Waliomo katika "ushirika usio mtakatifu"...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
“huu ni mwendelezo tu wa kampeni chafu unaoendeshwa na watu wachache ambao ni maarufu na ni wazito katika jamii yetu waliojiunga pamoja katika ushirika usio mtakatifu. Ambao kwa kutaka kutimiza malengo yao wameamua wanaoyajua wao wenyewe wameamua kuchafua majina, heshima, na hadhi za baadhi yetu.

Katika kikundi hicho wapo ambao hawaridhiki na nafasi za uongozi walizonazo, ambao wamejenga chuki kwa kudhani na kujiaminisha kuwa labda mimi nilihusika kuwazuilia kujichukulia fursa za ufahali na haki inayostahiki vyeo vyao...wapo ambao uwezo wa maarifa yao umewapeleka kutomudu ushindani wa kibiashara na badala yake wamejianimisha labda baadhi yetu ndio sababu ya kutofanikiwa kwao, na wapo ambao wamejiingiza katika kikundi hicho kwa sababu ya wivu. Mawazo yote hayo si sahihi, na yanaelekea kunipa uwezo ambao sina." - Rostam Aziz
 
Mkuu Mkjj heshima mbele,

Nimefungua haraka haraka hii thread nikajua list ya waliomo katika ushirika usio mtakatifu aliousema RA imewekwa hadharani kama ilivyokuwa kwa list of shame. duuuh mwenye idea Mh.RA alikuwa anamaanisha akina nani kwa majina tafadhali?
 
1.Mengi
2.sitta
3...
 
Anataka kusema nini hapa?

Semantics labda, lakini Tanzania mawasiliano kazi.

Ukisema "ushirika usio mtakatifu" unajionyesha jinsi ulivyo uppity na holier than thou-ish.

Ushirika wowote wa binadamu hauna utakatifu, sasa akisema ushirika "usio mtakatifu" that's a non-starter, no brainer, kwa sababu basically umetaja universal set ya shirika zote za binadamu, kuanzia ma Chavinista wa Venezuela Mpaka ma Sandinista wa Nicaragua, kuja kwa ma liberali wa Kimarekani mpaka Ma Mormon na Wakatoliki, kuanzia CCM mpaka TLP na vyote vya kati.

Kwa hiyo anataka kusema nini? Ushirika mchafu unaomfanyia deliberate slander?
 
nadhani yeye alikuwa ana kitu anamaanisha... lakini hakuthubutu kukisema. Kuna mambo mengine aliyasema ambayo nashangaa kwanin hayakuripotiwa na vyombo vya habari..
 
Kama alichosema kuhusu Richmond?au mwanakijiji ni jambo lipi..?
 
kuna hilo lakini nadhani alikuwa anazungumzia mambo fulani. Aliulizwa kuhusu michango yake kwa watu wengine i.e waandishi wa habari kama yawezekana anatunza rekodi kama ilivyo kwa Mtikila na yeye akawahakikishia kuwa wasiwe na wasiwasi kwani siyo michango au misaada yake anatunzia risiti...
 
kama ana ubavu aseme basi angalau tujue na yeye ni mwanamume kati ya mafisadi.
 
Yaani Kevo kwa maelezo ya RA haukuelewa anwalenga kina nani?Na unadani kwanini aliwakatalia ITV wasiingie baadaye akawaruhusu...kwanini Thisday/Kulikoni walikataliwa kuingia pale mlangoni?

kuna maelezo haukuyapata...utajua ni kina nani anwalenga,Mwenye ubavu wa kuwataja atakuwa Ngurumo Tu
 
Gembe.. this bring me to the question.. inakuwaje mtoa taarifa achague chombo gani cha habari kije kumsikiliza?
 
...RO anashutumiwa ndio engineer behind Richmond saga lakini publicly amekataa na hahusiki na ametoa nafasi kwa yeyote mwenye ushahidi amfungulie mashtaka au aonyeshe lakini mpaka sasa yamebaki maneno ya chini chini tuu RO ni fisadi fisadi,na hata Mwakyembe report hatukuona jina lake,sasa naanza kushtukia credibility ya wanaomshutumu huyu jamaa maana ni kama story za mitaani tuu...isije ikawa ni kama mambo ya wanamitandao na njaa za Mtikila kama walivyomfanyia Sumaye!
 
Koba hii reasoning ina matatizo.. wenye jukumu la kufanya uchunguzi na kutafuta ushahidi utakaosimama mahakamani siyo wanaotoa shutma. Mtu akivamiwa na majambazi na yakakamatwa au akajua ni kina nani waliomvamia akatoa taarifa Polisi, Polisi hawamuambii "katuletee ushahidi"! Chombo ambacho kina uwezo na madaraka ya kuchunguza uhalifu siyo raia wanaotoa shutma bali ni kile chenye madaraka ya kuchunguza hivyo.

Mfano mzuri ni suala hilo la Bungeni, kwanini Polisi hawakuwaambia waandishi au waliosema habari za unga unga kutoa ushahidi na badala yake ni wao ndio waliofanya utafiti na kutoa taarifa?

Mimi naweza kukuambia kuwa mwaka x,y Rostam alipokea kiasi cha fedha from x,y kwa ajili ya z fedha hizo ni za kifisadi auz ilikuwa na lengo hili au lile. Sasa mwenye chombo cha kuangalia anaangalia uzito wa tuhuma /shutma na kuona kama zinastahili kuchunguzwa. Akiona ndio basi anaanzisha uchunguzi.

Sasa huyo mwenye uwezo na nyenzo za kuchunguza akija na kuniomba ushahidi mimi nimpe ili kiwe nini? Nimemdokeza ni yeye jukumu lake kufuatilia. Vinginevyo watupe sisi sote nguvu ya kisheria ya kufanya uchunguzi, kukamata na kuwafikisha mahakanai. Then tutakusanya ushahidi wetu sisi wenyewe (sisi - wale ambao wanataka mafisadi na wezi wa mali zetu wachunguzwe)
 
...you have a point,lakini hii Richmond saga tunajua imeshamwangusha one of the most powerful guy in TZ (Lowassa) na majina mengi ya vigogo yametajwa wazi wazi sio kimajungu ni kwenye report za serikali kuanzia Karamagi mpaka Msabaha bangusilo na wao kuishia kujiuzulu,na official report ya Mwakyembe haikuwahi kumtaja RO kama amehusika au laa...napata shida kuamini huyu RO ndio architect wa hili saga akipeta huku wakuu wa nchi kina Lowassa wakianguka bila huruma.
 
Koba,

RA na wenzake ambao wameendelea kudai kwamba tupeleke ushahidi wanajua wazi kwamba wanalindwa na serikali kwa kushirikiana na vyombo vya dola (polisi, TAKUKURU, na UWT).

Kazi ya kukusanya ushahidi ni ya PCCB, POLISI na UWT ambao wanaweza kuingia mahali popote wakatoa order ya kupewa documents wanazihitaji kwa ajili ya kuzifanyia kazi. Hapa nina maanisha hata zile documents ambazo zimekuwa clissified kama siri wao wana access ya kuziona na kuzifanyia kazi.

Raia hana hiyo nguvu ya kufanya hayo, halafu Rais ama mtu anasimama mbele za watu na kusema wapeleke ushahidi. Ushahidi wa EPA uko mikononi mwa Polisi na PCCB kuanzia kadi za kufungulia accounts pamoja na documents nyinginezo za kuonyesha activities za accounts hizo na ndiyo maana wameweza ku-trace movement ya hizo fedha. Hakuna raia anayeweza kupata access ya hizo documents. Pamoja na hayo subiri report ikitoka utashangaa kama hiyo tume ya Rais ilikuwa inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ama layman fulani wa sheria na kusaidia na IGP na DG-PCCB. Usishangae ukiambiwa hakuna ushahidi wa kutosha kuwapeleka mahakamani na hivyo wameamua hela zirejeshwe na kuwaachia waendelee kupeta na huku kosa walilofanya ni ujambazi/wizi/kughushi.

