Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
Nina imani kuwa tulio wengi bado tunakumbuka vizuri hili sakata la ESCROW. Kauli iliyofunga mjadala ni ile iliyotolewa na mkuu wa nchi wa kipindi hicho kuwa pesa ile haikuwa ya umma.
Mimi sina tatizo na aliyetoa kauli hiyo kwa sababu nafahamu kuwa yeye alikuwa ni mtu wa kuletewa taarifa. Nina tatizo na hao waliompotosha kwa kumletea taarifa zisizokuwa za kweli ambapo leo ukweli unaonekana, kuwa pesa hizo zilikuwa ni za umma. Kuna watu ambao hawawezi kukwepa dhahama hii, kwa sababu wao ndiyo walikuwa wamebeba dhamana za Watanzania kwa kuwa katika nafasi walizoaminiwa ili kutulinda Watanzania tusiibiwe kwa namna yoyote ile.
Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati huo hawezi kunishawishi hata kidogo kuwa hata yeye hakujua kuwa zile pesa zilikuwa ni za umma. Vinginevyo akili wazi kuwa alikuwa katika ofisi hiyo kimakosa kwa sababu hakuwa na weledi wa kutosha kuitafsiri kisheria mikataba kama hiyo ya TANESCO na IPTL. Mwanasheria mkuu wa TANESCO sidhani kama naye hakujua kama ile pesa bado ilikuwa na mgogoro. Mh. Chenge, yeye ndiyo haswa naweza kusema aliijua vizuri ngoma hii. Kama Mwanasheria mkongwe atakuwa alichangia sehemu kubwa kushawishi kuwa ile pesa haikuwa ya kwetu tena.
Mimi namalizia kwa kuwaomba TAKUKURU wasiishie kwa wale waliopata mgawo wa Mkombozi pekee. Hata wapotoshaji wa Kikwete nao wana kesi ya kujibu.