Waliolitumia Jeshi la Polisi vibaya na kulifanya lionekane la ovyo ndio wanaolituhumu sasa

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,968
Ni jambo la kushangaza. Wale wale waliolitumia jeshi pa polisi vibaya kwaajili ya manufaa yao ndio wao tena wanaolituhumu na kutaka lichunguzwe.

Ni wazi CCM ndiye mnufaika mkuu wa matumizi mabaya ya jeshi la polisi dhidi ya wapinzani. Leo anainuka katibu wa propaganda kutaka lichunguzwe.

Lakini ni jeshi hilo hilo linalozuia mikutano ya wapinzani, kuwapiga, kwafungulia mashtaka fake na hata kuuwa kwaajili ya kuilinda CCM hadi wananchi wakalibatiza jina Policcm.

Wakati wapinzani wakiugulia maumuvu ya jeshi la polisi CCM yenyewe imekuwa kama mziwanda anayedekezwa na kufanya lolote bila kuzuiwa wala kuingiliwa na mtu.

Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dsm ni miongoni mwa viongozi wa serikali waliolitumia vibaya sana jeshi la polisi kwa kuwabambikia watu kashfa za madawa ya kulevya, kukamata na kuwaweka ndani watu bila hatia, kuvamia vyombo vya habari nk lakini laajabu leo naye anasema jeshi la polisi ni baya.

Sabaya naye ni mmoja wa viongozi waliolitumia jeshi la polisi vibaya sana kwa manufaa binafsi.

Kimsingi wanaofanya jeshi la polisi lionekane la hovyo ni viongozi wa serikali na siyo polisi wenyewe kwakuwa wao kazi yao ni kutii na kutekeleza amri na ndiyo nidhamu ya jeshi.

Viongozi ndio wanaowaaambia polisi mkamateni kiongozi fulani wa upinzani kishamfungulieni mashtaka.

Hakunza zaidi
 
Hii nchi itakuja kuwa kama Bangladesh au India, wenye Mamlaka na nguvu ya pesa ndio wanaoweza kuwa na sauti na kusikilizwa, maskini hapati nafasi hata kidogo.

Mnachokitafuta mtakuja kukipata badae, ngojeni watanzania wawachoke.

Bomu la vijana wasiokuwa na ajira, waliokaa tu bila shughuli yoyote litakuja kuwalipukia hamtoamini, vijana nawaona taratibu wanapoteza uzalendo.

Mtu akiajiriwa na mashirika ya nje anaona poa tu hata akiharibia nchi maana anaona kama selikari imemtupa, sasa imagine Huyu kijana akipewa silaha....!!
 
Tujikumbushe kidogo jinsi jeshi hilo linavyotumika kama toilet paper:

Hapa ilikuwa ni sherehe fupi baada ya jeshi hilo kutekeleza kwa mafanikio makubwa maagizo ya kupora chaguzi kutoka kwa Bashite.
3hc9.jpg
 
Back
Top Bottom