Waliokuwa Mawaziri Watiifu wa JPM Kumgeuka Sasa inaashiria Nini?

ukosefu wa maadili
You put it very well...Siyo ya kuchekea haya...Huyu mtu lazima hata tume ya maadili ihakikishe hapati nafasi yeyote ile ya kuongoza umma wa watanzania...Hawa watu ndiyo ambao wanatuingiza kwenye mikataba ya ajabu ajabu kisha tu anasikilizia upepo unaelekea wapi
 
Chawa wanatafuta mwelekeo kwa nguvu sana , maisha haya bana , wanasiasa sio mchezo .
Screenshot_20210329-172251.png
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mwenyezi Mungu anatupenda sana Watanzania kwa kufupisha awamu ya dhalimu na dhulmat jiwe. Sipati picha angekaa hadi 2025 au 2027 na kupewa ufalme wa kutawala milele. Furaha ya Watanzania wengi taratibu imeanza kurudi na hofu kupungua. Mwenyezi Mungu Mkubwa 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
Wacha tusherehekee Pasaka na muujiza wa karibuni.Mataifa mengine hulipa garama kubwa ya mateso na damu kwa miaka mingi zaidi kuondokana na viongozi wa namna hii.
 
Kuna watu kama johnthebaptist Ngojeni 21 days ziishe mtaona jinsi watakavyo mgeuka "shujaa wao wa dunia" mpaka mtashangaa!
Wafuasi wa ccm ni bora kufuga kuku watakutagia mayai iwe lishe ya watoto kuliko kuwa nao umewafuga zizini, watakusaliti tuu
 
Maccm ni mafisi na pia wanafiki wakubwa.
1617557663924.jpeg

Tumemsikia Waziri wafedha Mwigulu akitamka kuwa asemayo mama Samia kuhusu ukusanyaji kodi ni sahihi kabisa kwani utumiaji wa ubabe na hila sio njia nzuri (kama alivyokuwa anaunga mkono utendaji wa JPM), na Kigwangalla naye amepingana wazi leo na kauli alizokuwa anaziunga mkono kwa bidii kuhusu Nyungu na kujifukiza kuwa ni njia primitive zisizo na utafiti wa kisayansi tofauti kabisa na vigelegele walivyopiga kwa JPM.

Funga kazi ni Nape Nnauye aliyefyatuka na kusema utawala wa sasa ni mzuri sana tofauti na uliopita.
Jee mawaziri hawa wa zamani na sasa wanataka kutupa ujumbe gani? Walikuwa wanaburuzwa na Jiwe au walikuwa wanamnafikia tuu?
Au kuna nini humo ndani ya chungu?
View attachment 1743323View attachment 1743332View attachment 1743344
 
M adi leo siamini kama Mwigulu kawa waziri wa fedha ...hapa tutarajie nchi kuwa katika uchumi wa mtu mmoja mmoja.
 
Mwenyezi Mungu anatupenda sana Watanzania kwa kufupisha awamu ya dhalimu na dhulmat jiwe. Sipati picha angekaa hadi 2025 au 2027 na kupewa ufalme wa kutawala milele. Furaha ya Watanzania wengi taratibu imeanza kurudi na hofu kupungua. Mwenyezi Mungu Mkubwa 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
VP naona kama anachukua mikoba.
 
Tena matumbo ya hatari ambayo hata yanaweza kuuza nchi mchana kweupe kwa maslahi binafsi...Mtu kama huyo utamwaminije kwenda kunegotiate kwenye chumba cha kuta nne eti akatetee maslahi ya watanzania?
Nchi yangu nzuri Tanzania, ina watu wapole, watiifu, wakarimu, wasikivu sana. Ona aina hii ya viongozi,leo anakuambia hivi, hata kabla ya mwezi, kesho anageuza hivi. Wananchi huku chini nangulukulu mpaka tunachanganyikiwa
 
Hapo bado 21 za maombolezo, baada ya hapo tutasikia uwanja wa ndege wa Chato ubomorewe unaingizia hasara nchi, hifadhi ya wanyama ya bulegi ianzishwa kimakosa, Ee Mungu umeamua kuwafunulia watanzania mambo makubwa, viongozi kupitia CCM walivyo. Hivi huyu mama anawaona, anawasikia? sisi tunamshukuru Mungu tu, tunaona, tunasikiliza na tunahifadhi, wanajua kupretend kaah, hata hawana uoga.
Inaumiza Sana! Kigwangala sahau kurudi bungeni 2025!! Maana si kwa usaliti huo!! Unafiki wa kiwango Cha PhD!! Mapema kiasi hiki? Siyo siri, inauma sana!
 
Mama ana la kujifunza.
Asije akadhani wanaomwita mama, mama wote ni wazuri naona sasa naona viumbe tulivyo, ningekuwa mimi ndio Kingwangwala au Nape nisingesema hayo yote inaonyesha walivyo wanafiki, ina maana hata wa sasa watakuja kumnanga akiwa hana madraka, nakumbuka wimo wa '' wanadamu si wazuri'' nadhani aliimba Bitchuka
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mama jihadhari na watu hawa! Kama Leo wanamvunjia heshima Marehemu Dr Magufuli watakufanyia hivyo na kuzidi wewe mwenyewe siku moja!! Wapige mkasi!!
 
Kuna watu kama johnthebaptist Ngojeni 21 days ziishe mtaona jinsi watakavyo mgeuka "shujaa wao wa dunia" mpaka mtashangaa!
Wafuasi wa ccm ni bora kufuga kuku watakutagia mayai iwe lishe ya watoto kuliko kuwa nao umewafuga zizini, watakusaliti tuu
Hahahaaaa....... Sisi tuliwachagua Magufuli na mama Samia 2020 bwashee!

Kwa sasa tunampa ushirikiano wa 100% Rais Samia na makamu wake Dr Mpango kama tulivyompa alipokuwa na Magufuli
 
Inaumiza Sana! Kigwangala sahau kurudi bungeni 2025!! Maana si kwa usaliti huo!! Unafiki wa kiwango Cha PhD!! Mapema kiasi hiki? Siyo siri, inauma sana!
Kaamua awawahi machawa wengine, maana kaona Henry James kashavuka kihuzi mmemsahau... na yeye anaamini upepo tu ikifika Siku mbili tatu mtamsahau halafu ndio hawa wanasema vijana waji ajiri, nachokiona sasahivi kila mtu atataka afanye siasa maana watu wameshtuka kulikoni?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom