauaji ya wa Iraq mwaka 2003
 
Asante MsemajiUkweli kwa link. Lakini hoja yangu ni wahusika kuomba ushahidi huo kutoka US bila wao US kujali tunautumia wapi. Ukiangalia wao wamekataa kuitambua mahakama hiyo kushughulikia matters concerning citizens of USA sidhani kama kutoa ushahidi kuwapa wengine wautumie huko kama inagomba hiyo mkuu.
Hata hivyo jambo hilo ni la faida kwetu Watanzania na hata kwa huyo kiongozi aliyetajwa kwani kama ushahidi huo ni magumashi basi atakuwa amesafishwa na nchi imesafishwa na tuhuma hizo.
Au nini mawazo yako? Kama nilivyosema pale awali, jambo hili sio la kiitikadi bali ni jinai.

Sent using Jamii Forums mobile app
ICC ni Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu inayotumika kushitaki uhalifu ikiwamo mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu, uhalifu wa kivita. Ilianzishwa kuisaidia kazi mifumo ya kitaifa ya mahakama za nchi tofauti.

Mahakama ya ICC inakuwa na mamlaka pale mahakama za kitaifa zinapokataa ama zinaposhindwa kufanya uchunguzi ama kuendesha mashitaka juu ya uhalifu wa aina hii. Zaidi nchi ya nchi 120 ni wanachama wa mahakama ya ICC. Takriban nchi 30 ikiwamo Urusi zimejiandikisha lakini bado hazikuridhia mkataba wa mahakama hiyo. Hata hivyo Israel, Sudan na Marekani wameamua kutojihusisha na mahakama hiyo.

Kwa kinachoendelea Tanzania tuna qualify kabisa kufikishwa kwenye mahakama ya ICC kwa vile vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu vipo na Serikali haijachukua hatua. Angalia mauaji ya akina Ben Saanane, Azory Gwanda, Kangoye, Diwani wa Hananasif CDM, Diwani wa Ifakara- CDM na mauaji ya watu zaidi ya 340 wa Mkuranga, Kibinti na Rufiji. Vivyo hivyo mashumbulizi dhidi ya Tundu Lissu, Huu ni uhalifu dhidi ya binadamu na hakuna chochote kilichofanywa na Serikali katika kutafuta wahusika na kuwakikisha kwenye vyombo vya sheria..

Kuhusu swali lako kuwa Je ndugu wanaweza kupeleka ushahidi? Kwanza siyo lazima ndugu wapeleke. Sheria inaruhusu mtu yeyote aliyeguswa apeleke mashtaka then ICC kupitia vyombo vyao wanafanya uchunguzi ndipo mashtaka yanakamilika.

Kwa mfano kuna wale Waislamu wa Rohingwa ambao yapata watu 740,000 wameuawa chini ya majeshi ya Serikali ya Myanmar. na wengine wamebakwa na malizo kuharibiwa na mwishowe wameondolewa kwenye makazi yao. Pamoja na suala kwamba Mayanmar siyo nchi iliyoridhia Itikaki ya Mahakama ya ICC, lakini tayari nchi hiyo imeshakuwa kwenye uchunguzizi wa vitendo hivyo dhidi ya binadamu.

Je ni nani aliyepeleka malalamiko ya waislamu wa Rohingya? Ni Serikali ya Gambia pamoja na nchi zingine 57 ambazo ni wanachama wa OIC (Organization of Islamic Conference ndiyo waliopeleka malalamiko. Kwa mara ya kwanza Aung San Suu Kyi alitokea kwenye Mahakama ya ICC tarehe 10-12/ 12/ 2019 kwenda kutoa utetezi pamaoja na jopo la wanasheria wa Maynmar. Soma hapa kwa maelezo ya ziada;

Kwa Tanzania ni suala la muda tu, sioni namna ya watawala wetu walioweka pamba masikioni juu ya kukandamiza haki za kiraia, kufanya utekaji na kufanya mauaji kama watakwepa ICC. Naamini mchakato umeanza bila wao kujua. Yaweza kuchukua miaka mingi lakini watu kama Paul Makonda, Lazro Mambosasa, Cyprian Musiba na hata Jiwe mwenyewe siyo rahisi kukwepa kikombe hiki.

