BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,115
JK; nyumba zetu!
Tanzania Daima
LEO tunaandika suala hili kwa mara ya 12. Kwa mara nyingine tena, tunawakumbusha Watanzania wenzetu na viongozi wetu kuwa msimamo wetu katika suala linalohusu uuzwaji wa nyumba za serikali kwa viongozi wetu wakati wa serikali iliyopita uko wazi.
Imani yetu katika maamuzi haya ni kwamba, Watanzania tumeibiwa mali na viongozi wetu walioamua kuitumia vibaya dhamana ya madaraka tuliyowapa.
Bunge letu limekaa vikao vingi Dodoma tangu suala hilo lilipozuka na kulalamikiwa, na dalili zinaendelea kuonyesha wazi kuwa hakuna mwenye dhamira ya kuzikomboa nyumba zetu ambazo tunaamini tumeporwa.
Pamoja na kukiri kuwa Bunge limeendelea kuweka rekodi mpya kila wakati, hasa wakati huu lilipounda kamati teule ya kuchunguza mkataba wa Richmond, bado tunaendelea kulalamika kuwa limeacha suala jingine muhimu la kulitolea maamuzi ya kibunge.
Kama lilivyoshindwa kufikia maamuzi mazito ya pamoja katika masuala ya mgogoro wa Reginald Mengi na Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima, mikataba ya madini na mengine mengi, bado limeendelea kukwama kutumalizia suala la uuzwaji wa nyumba za serikali kwa baadhi ya watumishi wa umma.
Kimsingi, Bunge hilo pia limeshindwa kujadili au japo kudodosa kuhusu ulipofikia uamuzi wa serikali wa kuzirejesha baadhi ya nyumba hizo ambazo ziliuzwa kwa viongozi wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa.
Kwetu sisi wa Tanzania Daima, kama tulivyopata kusema huko nyuma, ukimya huu wa wabunge wetu, waliokuwa na fursa nyingi za kulivalia njuga suala hili, hata kama ikibidi kuandaa hoja binafsi, ni wa kukatisha tamaa.
Tunasema ni wa kukatisha tamaa kwa sababu suala hili ni moja ya mambo ambayo kwa kiwango kikubwa yalipingwa na watu wengi wakati wa utekelezwaji wake, hata kufikia hatua ya malalamiko haya kumfikia Rais Kikwete.
Mbele ya waandishi wa habari, Kikwete alilitangazia taifa hili mwanzoni mwa Oktoba mwaka jana kuwa, tayari serikali ilikuwa imeshaanza kuchukua hatua ambazo zitawezesha kurejeshwa kwa baadhi ya nyumba hizo ambazo alisema ziliuzwa kwa makosa.
Ingawa tulikuwa miongoni mwa Watanzania walioipokea kauli hiyo ya Kikwete kwa mikono miwili, msimamo wetu tangu wakati huo umekuwa wazi kabisa kwamba msamiati wa baadhi ya nyumba unapaswa kuondolewa na badala yake urejeshwaji unapaswa kuwa wa nyumba zote zilizouzwa.
Tunasema hivyo tukiamini kwa dhati kabisa kuwa, uamuzi mzima wa kuziuza nyumba hizo ulifanywa pasipo kuweka mbele masilahi ya taifa, na hivyo unapaswa kufutwa ili kumaliza fedheha hiyo ya kihistoria ambayo tutaendelea kuilalamikia siku nenda - rudi.
Tunaamini unyeti wa maeneo zilikojengwa nyumba hizo, umuhimu wa nyumba zenyewe na ukweli kwamba, uongozi ni dhana ya kupokezana vijiti kama alivyopata kusema Rais Kikwete, uamuzi wowote wa kuipokonya serikali rasilimali yake muhimu unapaswa kufutwa pasipo kuangalia matokeo ya kufanya hivyo. Tulitegemea wabunge wangeliona hili.
Tunahitimisha maoni yetu tukilikumbusha taifa kuachana na usahaulifu, hasa ule unaohusu masuala ya msingi.
Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa, ukimya wetu unatoa mianya ya nyumba zetu kuendelea kuuzwa kwa siri, huku zile tulizoahidiwa kurudishwa zikiendelea kubakia mikononi mwa watu. Hali hii lazima tukabiliane nayo.