Waliondaa katiba ya Tanzania ya mwaka 77 ndio chanzo cha yote haya

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,691
149,915
Chanzo cha matatizo yote haya ya kina Bashite ni matokeo ya hii Katiba tuliyonayo sasa kwani ni katiba inayompa Raisi madaraka makubwa sana na kumfanya yeye ni very special kuliko watanzania wote.

Chanzo cha matatizo yote tunayoyaona sass ni hivi vipengele vitatu.

1. Rais kuwa na kinga ya kutoshitakiwa

2. Rais kuwa na Mamlaka ya kulivunja Bunge.

3. Rais kuteua karibu kila mtu

Tatizo lingine limeletwa na utaratibu wa CCM kuwa Rais anaetokana na CCM ndie anakuwa mwenyekiti wa chama Taifa.

Matokeo yake ni kuwa Rais anakuwa na mamlaka makubwa serikalini na ndani ya chama na hata ile dhrrana ya chama kusimamia serikali inakuwa ni nadharia tu.

Bila kurekebisha mambo haya tutaendelea kuwa walalamikaji ndani ya nchi yetu licha ya ukweli kuwa Raisi ni mwajiriwa wetu.

Hata yale maneno ya Msukuma kuhusu kukiogopa sijui kitu gani kile(wengi naamini mnakijua) ni matokeo ya katiba hii tuliyonayo sasa na utaratibu huo wa CCM.

Sijui ni kwanini mwalimu Nyerere hakuona umuhimu wa kubadili katiba kabla hajaondoka madarakani licha ya kujua athari zinazoweza kulikumba Taifa kutokana na katiba hii!!
 
Wana bodi nawasalimu kwa jina LA JF.
Naomba tubadili katiba iwe hivi
1. Rais asiwe msemaji was mwisho. Kuwe na tume ya kumwelekekeza rais cha kusema .
Time hii iwe huru na ichaguliwe na wananchi kwa kura. Tunaweza kuchukua mjumbe mmoja kila mkoa.

2. Tume iunde dira ya nnchi.
Hapa tuwe na dira( vision ) ya nchi. Kila rais anayeingia madarakani aifuate dira hii. Hii itamuongoza rais cha kufanya si kama sasa rais anaweza kuanzisha mradi, akiondoka madarakani, anayeingia anaweza kuuacha na kuanzisha wake. Haijatulia.
NB: Tume /Bodi iwe na malaka kuliko rais. Hata jeshi liwe chini ya bodi hii.
Naamini tutatoka hapa tulipo, ukanda na ukabila utaisha.
Naomba maoni yako tuijenge Tanzania yetu.
 
Hapana ...mimi na wewe sasa tumefanya nini kuleta mabadiliko? Tuache kulaumu wazee wetu ...sisi ndio wenye nchi sasa ....tumefanya nini? ...Najua nitajibiwa kisiasa tu ....
 
Hapana ...mimi na wewe sasa tumefanya nini kuleta mabadiliko? Tuache kulaumu wazee wetu ...sisi ndio wenye nchi sasa ....tumefanya nini? ...Najua nitajibiwa kisiasa tu ....
Tunapaswa kuanza mijadala ya aina hii na kushinikiza mabadiliko ya katiba kama tunavyoshinikiza Bashite awajibishwe.
 
Back
Top Bottom