Waliokua wameomba vyuo kupitia NACTE sasa rasmi muombe kupitia TCU kwa gharama mpya

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
646
1,187
Kuna maombi ya vyuo watu waliomba kupitia NACTE na kulipia gharama ya sh 50,000/= na hii iliwahusu zaidi wenye sifa za diploma kwa kuazia GPA 2.7, watu walilipa nonrefundable fees na baadae NACTE wakafunga tovuti,
NACTE walifunga tovuti baada ya TCU kutoa utaratibu mpya wa sifa za udahili ambapo kwa form 6 muombaji anatakiwa awe na DD2 ama CE ambazo ni jumla ya point 4, ambapo zamani ilikua minimum EE2, kwa upande wa wenye diploma kwa mujibu wa mwongozo mpya wa TCU lazima sifa awe na minimum GPA 3.5 wakati zamani ilikua 2.7,

NACTE ilitangaza sifa ni 2.7 na watu waka apply ila TCU imebadili mwongozo lazima uanzie GPA 3.5, na wote inatakiwa wa apply kupitia TCU,

Sasa kwa wale waliokua wameomba kupitia NACTE kwa ule mwongozo wa 2.7 umefutwa na kwa sababu walisema pesa ya application ni nonrefundable basi anza kua apply kupitia TCU kwa gharama mpya tofauti na hapo chuo utakisikia kwa rafiki yako,
Pia kama ulia apply kupitia NACTE ukiwa unanzia GPA 2.7 basi usihangaishe pesa yako maana utakua umepotesa laki moja nzima, GPA inayotakiwa na TCU sasa hivi ni kuanzia 3.5
 
wanapaswa kurudisha hizo hela za wale walio na GPA below 3.5maana waliaapply kabla ya TCU kutoa tamko..zen ningependa kujua ni taasisi gani nchini inayoongoza huu mtaala wa elimu kati hizi,,wizara ya elimu,NACTE,TCU,
 
Jamani huko duniani kuna vyuo maalufu kama Havard university na Oxford university, je hizi point za EE2 unaweza dahiliwa au sisi ndo tunadahili aina hii ya ufaulu??
 
Elimu ya Tz ni kama gari yenye mfumo wa manual,
Mlimani unakanyaga clutch unaludi mbili,then moja;mteremkoni unakanyaga tena then unaruhusu free, chini ya mlima unatoa free then unaipa moja, mbili taaaatu,,, kaz kuwai sasa, mlimani, mtelemkoni au chini ya mlimaa, sa hivi ni mlimani
 
Kwa mwendo wa GPA ya 3.5 kuipata kupitia Diploma sio kazi rahisi, embu tafuteni utaratibu mwingine ili watu waendelee kusoma.
 
Hii haitakaa muda mrefu lazima watarudisha grade za zamani tu vyuo vingine havitapata watu kuna course zingine ni ngumu sasa mtu upate vipi 3.5 kama vipi wangeweka hata 3--- ila kwa walichofanya wamekosea
 
Muda utazungumza...hivi nacte wako chini ya tcu...

Nacte wanahusika na institute tcu wanahusika na universities why nacte amsikilize tcu.??
 
Kuna maombi ya vyuo watu waliomba kupitia NACTE na kulipia gharama ya sh 50,000/= na hii iliwahusu zaidi wenye sifa za diploma kwa kuazia GPA 2.7, watu walilipa nonrefundable fees na baadae NACTE wakafunga tovuti,
NACTE walifunga tovuti baada ya TCU kutoa utaratibu mpya wa sifa za udahili ambapo kwa form 6 muombaji anatakiwa awe na DD2 ama CE ambazo ni jumla ya point 4, ambapo zamani ilikua minimum EE2, kwa upande wa wenye diploma kwa mujibu wa mwongozo mpya wa TCU lazima sifa awe na minimum GPA 3.5 wakati zamani ilikua 2.7,

NACTE ilitangaza sifa ni 2.7 na watu waka apply ila TCU imebadili mwongozo lazima uanzie GPA 3.5, na wote inatakiwa wa apply kupitia TCU,

Sasa kwa wale waliokua wameomba kupitia NACTE kwa ule mwongozo wa 2.7 umefutwa na kwa sababu walisema pesa ya application ni nonrefundable basi anza kua apply kupitia TCU kwa gharama mpya tofauti na hapo chuo utakisikia kwa rafiki yako,
Pia kama ulia apply kupitia NACTE ukiwa unanzia GPA 2.7 basi usihangaishe pesa yako maana utakua umepotesa laki moja nzima, GPA inayotakiwa na TCU sasa hivi ni kuanzia 3.5
Habari yako ni nzuri sana ila chanzo cha habari yako ni nini au wewe ni NACTE?
 
Hii haitakaa muda mrefu lazima watarudisha grade za zamani tu vyuo vingine havitapata watu kuna course zingine ni ngumu sasa mtu upate vipi 3.5 kama vipi wangeweka hata 3--- ila kwa walichofanya wamekosea
Uko sahihi sana. Wanataka wasome OPEN.... 1. 9 GPA MINIMUM ENTRY.
 
NACTE

9TH JUNE 2016 18:43:00

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI, DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) UNAORATIBIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

Date Posted: 9th June 2016 18:43:00 Posted By: NACTE

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI,

DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) UNAORATIBIWA NA

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

Tarehe 3 Juni 2016 ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya udahili wa kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada ya Kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) unaoratibiwa na NACTE.

Baraza linapenda kuwaarifu waombaji udahili wa kozi tajwa hapo juu na umma kwa ujumla kuwa, kwa sasa maombi yote yaliyowasilishwa mpaka tarehe 3 Juni 2016 saa sita usiku yameanza kuchambuliwa kwa ajili ya kuchagua waombaji wenye sifa stahiki. Zoezi la kuchambua waombaji udahili na hatimaye kuchagua waombaji wenye sifa stahiki na waombaji hao kuidhinishwa na mamlaka husika na kutangazwa litachukua muda wa wiki nne (4)kuanzia tarehe 3 Juni, 2016.

Baraza linatambua uwepo wa waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kuwasilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016. Waombaji wa namna hii na wengine wanaopanga kuwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) wanaombwa kuwa na subira mpaka hapo majina ya waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya kufungwa kwa mfumo watakapotangazwa.

Baada ya kutangazwa majina ya waombaji waliochaguliwa, Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) utafunguliwa tena kwa ajili ya kujaza nafasi za udahili ambazo zitakuwa hazijajazwa na waombaji waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi, 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016.

Baraza linatarajia kufungua tena Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwa ajili ya kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya Juu na Shahada ya Kwanza wiki ya mwishoni mwa mwezi wa Sita, 2016.

Imetolewa na

Ofisi ya Katibu Mtendaji

NACTE

Tarehe: 9 Juni, 2016

COMMENTS

QUICK / RELATED LINKS

Central Admission SystemTanzania Commission for UniversitiesTanzania National WebsiteHigher Education Students Loans Board (HESLB)National Examination Council of Tanzania (NECTA)Tanzania Institute of Education (TIE)Commission for Science and TechnologyVocational Education Training Authority (VETA)International Association of Universities (IAU)Center for Higher Education Transformation (CHET)

Stay Connected

2kSHARES 1.5kTWEETS 620SHARES200FOLLOWERS

CONTACT NACTE

The Executive Secretary,The National Council For Technical Education:plot No. 719/1/4,
Mikocheni Light Industrial Area,
P. O. Box 7109,
Dar-es-Salaam,
Tanzania.Tel: 255-22-2780077 / 255-22-2780079Fax: 255-22-2780060E-Mail: info@nacte.go.tzWebsite: www.nacte.go.tz

NACTE ZONES

LATEST UPDATES

June 23rd 2016 NACTE

PUBLIC NOTICE - SPECIAL SERVICE CONDUCTED BY NACTE TO GET FEEDBACK FROM VARIOUS STAKEHOLDERS REGARDING COMMENTS, NUISANCE, CHALLENGES IN ALL SERVICES DELIVERED BY THE COUNCIL

June 9th 2016 NACTE

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI, DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA (CAS) UNAORATIBIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

May 31st 2016 NACTE

NEWS STORY - NACTE IS CONDUCTING A WORKSHOP ON CBET - CURRICULUM DEVELOPMENT TO MWALIMU NYERERE MEMORIAL ACADEMY STAFF, AT NACTE HEADQUARTERS, FROM 30TH MAY - 3RD JUNE, 2016

MORE UPDATES ...

NACTE TWEETER UPDATES

Tweets by @nacte

FOLLOW US ON FACEBOOK

HOME

CONTACT GALLERY PUBLICATIONS

COPYRIGHT 2007 - 2015 THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION. ALL RIGHTS RESERVED
 
Naomba kuuliza nacte na tcu ni vitu viwili tofauti sasa nacte wanawezaje kuhamishia mfumo tcu bila kutoa taarifa make kwenye tovuti yao hakuna taarifa yoyote kuhusu tcu wala taarifa yyte kuhusu maombi ya vyuo ss hawa nacte ina maana wamejitoa kudahili wanafunzi kimyakimya anae elewa mambo yanaendaje anijuze
 
Back
Top Bottom