Je, umeishamsikia Chenge akisema wapeleke ushahidi kuhusu vile vijisenti vyake ambavyo vilivumbuliwa na SFO? Anajua wazi kwamba hana ubavu wa kuingilia uchunguzi wa SFO na hajui matokea yake yatakuwaje. Lakini ingekuwa ni PCCB ama Polisi wa Bongo ndo wanachunguza ungeishamsikia akifoka kwa nguvu zote kwamba mwenye ushahidi apeleke polisi wakati polisi ndiyo wenye kazi ya kusaka ushahidi.

Kwa hiyo hili swala la ushahidi limekuwa ni kama kiini macho na excuse ya mafisadi wote. Wanapokuja kusema leteni ushahidi wanakuwa wana uhakika kwamba wameishaficha kila kitu na kwamba polisi/PCCB wanakuwa wameishawekwa sawa na ndiyo mwisho wa biashara. Sasa wananchi ndo tunatupiwa kazi ya polisi na PCCB huku wakijua hatuwezi kufanya hiyo kazi.

Tanzania hakuna sheria inayoruhusu wachunguzi binafsi kufanya hiyo kazi, kwa hiyo hata raia wasipokuwa na imani na PCCB/Polisi hawana option nyingine zaidi ya kukaa kimya na kuendelea kunung'unika.

Marmo juzi kawatisha wabunge kwamba wakishikwa na nyaraka za serikali ni kosa na wanaweza kufungwa. Hizo nyaraka ni siri, lakini siri za kuuza nchi pamoja mambo ya kifisadi na bado kuna mhuri mkubwa juu yake SIRI ama CONFIDENTIAL!

Haya mambo yanafanyika Tanzania tu kwa kuwa serikali iliyopo madarakani iliingia kwa njia za kifisadi na inashindwa kukemea ufisadi. Matokeo yake Rais anakuja kusema kwamba atasitisha zoezi la kukopesha mabilioni ya JK, hela yenyewe ni bilioni 21 na sijui hata ni ufisadi gani unaofanyika huko. Mbona alishindwa kusitisha malipo ya Dowans? TANESCO wamesubiri miaka miwili ya dharura imeisha ndo wanajidai kwamba wamesitisha mkataba wakati mkataba umeishafikia ukomo wake wa miaka 2. Mkataba ulianza August 2006, leo ni July 2008! Hivi wanatuona kwamba hatuna akili kiasi hicho? Mambo mengine yanatia kinyaa kabisa. Bunge lilisema wasitishe mkataba tangu April na ikiwezekana tuwadai hela, lakini hakuna anayeongelea kudai hela bali tunashangilia kusitishwa kwa mkataba uliofikia ukomo!
 
Koba hii reasoning ina matatizo.. wenye jukumu la kufanya uchunguzi na kutafuta ushahidi utakaosimama mahakamani siyo wanaotoa shutma. Mtu akivamiwa na majambazi na yakakamatwa au akajua ni kina nani waliomvamia akatoa taarifa Polisi, Polisi hawamuambii "katuletee ushahidi"! Chombo ambacho kina uwezo na madaraka ya kuchunguza uhalifu siyo raia wanaotoa shutma bali ni kile chenye madaraka ya kuchunguza hivyo.

Mfano mzuri ni suala hilo la Bungeni, kwanini Polisi hawakuwaambia waandishi au waliosema habari za unga unga kutoa ushahidi na badala yake ni wao ndio waliofanya utafiti na kutoa taarifa?

