Waliokuwa wafanyakazi New Habari waitaka Serikali imshinikize Rostam Aziz awalipe madai yao. Kuandamana nyumbani kwa Rostam na Bashe

Kampuni si ni an individual ?

Filisi kampuni kama bado ipo mchukue cha kwenu..., itakuwa sio hekima pesa itoke Williamson Diamond au Taifa Gesi ili iweze kulipia huku
Naona umetaja mali za Rostam
 
Haya mambo ya kuajiriwa na kampuni ambayo haina uwezo kudumu muda mrefu hukatisha tamaa kufanya kazi nayo. Rostam na Bashe hawakuona kuvuna kampuni ghafla kungeathiri vibaya wafanyakazi wao? Haya makampuni ya mifukoni mwa wenyewe yanakera sana katika suala la malipo kwa wafanyakazi wao
 
Wafanyakazi zaidi ya 200 waliokuwa wameajiriwa kwenye kampuni ya new habari(2006) limited inayomiliki magazeti ya Mtanzania na mengine wameiomba Serikali imshinikize mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz kuwalipa fedha zao ambazo ni mafao yao.

Msemaji wa wafanyakazi hao amesema wanaomba taarifa zao zimfikie Rais Samia baada ya mwajiri wao ya New Habari inayomilikiwa na Rostam Aziz chini ya afisa mtendaji mkuu, Hussein Bashe ambae sasa ni waziri wa kilimo kwa kushindwa kuwapelekea mafao yao kwenye mifuko ya hifadhi ya kijamii.

Msemaji amedai Rostam Aziz kupitia kwa mtendaji mkuu, Hussein Bashe waliwaondoa kazini Mei 31, 2019 bila kuwalipa stahiki za mafao kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na iliyokuwa PPF kwa mujibu wa sheria.

Pia wamedai mwajiri wao aliwaondoa kazini kwa lazima wafanyakazi wake bila kutangaza kwa umma pia sababu za kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Lakini pamoja na hatua ya kuwaondoa hawajawalipa mafao kama ambavyo walikuwa wamewaahidi.

View attachment 2106502
Nahisi ndio suluhu na ole wao waende mahakamani ndo watajua hawajui
 
Halafu huyu Rostam ndo kapata asilimia nyingi Williamson Diamonds Mwadui. Yaani nawaonea huruma wafanyakazi. Mafisadi makubwa haya Rostam na huyu msomali Bashe.
Nayeye alikuwa anawadai Petrus Diamonds waendeshaji wa Williamson Diamonds,pesa za huduma za uzalishaji kwa muda mrefu bila kumlipa,na wameshindwa kumlipa,ikabidi wamalizane kwa kumpa gawio la hizo asilimia..
 
Ilikua kampuni kubwa sana nini?, Rostam kainunua toka kwa ulinwengu, haizidi hata miaka kumi nyuma,,, leo inadaiwa bilioni 3tena za mafao,, kwa wafanyakazi 200 tu,,
Mbona hesabu hazikai sawa?
Labda alinunua ikiwa na madeni.. lakini pia bilioni 3 Kwa wafanyakazi 200 miaka 10 bado sio kubwa tukisema kila mfanyskazi anadai ml 15 tukizidisha na hiyo idadi ya watu 200 unaangukia hapo kwenye bl 3
 
Ilikua kampuni kubwa sana nini?, Rostam kainunua toka kwa ulinwengu, haizidi hata miaka kumi nyuma,,, leo inadaiwa bilioni 3tena za mafao,, kwa wafanyakazi 200 tu,,
Mbona hesabu hazikai sawa?

Je hayo mafao ni malimbikizo toka wakati mmiliki wake alikuwa Ulimwengu?
 
Back
Top Bottom