Lakini nina wasiwasi kuwa wale waliokuwa wanawatuma kupiga mashine kama yule Herry Kisanduku aliyemtolea Nape Nnauye bastola, au Bwire wanaweza wakawauwa ikabla ili kuharibu ushahidi
 
Nitangaze wazi kuwa taaluma ya sheria imenipita pembeni.

Ila hilo halinizuii kutaka kuelewa mimi na wale wote ambao wana ndugu zao wamepotea, wamejeruhiwa au kuuawa na hakuna hatua zozote zinazoonekana kuchukuliwa.

Serikali ya Marekani majuzi ilitoa tamko la kumtaja kiongozi mmoja (ambaye hata kabla tetesi zimemtaja) kuhusika na upotevu na uuaji wa watu walio kuwa itikadi tofauti naye.

Kwa vile baada ya tamko hilo ilitakiwa serikali iombe ushahidi huo toka USA kwa ajili kuchukua hatua na haikufanya hivyo, je inawezekana ndugu wa jamaa hao wote waliopotezwa au kushambuliwa (mfano Lissu) kuomba huo ushahidi na kuwapatia Prosecutors wa ICC washughulike na mtuhumiwa anayelindwa na utawala?

Au ni namna gani haki inatafutwa nje kama ndani inazuiwa?

Hili suala siyo la ushabiki wa kisiasa kwani naamini kama mkeo ni chama pinzani na cha kwako huwezi kutetea kama atauawa kwa sababu za aina yeyote kwa vile sio kada/shabiki wa chama chako, bali utataka haki itendeke.

Msaada tafadhali, kuipigania haki ni baraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa watu wasiojulikana Hawakuchukua hatua zipasavyo,na wasipo chukua wakimaliza muda wao hata ikichikua miaka 6 ama zaidi hatua zitachuliwa tu 'no one is above the law'
 
MsemajiUkweli, Asante MsemajiUkweli kwa link. Lakini hoja yangu ni wahusika kuomba ushahidi huo kutoka US bila wao US kujali tunautumia wapi. Ukiangalia wao wamekataa kuitambua mahakama hiyo kushughulikia matters concerning citizens of USA sidhani kama kutoa ushahidi kuwapa wengine wautumie huko kama inagomba hiyo mkuu.

Hata hivyo jambo hilo ni la faida kwetu Watanzania na hata kwa huyo kiongozi aliyetajwa kwani kama ushahidi huo ni magumashi basi atakuwa amesafishwa na nchi imesafishwa na tuhuma hizo.
Au nini mawazo yako? Kama nilivyosema pale awali, jambo hili sio la kiitikadi bali ni jinai.

Sent using Jamii Forums mobile app
JF jamvi la vilaza kweli; soma basi hata Rome statute.
 
ICC ni Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu inayotumika kushitaki uhalifu ikiwamo mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu, uhalifu wa kivita. Ilianzishwa kuisaidia kazi mifumo ya kitaifa ya mahakama za nchi tofauti.

Mahakama ya ICC inakuwa na mamlaka pale mahakama za kitaifa zinapokataa ama zinaposhindwa kufanya uchunguzi ama kuendesha mashitaka juu ya uhalifu wa aina hii. Zaidi nchi ya nchi 120 ni wanachama wa mahakama ya ICC. Takriban nchi 30 ikiwamo Urusi zimejiandikisha lakini bado hazikuridhia mkataba wa mahakama hiyo. Hata hivyo Israel, Sudan na Marekani wameamua kutojihusisha na mahakama hiyo.

