Waliomchinja Katibu wa CCM Kahama wakamatwa, Yumo pia diwani wa CCM

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Nawasilisha mada hii nikiwa na majonzi makubwa juu ya haya yanayotokea ndani y nchi yetu lakini sitasita kutilia shaka vyombo vyetu vya usalama hasa Jeshi la polisi kwani matukio yote ya kinyama ambayo yamewatokea wanachama au viongozi wa CCM watuhumiwa wameweza kukamatwa lakini cha ajabu matukio kama hayo ambayo wamefanyiwa wanachama au viongozi wa vyama vya upinzani hakuna yeyote aliyekamatwa hadi sasa kama vile
1. Mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMA kule Useriver Arusha
2. Mauaji ya yule kada wa CHADEMA kule Igunga
3. Kuvamiwa na mwisho wake kusababusha kifo cha Dr. Mvungi
4. Waliolipua Bomu pale Soweto Arusha
Tunajiuliza kwa nini hadi leo hawa hawa Polisi wameshindwa kukamata watuhumiwa huku wale waliohusika na matukio kama hayo kwa wanaCCM kama vile kule Mbeya na hili la Kahama wamekamatwa kulikoni kwa hili jeshi letu?

TANGAZO
Mwili wa marehemu Daudi Lusalula Mbatiro(56) baada ya kuchinjwa Desemba 5,2014-Picha kutoka maktaba ya Kitaani BONGO news blog
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha.Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kunasa mtandao wa watu wanaojihusisha na vitendo vya mauaji ya watu kwa kuchinja kwa visu,ikiwemo tukio la mauaji ya Katibu wa Chama Chama Mapinduzi kata ya Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga Daudi Lusalula Mbatiro(56) aliyeuawa kwa kuchinjwakama kuku mwaka jana kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaaTukio la kuuawa kwa katibu huyo wa CCM lilitokea Desemba 5,2014 saa mbili usiku wakati katibu huyo wa CCM kata ya Mwaluguru ambaye pia alikuwa ni katibu wa elimu,malezi na mazingira baraza la wazazi wa CCM wilaya ya Kahama akitokea kata ya Kagongwa kwenda nyumbani kwake Sungamile baada ya kutoka kwenye mkutano wa chama chake uliokuwa unafanyika mjini Kahama.
Waliotajwa na jeshi la polisi kuhusika katika mtandao huo ni pamoja na diwani wa kata ya Mwalugulu wilayani Kahama Bundala Kadilanha(CCM),mfanyabiashara wa Kagongwa Tobo Mwanasana,pamoja na Emmanuel Maziku,Masanja Shepa,Samwel Seni Budugu na Shija Shepa.Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alisema katika uchunguzi wa mauaji ya katibu wa CCM kata ya Mwalugulu Daudi Mbatiro jeshi la polisi limewakamata watuhumiwa Emmanuel Maziku na Masanja Shepa na baada ya kuhojiwa walikiri kuhusika na mauaji hayo.
Alisema baada ya kuwahoji watuhumiwa hao wawili,waliwataja wahusika wengine ambao ni Bundala Kadilanha(diwani wa Mwalugulu),Tobo Mwanasana(mfanyabiashara,Samweli Seni Budugu mkazi wa Mwakitolyo na Shija Shepa mkazi wa Mwalumba Kahama.Alisema awali jeshi la polisi baada ya kupata taarifa za watu hao liliweka mtego kwa kuwapigia simu ili kuwakodi kufanya mauaji katika kijiji cha Nyindu na kufanikisha kuwakamata watu hao ambao hujihusisha na matukio mbalimbali ya mauaji..
Alisema baada ya kuwafanyia mahojiano watu hao wawili walikiri kuhusika na matukio ya mauaji katika mkoa wa Shinyanga na Tabora kwa kukodiwa ili kuchinja watu kwa kisu na wao sio wakata mapanga ingawa wanaua vikongwe na kulipiza kisasi.
Kamanda Kamugisha alisema watuhumiwa walisema kiongozi wao ni Samweli Seni Budugu na wenzake ni Tobo Mwanasana,Bundala Kadila na Shija Shepa na kabla ya mauaji hayo wanaenda kupakwa dawa kwa waganga wao wa jadi ambao ni John Shija mkazi wa kijiji cha Lyabukande na mwingine aliyetajwa kwa jina mojala Tabu mkazi wa Kizungu.
Kamanda Kamugisha alisema watuhumiwa wote wamekiri kuhusikana matukio ya mauaji ya marehemu Ngolo Sakumi(69) mkazi wa Mwalugulu na walikodiwa kwa shilingi1,000,000/= aliyewakodi ni Jikuba Kajile na Lukuba Nangi.
Tukio jingine walilokiri kuhusika ni mauaji ya Mary Seleman Masenya(45) mkazi wa kijiji cha Matinje na walikodiwa kwa shilingi 800,000/= na wanawake watatu ambao ni wake wenza wa marehemu.
Alitaja tuko jingine walilohusika ni lile la mauaji ya Mboje Seni(70) mkazi wakijiji cha Butondo na walikodiwa kwa shilingi 800,000/= walikodiwa na Mwanabundi mkazi wa Butondo na tukio jingine ni mauaji ya Kwigema Lubinza(60) mkazi wa kijiji cha Kakulu kata ya Nyahanga.Kamanda huyo alisem jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwakamata wahusika wengine wa matukio hayo ikiwa ni pamoja na waganga wa kienyeji waliohusika huku akiwataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwawahusika wote wa mauaji ya kukodiwa na mauaji ya vikongwe ili kukomesha kabisa mauaji hayo..
 
