Waliompotosha JK kuhusu pesa za ESCROW nao washughulikiwe

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,172
2,000
Nina imani kuwa tulio wengi bado tunakumbuka vizuri hili sakata la ESCROW. Kauli iliyofunga mjadala ni ile iliyotolewa na mkuu wa nchi wa kipindi hicho kuwa pesa ile haikuwa ya umma.

Mimi sina tatizo na aliyetoa kauli hiyo kwa sababu nafahamu kuwa yeye alikuwa ni mtu wa kuletewa taarifa. Nina tatizo na hao waliompotosha kwa kumletea taarifa zisizokuwa za kweli ambapo leo ukweli unaonekana, kuwa pesa hizo zilikuwa ni za umma. Kuna watu ambao hawawezi kukwepa dhahama hii, kwa sababu wao ndiyo walikuwa wamebeba dhamana za Watanzania kwa kuwa katika nafasi walizoaminiwa ili kutulinda Watanzania tusiibiwe kwa namna yoyote ile.

Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati huo hawezi kunishawishi hata kidogo kuwa hata yeye hakujua kuwa zile pesa zilikuwa ni za umma. Vinginevyo akili wazi kuwa alikuwa katika ofisi hiyo kimakosa kwa sababu hakuwa na weledi wa kutosha kuitafsiri kisheria mikataba kama hiyo ya TANESCO na IPTL. Mwanasheria mkuu wa TANESCO sidhani kama naye hakujua kama ile pesa bado ilikuwa na mgogoro. Mh. Chenge, yeye ndiyo haswa naweza kusema aliijua vizuri ngoma hii. Kama Mwanasheria mkongwe atakuwa alichangia sehemu kubwa kushawishi kuwa ile pesa haikuwa ya kwetu tena.

Mimi namalizia kwa kuwaomba TAKUKURU wasiishie kwa wale waliopata mgawo wa Mkombozi pekee. Hata wapotoshaji wa Kikwete nao wana kesi ya kujibu.
 
Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,989
2,000
Nani alikuambia kuwa alipotoshwa?Angepotoshwa waliochota pesa kupitia Stanbic wangefichwa????Kwanini wamiliki wa Simba trust mpaka leo ni siri kubwa???
JK hakupotoshwa,kelele zote zile za bunge hakuzisikia?Kwanini aliruhusu Muhongo aachie ngazi kama kweli alipotoshwa???Yaani unamwachisha kazi waziri wako kwa pesa isiyo ya serikali,does it make sense to you?
Msitake kuonea watu wadogo bhana,Kikwete alijua kabisa mchezo mzima!
 
Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,989
2,000
Jitihada za kumuweka KIKWETE mbali na ESCROW hazijawahi kumuacha mtu salama.

Kikwete naye ni muhusika mmojawapo, hatuwezi kulishughulikia hili tatizo likaisha kwa haki, bila kumgusa Jakaya.
Yaani mkuu umesema kweli,hili ni jaribio la kumtoa JK kwenye issue ya Escrow!
 
mwayena

JF-Expert Member
Apr 21, 2016
2,633
2,000
kikwete alipotoshwa????????dah! kuna watu hawafatilii kabisa mambo ya nchi hii.mtoa mada kumbe ule mchezo ulichezwa na mzee wa msoga ulikusomba mzima mzima? alikua anajua anachokiongea yule bwana siku ile.labda kama una mpango wa kumtetea na kumtenga na kikombe hiki.
 
Batale

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,111
2,000
Yeye mwenyewe zliwahi tuasa watanzania "za kuambiwa changanya na za kwako ", kwanini yeye hakuchanganya?. Hawezi kwepa hili.
 
PMM

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
778
250
Nina imani kuwa tulio wengi bado tunakumbuka vizuri hili sakata la ESCROW. Kauli iliyofunga mjadala ni ile iliyotolewa na mkuu wa nchi wa kipindi hicho kuwa pesa ile haikuwa ya umma.

Mimi sina tatizo na aliyetoa kauli hiyo kwa sababu nafahamu kuwa yeye alikuwa ni mtu wa kuletewa taarifa. Nina tatizo na hao waliompotosha kwa kumletea taarifa zisizokuwa za kweli ambapo leo ukweli unaonekana, kuwa pesa hizo zilikuwa ni za umma. Kuna watu ambao hawawezi kukwepa dhahama hii, kwa sababu wao ndiyo walikuwa wamebeba dhamana za Watanzania kwa kuwa katika nafasi walizoaminiwa ili kutulinda Watanzania tusiibiwe kwa namna yoyote ile.

Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali wakati huo hawezi kunishawishi hata kidogo kuwa hata yeye hakujua kuwa zile pesa zilikuwa ni za umma. Vinginevyo akili wazi kuwa alikuwa katika ofisi hiyo kimakosa kwa sababu hakuwa na weledi wa kutosha kuitafsiri kisheria mikataba kama hiyo ya TANESCO na IPTL. Mwanasheria mkuu wa TANESCO sidhani kama naye hakujua kama ile pesa bado ilikuwa na mgogoro. Mh. Chenge, yeye ndiyo haswa naweza kusema aliijua vizuri ngoma hii. Kama Mwanasheria mkongwe atakuwa alichangia sehemu kubwa kushawishi kuwa ile pesa haikuwa ya kwetu tena.

Mimi namalizia kwa kuwaomba TAKUKURU wasiishie kwa wale waliopata mgawo wa Mkombozi pekee. Hata wapotoshaji wa Kikwete nao wana kesi ya kujibu.
Inawezekana kabisa Mh Rais Mstaafu asijue, lakini baada ya joto lote lite!, siamini naye angekuwa front line kutuambia si za umma. Hata hivyo, nashauri aachwe apumzike kama alivyo tujuza Mh Rais ikiwa tu watanzania tutajuzwa nani hasa ndio SIMBA TRUST?
 
Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
3,493
2,000
Jamani mwenye clip ya bunge wakati wa mjadala wa Escrow atuwekee. Kulikuwa na malumbano makali kati ya Lissu na mwanasheria mkuu wa serikali jaji Werema. Lissu alisema zile ni fedha za serikali na Werema anasema siyo fedha za serikali. Nashangaa leo wahusika wanatuhumiwa kuhujumu nchi kwa kuiba fedha za umma. CCM jamani!
 
Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,364
2,000
hii kesi imekaa kikiki kiki...........................

mara wameshasema wazee hawahusiki wasisumbuliwe na ni dhahiri kabisa wanahusika
 
Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,580
2,000
JK ndiye aliye wapotosha viongozi wa chini yake,ndiye anayetakiwa kuwa mshitakiwa wa kwanza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom