Waliokuwa wafanyakazi New Habari waitaka Serikali imshinikize Rostam Aziz awalipe madai yao. Kuandamana nyumbani kwa Rostam na Bashe

Ilikua kampuni kubwa sana nini?, Rostam kainunua toka kwa ulinwengu, haizidi hata miaka kumi nyuma,,, leo inadaiwa bilioni 3tena za mafao,, kwa wafanyakazi 200 tu,,
Mbona hesabu hazikai sawa?

Hapa ndipo Ulimwengu alipotajwa kuwa hiyo kampuni ilikuwa yake na ndiye aliyemuuzia Rostam Aziz!! Ndio sababu ya kuulizia kama kulikuwa na malimbikizo ya hizo stahili!!
 
Halafu huyu Rostam ndo kapata asilimia nyingi Williamson Diamonds Mwadui. Yaani nawaonea huruma wafanyakazi. Mafisadi makubwa haya Rostam na huyu msomali Bashe.
Na bado inasemekana hata huko North mara kupitia kampuni ya Caspian maana inasemekana kuna mkono wako pia amepewa tenda ya kufanya uchimbaji kwenye pit ya rama kazi wanayo hao staff wake
 
Hivi wandishi wa habari ni vilaza kiasi hiki?
Hawajui hatua za kufanya?
Shauri hili lafaa kupelekwa wizara ya kazi na wawe na mwanasheria.
Wewe ndo kilaza, akili yako inafikiri wafanyakazi wote kwenye makampuni na mashirika ya habari ni waandishi wa habari?
Kuna wahudumu Hadi ma engineer wa mitambo pale.
 
Acha kuchanganya mada. Ulimwengu anamiliki kampuni inayotengeneza Raia Mwema. Hajawahi kuwa mmiliki wa Habari House.
Habari corporation iliwahi kumilikiwa na wakina Ulimwengu, Rweyamamu etc ikiwa na magazeti ya Rai na mengineyo baadae ndipo akamuuzia Rostam na kipindi hicho Rostam ana bifu na R. Mengi mbaya kabisa wakiitana Fisadi papa vs Fisadi nyangumi Nilidhani alinunua hivyo vyombo ili apambane na Mengi aliyekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kumpa madongo
 
Halafu huyu Rostam ndo kapata asilimia nyingi Williamson Diamonds Mwadui. Yaani nawaonea huruma wafanyakazi. Mafisadi makubwa haya Rostam na huyu msomali Bashe.
Na awamu ya 5 alionekana bonge la mzalendo!! Mbele ya shujaa wao wa Afrika
 
Habari corporation iliwahi kumilikiwa na wakina Ulimwengu, Rweyamamu etc ikiwa na magazeti ya Rai na mengineyo baadae ndipo akamuuzia Rostam na kipindi hicho Rostam ana bifu na R. Mengi mbaya kabisa wakiitana Fisadi papa vs Fisadi nyangumi Nilidhani alinunua hivyo vyombo ili apambane na Mengi aliyekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kumpa madongo
Ah sawa sawa nishakumbuka ni kweli enzi za Rai. Zama za Mkapa.
 
ROSTAM AZIZ AKUBALI YAISHE

👇👇👇

Habari za jioni Wapambanaji.
Nichukue fursa hii kuwashukuru wote waliofanikisha tukio letu la Press Confernce juzi.

Tunamshkuru Mungu Press imekuwa na positive impact kila mahali na hata wanaojifanya kujitetea hawana hoja.

Muhimu na kubwa tumefanya kikao na Rostam Aziz amekubali kutulipa mafao yetu mara moja. Amekubali kutukabidhi kesho cheque 2 ambazo1. NSSF & PSSSF (tumeziona na kuverfy benk).

Atuma mwakilishi kuwasilisha cheque hizo mbele ya waandish wa habari leo Jumamosi saa 4:00 asubuhi Landmark Hotel. Tumepzipokea na sasa tutaziwasilisha kwa wahusika
 
Mwenyekiti akionesha Hundi zilizoandikwa na RIstam Aziz kwenda mifuko ya Hifadhi NSSF na PPF kulipa madai Yao.

IMG_20220205_152608_717.jpg
 
Wafanyakazi zaidi ya 200 waliokuwa wameajiriwa kwenye kampuni ya new habari(2006) limited inayomiliki magazeti ya Mtanzania na mengine wameiomba Serikali imshinikize mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz kuwalipa fedha zao ambazo ni mafao yao.

Msemaji wa wafanyakazi hao, Arodia Peter amesema wanaomba taarifa zao zimfikie Rais Samia baada ya mwajiri wao ya New Habari inayomilikiwa na Rostam Aziz chini ya afisa mtendaji mkuu, Hussein Bashe ambae sasa ni waziri wa kilimo kwa kushindwa kuwapelekea mafao yao kwenye mifuko ya hifadhi ya kijamii.

Msemaji amedai Rostam Aziz kupitia kwa mtendaji mkuu, Hussein Bashe waliwaondoa kazini Mei 31, 2019 bila kuwalipa stahiki za mafao kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na iliyokuwa PPF kwa mujibu wa sheria.

Pia wamedai mwajiri wao aliwaondoa kazini kwa lazima wafanyakazi wake bila kutangaza kwa umma pia sababu za kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Lakini pamoja na hatua ya kuwaondoa hawajawalipa mafao kama ambavyo walikuwa wamewaahidi.

View attachment 2106502

=====

UPDATES: 05 Februari 2022

======

Baada ya Masaa 24 Toka Wanaodai Mafao kuongea na Wanahabari, Hatimaye Wafanyakazi Wamekiri kwamba Rostam Aziz kawalipa Mafao yao.

Wakati akosoma taarifa kwa vyombo vya Habari, Arodia Peter amesema kwamba juzi baada ya kuongea na vyombo vya habari, Rostam Aziz aliwaita kwa kikao cha dharura. Rostam alisema alikuwa hana habari kama anadaiwa, hivyo muda huo huo akafanya Malipo yote waliyokuwa wakidai ikiwemo Mafao kwenye mifuko ya Jamii.

Wafanyakazi wa New Habari ambayo inamiliki Magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwa, Dimba na The African, Walikuwa wanazungushwa kulipwa mafao yao kwa miaka Mitatu baada ya kuachishwa kazi.

Pia, soma: Rostam Aziz akubali yaishe, atoa hundi za malipo ya waliokuwa wafanyakazi wa New Habari (2006)
Haya maumivu muda si mrefu yatahamia kwa iliyokuwa Tigo/Zantel, wafanyabisahara wetu hawa matycoon wanaishi kiujanja ujanja sana hasa kwenye hizi banana republic
 
Back
Top Bottom