Waliompora KSh 245k binti yake Raila wafikishwa Mahakamani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Korti jijini Nairobi imewafungulia mashataka mtu na mke wake kwa kosa la wizi na kutumia jina la mtu mwingine baada ya wawili hao kulaumiwa kwa kumwibia binti yake aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga.

Aliyekuwa mpambe wa Rosemary Odinga, John Ayub na mke wake Christine Anyango, walikamatwa kwa madai ya kuiba KSh 245,000.

Kulingana na Citizen Digital, wizi huo unadaiwa kutekelezwa Novemba, 15 2018. Mke wa John alishtakiwa kwa kosa la kutumia jina la mtu mwingine kusajili kadi ya simu kabla ya kuzichukua pesa hizo. Inadaiwa kuwa, Christine aliisajili kadi hiyo kwa kutumia jina la David Munyasia.
 
Back
Top Bottom