Kwa kinachoendelea Tanzania tuna qualify kabisa kufikishwa kwenye mahakama ya ICC kwa vile vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu vipo na Serikali haijachukua hatua. Angalia mauaji ya akina Ben Saanane, Azory Gwanda, Kangoye, Diwani wa Hananasif CDM, Diwani wa Ifakara- CDM na mauaji ya watu zaidi ya 340 wa Mkuranga, Kibinti na Rufiji. Vivyo hivyo mashumbulizi dhidi ya Tundu Lissu, Huu ni uhalifu dhidi ya binadamu na hakuna chochote kilichofanywa na Serikali katika kutafuta wahusika na kuwakikisha kwenye vyombo vya sheria..

Kuhusu swali lako kuwa Je ndugu wanaweza kupeleka ushahidi? Kwanza siyo lazima ndugu wapeleke. Sheria inaruhusu mtu yeyote aliyeguswa apeleke mashtaka then ICC kupitia vyombo vyao wanafanya uchunguzi ndipo mashtaka yanakamilika.

Kwa mfano kuna wale Waislamu wa Rohingwa ambao yapata watu 740,000 wameuawa chini ya majeshi ya Serikali ya Myanmar. na wengine wamebakwa na malizo kuharibiwa na mwishowe wameondolewa kwenye makazi yao. Pamoja na suala kwamba Mayanmar siyo nchi iliyoridhia Itikaki ya Mahakama ya ICC, lakini tayari nchi hiyo imeshakuwa kwenye uchunguzizi wa vitendo hivyo dhidi ya binadamu.

Je ni nani aliyepeleka malalamiko ya waislamu wa Rohingya? Ni Serikali ya Gambia pamoja na nchi zingine 57 ambazo ni wanachama wa OIC (Organization of Islamic Conference ndiyo waliopeleka malalamiko. Kwa mara ya kwanza Aung San Suu Kyi alitokea kwenye Mahakama ya ICC tarehe 10-12/ 12/ 2019 kwenda kutoa utetezi pamaoja na jopo la wanasheria wa Maynmar. Soma hapa kwa maelezo ya ziada;

Kwa Tanzania ni suala la muda tu, sioni namna ya watawala wetu walioweka pamba masikioni juu ya kukandamiza haki za kiraia, kufanya utekaji na kufanya mauaji kama watakwepa ICC. Naamini mchakato umeanza bila wao kujua. Yaweza kuchukua miaka mingi lakini watu kama Paul Makonda, Lazro Mambosasa, Cyprian Musiba na hata Jiwe mwenyewe siyo rahisi kukwepa kikombe hiki.

Lakini nina wasiwasi kuwa wale waliokuwa wanawatuma kupiga mashine kama yule Herry Kisanduku aliyemtolea Nape Nnauye bastola, au Bwire wanaweza wakawauwa ikabla ili kuharibu ushahidi
Mkuu Stuxnet asante sana kwa uchambuzi wako mzuri.
Kwamba kumbe mashtaka ICC yaweza kupelekwa na yeyote yakiwa thabiti, na kama nilivyosema hili suala sio la kiitikadi maana naamini kama kuna mauaji au uhalifu dhidi ya binadamu haujafanywa na CCM, Chadema au CUF bali na watu individual kwa kutumia madaraka yao basi tushikamane wote na taasisi zile za haki za binadamu zifungue mashtaka na zipate msaada wa ushahidi walio nao US.
Mfano Kenyatta na wenzake waliposhtakiwa lilikuwa suala lake na mambo ya nchi yaliendelea kama kawaida kwanini sisi mtu kama huyu aliyetajwa iwe big issue hadi serikali kufichaficha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JF jamvi la vilaza kweli; soma basi hata Rome statute.
Hata ukisoma utangulizi nimeeleza kuwa sheria sio fani yangu. Na thread iko katika mfumo wa kutaka kuelimika. Mpaka hapo tuu, mtu akisoma post yako anapata kuelewa kilaza ni nani hapo.
Ungekaa pembeni hapa hakuna uchama bali tunazungumzia haki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom