Waliomshambulia Kubenea na Ndimara waachiwa huru! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliomshambulia Kubenea na Ndimara waachiwa huru!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Oct 6, 2010.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mahakama leo imewaachia huru watuhumiwa kwenye kesi ya kumvamia na kumshambulia Mhariri wa Mwanahalisi Saed Kubenea na Mshauri wake Ndimara Tegambwage.

  Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya TBC, HAkimu aliwaachia huru washitakiwa wote kwenye kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa 2008 kwa madai kuwa ushahidi wa Polisi uliotolewa Mahakamani dhidi ya Wahistakiwa ni dhaifu!

  Hivi Polisi wetu waliowakamata watu hao na kuwafungulia mashitaka ni makini kiasi gani? AU ndo yale yale kufanya kazi zao kisiasa zaidi badala ya kuzingatia taaluma? Kama Polisi waliona hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya Watuhumiwa hao, kwa nini basi hawakuomba kuondoa kesi hiyo badala ya kujidhalilisha kiasi hicho? Au kulikuwa na maelekezo maalumu ya kuhakikisha Watuhumiwa hao wanaachiwa huru?
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hapo ndo utajua CCM NA TAIFA KUOZA
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hii kesi iliingiliwa sana na RA na EL na wawili hao ndiyo waliosababisha ifutwe kwa kumpotezesha mtuhumiwa muhimu (hakuonekana, nasikia alisafirishwa nchi jirani)) na pia baadhi ya mashahidi ambao baada ya kutoa maelezo hawakuwa wanafika kwenye kesi.

  Mimi naamini kabisa Kubenea mwenyewe (na Ndimara) sasa wataweka wazi mazingira ya kesi hiyo kwa vile sasa imefutwa, na tutegemee matoleo yajayo ya gazeti lake.

  Aidha kKuna baadhi wamekuwa wakishangaa kwa nini Kubenea analiendeleza bifu kati yake na RA na EL -- ni kutokana na kuhusika kwao kwa shambulio hilo. Tungoje, tutayasikia mengi -- maana pamefika patamu na kwa kuwa ni wakati wa kampeni kuna watu wataumbuka.
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,094
  Likes Received: 5,562
  Trophy Points: 280
  Kwa akili yako uliona kuna kesi pale???ile misukule imetolewa kafara ikaakikishiwa itatolewa pole ndugu nchi yetuuuuuuuuu
   
 5. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hao walifunguliwa kesi,ni kama boya tu wahusika wenyewe wanakula kuku tu mtaani!Hakuna haki hapa duniani,haki ipo mbinguni kwa mungu.
   
 6. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  pole kubenea
   
 7. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Our police force lacks professionalism na ndo maana yanapotokea mambo ya Kisiasa wanajiingiza kwa nguvu sana kama walivyofanya Shimbo na Mwema juzijuzi; hilo pia tunaliona kwenye Kampeni zinazoendelea nchini ambapo Vijana wa CCM huingilia mikutano ya Kampeni ya Wapinzani lakini hawachukui hatua zozote (refer PCCB case Vs CHADEMA in Arusha).

  Hebu fikirieni vituko vya Jeshi letu la Polisi hasa pale kunapotokea Uvunjaji wa Sheria halafu Polisi wanatangaza kuunda Tume ya kuchunguza matukio hayo. Vituko vitupu!
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kama ndivyo basi utendaji wa polisi unatoa mianya ya wahalifu kujiimarisha na kutoogopa sheria kwakuwa hata kama wakishikwa na kupelekwa mahakamani basi ushahidi kutoka polisi utawaweka huru.

  Vyuo vya polisi vinapaswa kuangaliwa mitaala yake na kuboreshwa ili tuwe na jeshi lenye kufanya kazi kwa umakini mkubwa.
   
 9. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Nchi imeoza unataka haki...eboo!
   
 10. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Kama ulimsikia mkulu akimnadi RA, EL,na waziri wa mahela wa zamani, ndo utajua kuwa usanii unafanyika kutulaghai. Kama ndivyo, basi na akina kubenea kwa kuwa hawapendwi na hao mafisadi, wamegeuziwa kibao.
   
