Waliopata div two ya 11 na ya 12 wakakosa vyuo, lazima TCU ijitafakari

kweli mkuu, lakini mfumo wetu wa elimu hautuandai hivyo, anayehitimu high school anakuwa na maarifa ya kujibia mitihani tu juu ya kile alichojifunza, hana elimu ya kujitegemea, angalau kwa hawa wa diploma na VETA wanaweza kutembea juu ya usemi huo
Upo sahihi mkuu, ila maarifa sahihi ya kuja kutatua changamoto kwenye jamii hayatoki darasani mkuu bali hujengwa kupitia darasani. Na pia lengo la elimu ytu ni kujua kusoma na kuandika tuu!!
 
hao unaowasema wana D mbili!??kinachohitajika ni principal 2 sio unapata B+ halafu E,E utegemee utaenda chuo, wewe kama umetoka form 6 vigezo ni principal 2 tuu,kama unazo principal na haujapata chuo jua umeapply kwenye ushindani zaidi na vigezo vyako havizidi vya wengine ndio maana umekosa.

Kaka ukiwa na B NA E UNAENDA CHUO,THATS MEANS PRINCIPLE PASS UNAZO B NI PRINCIPLE NA E NI PRINCIPLE
 
Kaka ukiwa na B NA E UNAENDA CHUO,THATS MEANS PRINCIPLE PASS UNAZO B NI PRINCIPLE NA E NI PRINCIPLE
whatever utakavoidefine hiyo principle ila kinachohitajika ni D mbili na sio hiyo ya B na E, mtu mwenye D mbili anaclear chance ya kupata chuo kuliko huyo mwenye B na E,
tatizo hamjaelewa hapa,serikali na vyuo imetengemeza system ambayo hiyo system inasoma na kupitisha only wenye kutimiza hizo D mbili kwahiyo wewe kama umepungukiwa moja system inakutema directly,haina swalia mtume....
 
Upo sahihi mkuu, ila maarifa sahihi ya kuja kutatua changamoto kwenye jamii hayatoki darasani mkuu bali hujengwa kupitia darasani. Na pia lengo la elimu ytu ni kujua kusoma na kuandika tuu!!
'you can't think beyond your education level' ni nukuu ya bwana mmoja,. sasa kama maarifa hatutayavuna kwenye institutions hizo ambazo ndivyo vyuo, tuvune wapi tena? lazma tukapate maarifa huko vyuoni yatakayo tuongoza katka kujitegemea. elimu ya kujitegemea haiko huku ktk level za chini ila vyuoni. kujua kusoma na kuandika tu hakutoshi katika mapambano ya dunia ya leo, tunahitaji upana wa fikra ili tujikwamue
 
Hv akina Isack Newton, Gallileo Gallillei & Albert Einstein mambo waliyo yagundua waliyasoma wapi zaid ya kupata basics tuu za masomo ya kawaida? Akina Ferrari, Suzuki, Fiat nao waliyasoma wapi hayo mambo waliyo gundua? akina Faradays nao je?

Msingi wa elimu ni kujua kusoma na kuandika, ndio maana baada ya hapo watu huchagua kitu gan wakajiendeleze nacho mbeleni
 
Kabla ya kulalamika jiulize haya maswali mawili.
1/Je, muombaji ana sifa stahiki kupata hiyo kozi katika hicho chuo?(VIGEZO)

2/Je, waliopata chuo na hizo kozi wana sifa gani za ufaulu?(USHINDANI)
 
Nina binti yangu ana division two ya kidato cha nne na ana division two ya 12 kidato cha Sita kombi ya CBG amekosa chuo awamu ya kwanza na ya pili kozi alizoomba ni education with science MUCE, DUCE na Main campus UDSM, education with science UDOM na SUA kozi za HUMAN NUTRITION, WILDLIFE, BIOTECHNOLOGY zote hizo wanamwandikia NOT SELECTED sasa sijui achague kozi gani ili awe SELECTED
Ni vyuo ndio havijamchagua sio TCU. Tunarudi pale pale, ushindani ni mkubwa sana vyuoni.
 
AJE TANZANIA INSTITUTE OF RAIL TECHNOLOGY (TIRTEC) ajisomee zake DIPLOMA OF LOCOMOTIVE ENGINEERING IN DIESEL ELECTRICAL mpaka amalize miaka 3 hiyo anakuja job kucheza na DIESEL ELECTRIC LOCOMOTIVES baadae anajiendeleza mwenyewe au hataki kufanya kazi kwenye SGR??
Kiko wapi na gharama zikoje?
 
Hv akina Isack Newton, Gallileo Gallillei & Albert Einstein mambo waliyo yagundua waliyasoma wapi zaid ya kupata basics tuu za masomo ya kawaida? Akina Ferrari, Suzuki, Fiat nao waliyasoma wapi hayo mambo waliyo gundua? akina Faradays nao je?

