Walioomba ajira TRA Novemba wameshaitwa kwenye usaili?

Genesis og

New Member
Nov 18, 2021
2
6
Habari wadau,

Samahani kwa wale walioomba nafasi za ajira TRA za mwezi November ambazo deadline ilikuwa tarehe 4 washapata majibu ya kuitwa kwenye usaili maana ajira portal huwa wanatoa majibu baada ya week 2 kupita yangu deadline.
 
Hukuskia Mchengerwa akipiga kelele juzi. Inshort watu wapo kazini tayari. Fanya mambo mengine ndugu yangu
 
Kuna watu kadhaa wameripoti katika vituo mbalimbali vya kazi TRA mwezi uliopita
Wale walichukuliwa kutoka kwenye Reserve yao tu. Hawakuwa wengi ni Ma IT kadhaa na madereva kiasi. Huu uongo hauna maana kwa jamii. Na tena sasa ni mwezi wa pili kama si watu wapo kazini.
 
Hiyo reserve yao hao maIT na madereva waliwafanyia lini usaili? kama wamechukua katika database ya PSRS mbona wanawekwa kwa miezi 6 kisha wanaondolewa inakuwaje hao wakawepo muda mrefu? Alafu unasemaje huu ni uongo wakati hapo kwenye comment yako umekiri kweli kuna watu kadhaa wamechukuliwa
 
Usaili wa bara umeshaisha uliobaki lazima ukafanyike zanzibar kukamilisha asilimia 21 % yao.

Kama unataka kazi TRA Fanya manuva upate kitambulisho cha mkazi zanzibar .. huko ushindani sio mkali.. maana wa Zanzibar wengi hawapendi shule
 
Inawezekana 21% isifike kwa wenye vigezo huko Zanzibar so Wa Bara wanaweza kwenda kujaza ili kufikisha idadi inayotakiwa
 
Usaili wa bara umeshaisha uliobaki lazima ukafanyike zanzibar kukamilisha asilimia 21 % yao.

Kama unataka kazi TRA Fanya manuva upate kitambulisho cha mkazi zanzibar .. huko ushindani sio mkali.. maana wa Zanzibar wengi hawapendi shule
Nani kasema wazanzibari hawapendi shule?

Ushahidi tafadhali
 
Kuna sehemu nimeandika wa znz wote hawapend shule?

Weka matokeo ya necta ya shule za znz tulinganishe na bara
Wazanzibar wanapenda shule ila populations yao sio kubwa na hivyo kupelekea hiyo 21% ya ajira isifike kutokana na watu wenye vigezo kuwa wachache
 
Usaili wa bara umeshaisha uliobaki lazima ukafanyike zanzibar kukamilisha asilimia 21 % yao.

Kama unataka kazi TRA Fanya manuva upate kitambulisho cha mkazi zanzibar .. huko ushindani sio mkali.. maana wa Zanzibar wengi hawapendi shule
nina jamaa yangu anademu wake wa kizanzibar ambaye anakoneksheni na familia ya chifu wa kule visiwani, kuna siku huyo demu kakutana na bwana mkubwa akaulizwa ushapata kazi? akajibu hapana akaambiwa basi tafuta siku uje zenji tuongee, demu kafunga safari yeye na bwana ake hadi znz akapangiwa appointment akaenda kuonana na mkuu akaelezea shida zake akasema na huyu ni mchumba wangu wote hatujapata kazi basi simu ikapigwa bara waliporudi wote wamepangiwa vituo vya kazi jamaa yangu siku hizi kawa bosi kwa kupitia babe wake
 
Yeah,we don't know what tomorrow will bring mkuu...!
 
Back
Top Bottom