 11. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kubenea amebenewa hapo!Haki haikutumika kabisa
   
 12. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alishasema Sumaye, ukitaka mambo yako yakunyookee wewe kuwa CCM. Kinyume na hapo subiri kinyume cha mambo kunyooka
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,549
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Mbona hayo ndiyo mapigo ya serikali ya jk. Hamkumbuki ya marehemu ditopile na zombe?
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Nami nimesikia hivyo hivyo -- kwamba uchunguzi wa kesi hiyo alianza kuivurunda Tibaigana ambaye alikuwa anapokea amri kutoka kwa RA na EL. Lakini nami pia naamini Kubenea, nimjuavyo mimi, sasa atayaanika yoote -- subirini tu.
   
 15. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #15
  Oct 6, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,219
  Likes Received: 7,338
  Trophy Points: 280
  Kama mtakumbuka, Kubenea na mwenzake walishambuliwa baada ya gazeti lao kuanika ufisadi kila uchao. JK alikwenda Hospitali mara moja na kuruhusu serikali ilipie gharama za matibabu India. Hii ilikuwa ni baada ya jamii kukasirishwa na kitendo kile, huku serikali ikijua wazi kuwa wapo washiriki Muhimu sana wa kesi hiyo. Hakuna mtu aliyekamatwa wakati kubenea akiwa India, lakini siku aliporejea alisema jumatatu inayofuata angeweka mambo hadharani. Cha kushangaza alhamisi kabla ya jumatatu, watu wakakamatwa. Sisi wengine tulijua kuwa waliokamatwa sio wahusika ni vibaka tu wamesingiziwa, na sababu kubwa ni kuwa kesi ikienda mahakamani basi haijadiliwi nje kwa sheria za nchi yetu. Tulijua kuwa walikuwa wanamziba Kubenea mdomo. Kwahiyo kama habari hii ni sahihi basi hiki ndicho tulitarajia. Hakuna sababu ya kuwalaumu Polisi maana wanapokea maagizo kutoka ngazi za juu.
  Kwavile kesi imekwisha, sasa Kubenea weka mambo hadharani. Na hii pia itumike kama silaha ya uchaguzi ili uzandiki huu ufike mwisho.
   
 16. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #16
  Oct 6, 2010
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Aliyempiga jk mtama afungwa miaka sita!
   
 17. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  YANA MWISHO BWANA ALIKUWEPO Kamuzu Banda, Sani Abacha, Mabotu, King Bagaza, Foday Sankho n.k. wako wapi?
   
 18. architector

  architector Member

  #18
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wacheni unafiki kusema msiyoamini utawala wa sheria ndio huo si lazima kila mtuhumiwa apatikane na hatia ndipo ionekane mahakama na vyombo vyetu vya dola vinafanya kazi kama hamuoni hivyo anzisheni jpolisi na forum court yenu muwahukumu!
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Tena Huyu mi nilitaka amkate kelbu Kama lie ya mwinyi au amtwishe ndoo awe mapengo ache kuchekacheka
   
 20. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe 100%. Shida yangu ni pale prosecutors wako tayari kuwatosa watu ambao hawahusiki ilmradi ionekane kwa jamii kwamba ipo kesi! Nadhani hili ndilo tatizo kubwa. Inanikumbusha mjomba wangu mmoja ambaye kwa namna ya ajabu alipenda sana maisha ya jela( unaweza usiamini). Kila ilipotokea wizi, yeye alikuwa wa kwanza kujitokeza na kusema anamjua mwizi, mara nyingi walimweka ndani wakimtuhumu pengine yeye ndiye aliyeiba. Lakini enzi zile za Nyerere Jeshi la Polisi lilifanya kazi vizuri. Alifanya hivi mara nyingi na wakati fulani alisota ndani zaidi ya miaka 8 baada ya kudai alikuwepo wakati mauaji fulani yalifanyinka kwenye baa kule Moshi. Lakini Polisi waliweza kubaini kilichotekea na kumfahamu huyu alikuwa anawasumbua. Alishtakiwa baadae kwa kosa la kubabaisha na kupotosha uchunguzi wa kipolisi. Lakini walau nakumbuka Jeshi la Polisi lilifanya vizuri sana kazi yake, ni miaka ya 70.

  Kwa Kubenea, naamini hawa walioachiwa walikamatwa kama kisanii na ndio maana hawajaonekana na hatia. Lakin nina wasiwasi waliofanya kosa hili wanajulikana na wanalindwa ili wasiletwe mbele ya sheria. Hili ndilo linalotisha!
   
Loading...