Mimi naweza kukuambia kuwa mwaka x,y Rostam alipokea kiasi cha fedha from x,y kwa ajili ya z fedha hizo ni za kifisadi auz ilikuwa na lengo hili au lile. Sasa mwenye chombo cha kuangalia anaangalia uzito wa tuhuma /shutma na kuona kama zinastahili kuchunguzwa. Akiona ndio basi anaanzisha uchunguzi.

Sasa huyo mwenye uwezo na nyenzo za kuchunguza akija na kuniomba ushahidi mimi nimpe ili kiwe nini? Nimemdokeza ni yeye jukumu lake kufuatilia. Vinginevyo watupe sisi sote nguvu ya kisheria ya kufanya uchunguzi, kukamata na kuwafikisha mahakanai. Then tutakusanya ushahidi wetu sisi wenyewe (sisi - wale ambao wanataka mafisadi na wezi wa mali zetu wachunguzwe)

Reasoning yako ni nzuri tatizo ni serikali yetu inafungia sana macho maneno ya whistle blowers.

RA nafikiri alitajwa na Mwakyembe ingawa sio moja kwa moja kwenye RDC bali kwenye transfer ya RDC to DOWANS. E-mail yake ilitumika kwa hiyo anayo ya kujieleza uhusiano wake na RDC which is = DOWANS.
 
...you have a point,lakini hii Richmond saga tunajua imeshamwangusha one of the most powerful guy in TZ (Lowassa) na majina mengi ya vigogo yametajwa wazi wazi sio kimajungu ni kwenye report za serikali kuanzia Karamagi mpaka Msabaha bangusilo na wao kuishia kujiuzulu,na official report ya Mwakyembe haikuwahi kumtaja RO kama amehusika au laa...napata shida kuamini huyu RO ndio architect wa hili saga akipeta huku wakuu wa nchi kina Lowassa wakianguka bila huruma.

Bado napigwa na butwaa. Hivi hao uliowataja hapo na wengine wengi, si pia walisafishwa na TAKUKURU katika sakata hilo hilo la Richmond? Iweje sasa ukubaliane na report ya Mwakyembe kuhusu hao na usitumie report ya TAKUKURU kuhusu wote hao na RA?

Pia kama RA hakuguswa na report ya Mwakyembe kwa njia ye yote inayompa athari zo zote kijamii na kisiasa, ni vipi alitaka apewe nafasi ya kujitetea ndani ya bunge, na hatimaye kutoa maelezo yake kwa Spika. Na kwa nini aliona haja ya kupiga baragumu na vinumbi kuwa hausiki, wakati akijua kuwa hausiki na report ya Mwakyembe haimtaji?

Wale wezi wa pamba nawajua, wana mabaki ya pamba kwenye videvu vyao. Ukiona mtu anajishika kidevu kujisafisha, jua ana lake jambo ...............

RA sasa hivi yuko kwenye harakati ya kujishika kidevu .................., labda anawashwa tu na ndevu au ..............................
 
...RO anashutumiwa ndio engineer behind Richmond saga lakini publicly amekataa na hahusiki na ametoa nafasi kwa yeyote mwenye ushahidi amfungulie mashtaka au aonyeshe lakini mpaka sasa yamebaki maneno ya chini chini tuu RO ni fisadi fisadi,na hata Mwakyembe report hatukuona jina lake,sasa naanza kushtukia credibility ya wanaomshutumu huyu jamaa maana ni kama story za mitaani tuu...isije ikawa ni kama mambo ya wanamitandao na njaa za Mtikila kama walivyomfanyia Sumaye!

Mkuu ulimaanisha RA na siyo RO, au? RO ni mkuu wa usalama wa taifa
 
.....seems kila mtu kuanzia mtaani mpaka ikulu wanajua mwizi fisadi ni nani lakini anayetakiwa kuchunguza na kushtaki hafanyi kazi yake...hatuna serikali pale tuna wababishaji tuu,dawa ni kuwachomoa come 2010 tusipofanya hivyo hatuna haki ya kulalamika maana majority watakuwa wanakubaliana na wanachofanya!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom