Waliokufa Ajali ya Meli Zanzibar Ni 1696?

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
WAKATI habari zikisema Waziri wa Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Hamad Masoud Hamad, amesema yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake kutokana na ajali ya meli ya Spice Islander iliyozama hivi karibuni katika eneo la Nungwi na kuua mamia ya watu, Chama cha Wananchi (CUF), kimesema watu waliokufa katika ajali hiyo, ni zaidi ya 1696.

Source: mzalendo.net

inawezekana burner, coz hata waokoaji si wamesema waliookolewa ni wale tu waliokuwa juu juu kama chuwa za mchele. mchele wenyewe ndo umo ndani ya boti wote umezama. kwa sasa hakuna mwenye uwezo wa kutoa takwimu sahihi juu ya wangapi wamekufa ila wanao uwezo wa takwimu juu ya wangapi wameokolewa hai ama wamekufa.

nachojua wamekufa watu wengi coz tunasikia na kusoma wale wahanga wakisema wamepotelewa na ndugu zao,naona watu wangeorodheshwa wale waliopotelewa na ndugu tungepata idadi kamili

Basi hii ni ajali kubwa kuliko ile ya MV Bukoba.
Mkuu, ajali ya MV Bukoba ni kuwa hata ukiwauliza wale waliopona kwenye MV Bukoba watakuambia waliopatikana na wachache kuliko waliopotea.
Kuna watu wa Bukoba na Mwanza wanasema watu waliofariki kwenye MV Bukoba ni zaidi ya 2500

Sasa hii nchi inaelekea wapi, kila kitu uchakachuwaji... Mi nachoka kabisa.

Wale wasauzi kungepatikana watu makini wa kuwahoji tungeujua ukweli ambao ni wasiwasi mkubwa umefichwa. Sitaki kuamini eti walishindwa kufikia meli kwa sababu ya kina kirefu...inawezekana baada ya kureport kwa watawala walioyaona huko chini ndio wakaambiwa wasiendelee ili kukwepesha aibu. Ipo siku kuna mtu/watu watatakiwa kujibu yote haya!

This is what Plato calls a Noble Lie, That it is permissible for the Leader to lie in certain environment!

mkuu, ajali ya mv bukoba ni kuwa hata ukiwauliza wale waliopona kwenye mv bukoba watakuambia waliopatikana na wachache kuliko waliopotea.
Kuna watu wa bukoba na mwanza wanasema watu waliofariki kwenye mv bukoba ni zaidi ya 2500

ndo tz yetu. Kumbukumbu hatuwezi ama mafisadi wanajiosha ili madudu yao tusiyashitukie.

Wale wasauzi kungepatikana watu makini wa kuwahoji tungeujua ukweli ambao ni wasiwasi mkubwa umefichwa. Sitaki kuamini eti walishindwa kufikia meli kwa sababu ya kina kirefu...inawezekana baada ya kureport kwa watawala walioyaona huko chini ndio wakaambiwa wasiendelee ili kukwepesha aibu. Ipo siku kuna mtu/watu watatakiwa kujibu yote haya!
Hapana!
Wale jamaa hawakuja au hawana vifaa vya kuzamia mkondo wa Nungwi.Umewahi kupita lile eneo!.Maji yako meusii na saa nyengine bluu.Ile meli ilikuwa na nondo za kujengea nyingi na sukari na ilianza kuzama kwa nyuma hivyo imekwenda kama chubwi,unaijua!.

Unajuwa ukizamia na vifaa duni unaweza kupoteza maisha mwenyewe bure!.

Angalia DEEP DIVING

labda! Lakini wao walikuja kufanya nini? Na wanajeshi wetu pia hawana vifaa?

mpaka mwaka huu tutayaona menge yenye kusikitisha na kudhihirisha ulegelege wa serikali usiokuwa na kuwajibishwa

Wale wasauzi kungepatikana watu makini wa kuwahoji tungeujua ukweli ambao ni wasiwasi mkubwa umefichwa. Sitaki kuamini eti walishindwa kufikia meli kwa sababu ya kina kirefu...inawezekana baada ya kureport kwa watawala walioyaona huko chini ndio wakaambiwa wasiendelee ili kukwepesha aibu. Ipo siku kuna mtu/watu watatakiwa kujibu yote haya!
yani hapa mimi nimebaki na kicheko,wanatudanganya kitoto kabisa,ina maana wakati wasouth wanakuja hawakujua kina cha maji maeneo ya nungwi?siamini kama wataalamu hawa wanafanya kazi kwa kubahatisha namna hii.kuna tatizo gani tukisema waliokufa ni 1000+ halafu tukajua chanzo cha ajali na kujaribu kukabiliana nacho?au ndio tuseme "a matter of national security"

• Thanks
Reactions: SMU
nachojua wamekufa watu wengi coz tunasikia na kusoma wale wahanga wakisema wamepotelewa na ndugu zao,naona watu wangeorodheshwa wale waliopotelewa na ndugu tungepata idadi kamili
Sijui tutaerevuka lini wiki nzima idadi ya wasiojulika waliko(dead and missing) haijulikani. From day 1 palitakiwa pawe na ofisi ya kuripoti wasafiri kwa majina afu waliookolewa na maiti zinapunguzwa pale,tunapata hata close estimate. Au serikali inaona walitaja idadi ndogo hawataaibika ?

Halafu tuacheni Uongo wa wazi na kuingiza siasa hata katika mambo mazito kama yale,
Huwezi kusema eti waliopatikana hai ni 600, maiti 200 halafu eti wengine "hajulikani waliko" maana yake nini?
Hili kundi la tatu linatoka wapi hili?
Huku ni ku-minimize tu takwimu za waliofariki!!!
Pale sio msituni eti uweze kusema labda mmepoteana, mtakutana mbele ya safari, pale ni kwenye maji ati!!
Makundi ni mawili tu, walioko hai, kama mtu hayupo kati kundi hili basi ni marehemu, sasa labda katika group hili la marehemu ndio wagawe sub-groups za marehemu waliopatikana na wale waliobaki chini ya bahari.
Serikali iache siasa hata katika mambo yanayogusa jamii kama haya!!!!

Back
Top Bottom