Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,707
- 71,017
Tumemsikia Waziri wafedha Mwigulu akitamka kuwa asemayo mama Samia kuhusu ukusanyaji kodi ni sahihi kabisa kwani utumiaji wa ubabe na hila sio njia nzuri (kama alivyokuwa anaunga mkono utendaji wa JPM), na Kigwangalla naye amepingana wazi leo na kauli alizokuwa anaziunga mkono kwa bidii kuhusu Nyungu na kujifukiza kuwa ni njia primitive zisizo na utafiti wa kisayansi tofauti kabisa na vigelegele walivyopiga kwa JPM. Funga kazi ni Nape Nnauye aliyefyatuka na kusema utawala wa sasa ni mzuri sana tofauti na uliopita.
Jee mawaziri hawa wa zamani na sasa wanataka kutupa ujumbe gani? Walikuwa wanaburuzwa na Jiwe au walikuwa wanamnafikia tuu?
Au kuna nini humo ndani ya chungu?
Jee mawaziri hawa wa zamani na sasa wanataka kutupa ujumbe gani? Walikuwa wanaburuzwa na Jiwe au walikuwa wanamnafikia tuu?
Au kuna nini humo ndani ya chungu?