Kama wanaweza uwana wenyewe je sisi wengine. Tutafakari natuchukue hatua ccm nimdudu mbaya sana kwenye nchi hii
 
Hao wauaji wangekuwa ni wapinzani, hilo lingekuzwa na kuwa tukio la kitaifa, na bila shaka wangefanyiwa unyama mbaya sana. Lakini kwa vile ni magamba wenyewe kwa wenyewe, utasikia mahakama inasema waende waongee yaishe ili kukinusuru chama.
 
Ni jambo la aibu na kusikitisha kwa kweli. Hata Kama hakuna ajira huwezi kukubaliana na ajira ya kuuwa BINADAMU mwenzako Kama kuku.
 
inasikitisha sana lakini inafariji kusikia wauaji wamekamatwa big up polisi
 
Mbele ya CCM binaadamu wote si sawa..kuna wanaostahili vifo na mabalaa(WAPINZANI)...na pia kuna wanaostahili kuishi kama peponi...(WATAWALA)..hauhitaji kuwa na lundo la vyeti vya kitaaluma kuigundua hali hiyo bali ni kwa kutumia milango yako ya fahamu tu na kufuatilia mtiririko wa matukio utaona ni jinsi gani serikali ya CCM walivyo wanyama.....
Wakati sisi wanyonge tukishuhudia ndugu zetu wapendwa wakitufia mikononi mwetu kutokana na huduma mbovu na ukiritimba uliokithiri katika vituo vya afya pamoja na ukosefu wa madawa na vifaa tiba...wao na familia zao na wapambe wao hata wakijikata na kisu jikoni wanakimbizwa ulaya....
Wakati sisi wanyonge wakitujengea majengo wanayoyaita shule huku uakiwa hayana sifa ya kuwa shule kwa maana hakuna walimu, vitendea kazi, wala vitabu chini ya mtaala mbovu..watoto wao na wa familia za wapambe wao..wanawapeleka kwenye shule za kimataifa zenye walimu wengi mpaka mtoto akikohoa atauliza ulikuwa unasemaje...??
Wahenga walipata kusema kuwa..hakuna marefu yasiyokuwa na ncha...naamini kabisa iko siku tutashuhudia anguko kuu la CCM kama si mimi mwenyewe basi hata vitukuu vyangu...litakuwa ni anguko kuu ambalo halijapata kutokea nchini kwetu....
TIME WILL TELL
 
Akili ya viongozi wa CCM walio wengi imepumbazwa na kudhani watatawala milele ndio maana wanafanya vitendo vya kinyama kwa vile wanajua hakuna wa kuwafanya kitu.
 
Mbele ya CCM binaadamu wote si sawa..kuna wanaostahili vifo na mabalaa(WAPINZANI)...na pia kuna wanaostahili kuishi kama peponi...(WATAWALA)..hauhitaji kuwa na lundo la vyeti vya kitaaluma kuigundua hali hiyo bali ni kwa kutumia milango yako ya fahamu tu na kufuatilia mtiririko wa matukio utaona ni jinsi gani serikali ya CCM walivyo wanyama.....
Wakati sisi wanyonge tukishuhudia ndugu zetu wapendwa wakitufia mikononi mwetu kutokana na huduma mbovu na ukiritimba uliokithiri katika vituo vya afya pamoja na ukosefu wa madawa na vifaa tiba...wao na familia zao na wapambe wao hata wakijikata na kisu jikoni wanakimbizwa ulaya....
Wakati sisi wanyonge wakitujengea majengo wanayoyaita shule huku uakiwa hayana sifa ya kuwa shule kwa maana hakuna walimu, vitendea kazi, wala vitabu chini ya mtaala mbovu..watoto wao na wa familia za wapambe wao..wanawapeleka kwenye shule za kimataifa zenye walimu wengi mpaka mtoto akikohoa atauliza ulikuwa unasemaje...??
Wahenga walipata kusema kuwa..hakuna marefu yasiyokuwa na ncha...naamini kabisa iko siku tutashuhudia anguko kuu la CCM kama si mimi mwenyewe basi hata vitukuu vyangu...litakuwa ni anguko kuu ambalo halijapata kutokea nchini kwetu....
TIME WILL TELL

:thumbup::thumbup::thumbup:
 
Nakushukuru sana kwa kuleta huu uzi,siku chache nilipojiunga jamii forum nilileta uzi uliosema tampata vipi waziri wa mambo ya ndani ili nimtajie waliomuua diwani wa CCM kata ya Bugarama Kahama. Mungu ni mwema baadhi ya waliomuua mmoja alikufa katika tukio la ujambazi mwaka juzi na diwani aliyewakodi kumuua huyu diwani marehemu (PAUL KISIMIZA mwenyeji wa kijiji cha Buyange) nae mwanzoni mwa huu mwaka alikutwa amekufa pekee yake chumbani ndani ya gesti moja mjini Shinyanga. Chanzo cha mauaji ni baada ya huyo marehemu kumshinda katika kura za maoni ndani ya chama (CCM) huyu diwani aliyefia gesti Shinyanga. Pesa ya kuwalipa hao wauaji aliuza uwanja mmoja uliopo kijiji cha Bugarama pia mganga wa jadi aliyekuwa na jukumu la kuwaosha dawa wauaji bado yupo hapo kijijini Bugarama. Kwa kifupi kama ningepata maelezo ya kutosha hakika ningewataja wote mbele ya waziri kwani niliona kwenda polisi ningehatarisha maisha yangu bure. Kumbuka hadi huyu diwani anafia gesti alikuwa amekimbia makazi yake yaliyopo Bugarama. Kwa sasa niko Mbeya katika kusaka maisha siku nikitua Dar lazima nijaribu tena kumuona Waziri wa mambo ya ndani ili hawa waliobakia wapitiwe kabla ya uchaguzi huu.
 
Huwa siamini story za polisi ..kwanza nimwala rushwa wakubwa..kesi zao ni za kukungaunga tu ..mxxxx
 
Back
Top Bottom