Waliomaliza JKT wadai watajiingiza kwenye ujambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliomaliza JKT wadai watajiingiza kwenye ujambazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 22, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Waliomaliza JKT wadai watajiingiza kwenye ujambazi

  Fredy Azzah na Vicky Kombe


  BAADHI ya vijana waliomaliza mkataba wa mafunzo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Desemba 25 mwaka jana, wamelowea jijini Dar es Salaam kwa madai ya kusaka ajira ili kufanikisha maisha yao.


  Pamoja na uamuzi huo, vijana hao walidai wanaishi kwa taabu, baada ya kukosa mahali pa kulala, kukosa chakula na kujikuta wakizurura usiku kucha mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.


  Baadhi ya vijana hao waliozungumza na Mwananchi, walisema wanalazimika kutembea kwa makundi nyakati za usiku kutokana na kutokuwa na mahali za kulala na hivyo kuamua kuwa kwenye makundi hayo hadi asubuhi kutokana na kuhofia kuitwa vibaka kama watakuwa mmoja mmoja.


  "Haya maisha tunayoishi siyo ya kuishi binadamu wa kawaida kaka, sisi tunajiunga kwenye makundi ya watu kama saba au zaidi, halafu tunazunguka usiku kucha, tunafanya hivi, kwasababu tumetoka katika mikoa mbalimbali na hapa mjini, wengi wetu hatuna ndugu, kwahiyo bora tuwe katika makundi na kuzunguka usiku wote, ili tusijikusanye mahali pamoja," alisema Juma Saidi Juma (27) ambaye ni mwenyeji wa songea.


  Juma alisema mwaka jana , vijana karibu 1, 500 walimaliza mafunzo ya miaka mitatu Mugulani na kwamba karibu vijana 500 kati ya hao wapo jijini Dar es Salaam wakihaha kutafuta ajira za ulinzi kwenye kampuni mbalimbali.


  Wakati vijana hawa wakieleza hayo, baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliowaona vijana hao wakizunguka nyakati za usiku walisema, kama serikali haitawaangalia vijana hao, wataweza kujenga genge kubwa la majambazi wa kutumia silaha.


  Vijana hao ambao walisema wanapatikana kwa wingi mitaa ya Tunisia Kinondoni, mitaa ya Chang'ombe na Kariakoo walisema baada ya kumaliza mafunzo ya uzalishaji mali JKT kwenye vikosi mbalimbali vilivyopo nchini , waliambiwa warudi nyumbani mwaka jana.


  "Tulipewa nauli kila mmoja ili turudi kwatu, kwa wale wa Dar es Salaam pamoja na kulitumikia jeshi kwa miaka miwili, hakuna aliyepewa nauli iliyozidi Sh500 na sisi wa mikoani tulipewa nauli za kutosha kutufikisha majumbani kwetu," alisema Focus Stanley kutoka Musoma na kuongeza:


  "Mimi nimetoka nyumbani miaka mitatu iliyopita, leo unaniambia nirudi huku nikiwa sina chochote niende kufanya nini kijijini, mimi nimefundishwa kutumia silaha, siwezi kurudi kijijini, sanasana nitaendelea kukaa hapa mjini, niendelee kutafuta kazi na nikikosa, lazima nitajiingiza katika ujambazi," alisema kijana huyo.


  Msemaji wa Jeshi la Wananchi na JKT, Luteni Kanali Kasambala Mgawe alipoulizwa juu ya suala hilo, alisema lengo la JKT ni kufundisha vijana uzalendo na ukakamavu.


  "Mgambo wamekuwa wakifundishwa kutumia silaha tangu miaka ya 70, sijawahi kusikia hata watu wakisema kuwa mgambo ni chanzo cha ujambazi, lakini hata maafisa wajeshi huwa wakistaafu hawawi nyang'anyang'a wanaweza kufanya wizi lakini hawafanyi," alisema Luteni Mgawe.


  Hata hivyo alisema jeshi hilo halipaswi kulaumiwa juu ya ajira za vijana hao bali serikali inapaswa kujua vijana hao wataenda wapi mara baada ya kuitimu mafunzo yao.


  "JKT haiwezi kuajiri vijana wote kwenda TPDF (JWTZ), kwa mfano tutakapoanza kuwachukua vijana hawa kwa mujibu wa sheria kwa kila awamu tutakuwa tunachukua vijana 10,000 ina maana kwa mwaka tutawachukua vijana 20,000 sasa wote hawa jeshi haliwezi kuajiri na sisi tuna sheria zetu," alisema Luteni Mgawe na kuongez
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Jan 22, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hatari, hatari silaha zilivyotapakaa kule mipakani kweli inatisha, na Mungu apishie mbali huu mpango wa hao vijana uwe tisha toto. maana bunduki Kigoma na Karagwe huuzwa kati ya dola 5-25 (USD) KWA MTUTU.
   
Loading...