Msingi wa elimu ni kujua kusoma na kuandika, ndio maana baada ya hapo watu huchagua kitu gan wakajiendeleze nacho mbeleni
Hakika mkuu, lakini hao uliowataja walipata misingi kwenye nchi zenye mfumo mzuri wa elimu ikiwa ni pamoja na uchumi mzuri, usisahau gunduzi zao zlichukua muda na uwekezaji mkubwa. je hawa wataalam kama wahandisi, madaktari, wanasheria n.k tutawapata wapi kama sio huko, but nimekuelewa lazma tuanze kubadili mind set zetu kuanzia kwenye grassroot level na inawezekana
 
AJE TANZANIA INSTITUTE OF RAIL TECHNOLOGY (TIRTEC) ajisomee zake DIPLOMA OF LOCOMOTIVE ENGINEERING IN DIESEL ELECTRICAL mpaka amalize miaka 3 hiyo anakuja job kucheza na DIESEL ELECTRIC LOCOMOTIVES baadae anajiendeleza mwenyewe au hataki kufanya kazi kwenye SGR??
Huko TIRTEC mnaoenda wengi hamna vyeti visafi.
 
Hakika mkuu, lakini hao uliowataja walipata misingi kwenye nchi zenye mfumo mzuri wa elimu ikiwa ni pamoja na uchumi mzuri, usisahau gunduzi zao zlichukua muda na uwekezaji mkubwa. je hawa wataalam kama wahandisi, madaktari, wanasheria n.k tutawapata wapi kama sio huko, but nimekuelewa lazma tuanze kubadili mind set zetu kuanzia kwenye grassroot level na inawezekana
Nashukuru kwa kunielewa mkuu, ila leo hii ukifuatilia ktk limu yetu ni watu wachache sana ambao wamefuata ndoto na malengo yao ktk kada walizo chukua kwenye elimu ya juu. Kwa hali hiyo ubunifu utakuwa jambo gumu sana sababu wamekuwa km wamelazimishwa hivyo kupelekea ubunifu na ufanisi kuwa nadharia na wengi kulenga kuajiriwa tuu
 
.....tulianza kupotea zamani sana (lawama zimuendee mkoloni/mzungu) , na ukipotea sidhani km utafika unakotaka kwenda ,

Haya maneno ....."soma kwa bidii sana mwanangu ufaulu, upate kazi nzuri"..... Ndio yaliyotufikisha hapa.
 
Vijana wanatakiwa wapewe elimu ya uchaguzi sahihi pindi wakiwa shuleni(A-level),yani mtu anaona kuna course inahitaji watu wachache na ipo kwenye chuo pendwa mfano UDSM,SUA,DIT na vingine vingi alafu ufaulu wako ni mdogo alafu unaomba na kuweka 100% kwamba utapata yani jua kua unacheza bahati nasibu.
NOTE
1.Ukiwa unachagua course katika chuo fulani basi fanya utafiti wa kutosha ikiwezekana angalia waliochaguliwa miaka iliopita hua wanachukua ufaulu gani mfano UDSM hua wanatoa selected candidates na ufaulu wao.
2.Angalia idadi ya wanafunzi wanaotakiwa na chuo chenyewe.
3.Ikiwezekana kama ufauluwako ni mdogo kama Div 2 na kuendelea basi angalia course zinazo hitaji watu wengi.
4.usi ng'ang'anie vyuo vikubwa, kama course yako ipo kwenye vyuo vingine na ni vyuo bora basi omba pia kwenye hivyo vyuo.

Zingatia hili
5.Mfano Chuo kama UDSM kwa mtazamo wangu ni chuo ambacho KINATENDA HAKI KWA KILA MTU hivyo hakiangalii tu watu wenye ufaulu mkubwa kinachanganya watu wenye ufaulu mkubwa,wakatikati na wengine hivyo usishangae kuona una ufaulu mkubwa alafu ukatemwa na mwenye wakawaida akachaguliwa.
HIVYO USISITE KUOMBA TENA KWA AWAMU YA PILI HUENDA NAFASI YAKO IKAWA HUKO.

Mfano halisia; Katika masomo yangu mimi niliwahi kuomba awamu ya kwanza nikakosa ila nikaomba tena awamu ya pili same course same university then nikachagulia.
 
tusiwe tunalaumu tu bila kutafakari na kufuatilia maana yawezekana aliomba kozi ambazo wengi wana ufaulu wa juu kulingana masomo yake au aliomba kozi ambayo haiendani ya ufaulu wake,Jaribu kufuatilia kwa ukaribu
 
whatever utakavoidefine hiyo principle ila kinachohitajika ni D mbili na sio hiyo ya B na E, mtu mwenye D mbili anaclear chance ya kupata chuo kuliko huyo mwenye B na E,
tatizo hamjaelewa hapa,serikali na vyuo imetengemeza system ambayo hiyo system inasoma na kupitisha only wenye kutimiza hizo D mbili kwahiyo wewe kama umepungukiwa moja system inakutema directly,haina swalia mtume....
Acha story wewe

Tunachoangalia ni pts 4 kwenye masomo mawili

B=4 na E =1 ukijumlisha unapata 5

D=2 na D =2 ukijumlisha unapata 4

Kwa hyo MTU mwenye chance kubwa ya kupata ni aliepata AE,BE,CE lastly DD

hii elimu ni kubwa sana,ila ukiwa mpole utaielewa!

Principle pass ni A HADI E
 
Back
Top Bottom