Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Jicho la tatu linaonesha kiu ya wanaodai katiba mpya ni madaraka na wanaosema iliyopo inafaa pia wanataka kubaki madarakani. Suruhisho ni nini!??
Katiba iliyopo na hata mpya inayopiganiwa haiwezekani kuwa kamilifu na timilifu kamwe hasa hasa itakayoandaliwa katika mazingira haya yenye kila aina ya mihemuko ya kisiasa
Rais aliyepo Sasa amejitahidi kwa kiasi kikubwa kuonesha kuwa katiba iliyopo ilikanyagwa kwa makusudi na mtangulizi wake. Mfano kesi za kubambikia, kuminya uhuru wa habari,nk.
Kumbe Rais anaweza kuamrisha kitu nje ya katiba na kikawa na asifanywe chochote!
Hapa Rais Samia anatupa ujumbe kuwa dawa si katiba mpya pekee! Anatueleza tuna jambo kubwa la kufanya zaidi ya kudai katiba mpya!
Nawiwa kujiuliza, hivi tunadhani hiyo katiba mpya itakuwa na uwezo kabisa wa kumfunga break Rais asiweze kutumia vyombo vya ulinzi na usalama atakavyo?
Tuna uhakika tukipata katiba mpya itakayoruhusu tume huru na kupunguza madaraka ya Rais na tukaendelea na aina ya watanzania hawa hawa, wasomi hawa hawa itamzuia huyo Rais kutumia vyombo vyake hivyo vichache atakavyopewa kikatiba kuingilia vyombo vingine au kuvunja haki za raia atakavyo?
Najua mtasema ndio atazuiwa na katiba na kutakuwa na uwezo wa kumshughulikia kwa kuvunja katiba!
Huenda mkawa sahihi, lakini tujiulize ni mara ngapi wanasiasa hawa hawa na makundi mengine yasiyo ya kisiasa yametueleza kuwa Rais aliyepita alivunja katiba na haki za raia kwa makusudi? Tulimfanya nini??
Huenda maswali yangu yanaonekana ya kizwazwa lakini yatafakari kwa kina
Mapendekezo yangu ni haya:-
1. Wanasiasa wajikite zaidi kutoa elimu ya uraia na kujitambua kwa wananchi na kuwajengea uwezo wa kujiamini na utambuzi wa haki zao. Katiba mpya bila elimu ya uraia itakuwa kazi bure!
Elimu ikitolewa na ikaeleweka, mwananchi atajua haki zake, atajua kuzidai na atajua kuzitetea na atazipigania kwa kujiamini. Halikadhalika viongozi watawaheshimu wananchi na wataongoza kwa adabu
2. Mchakato wa katiba mpya 2014 ulivurugwa na wanasiasa hawa hawa wanaoidai leo. Huu ni uthibitisho kuwa wanasiasa wanaweza wasituletee katiba nzuri kwasababu za kimaslahi.
Walioko nje watataka katiba itakayowapa fursa ya kuingia ndani na walioko ndani watapigania vipengere vitakavyowahakikishia kuendelea kubaki madarakani
Hapa mkatae mkubali lakini ukweli ndio huo! Watajificha nyuma ya kivuli Cha kuwatetea wananchi lakini mioyoni wana Jambo lao!
Kinachoweza kufanyika ni kuunda kamati maalumu ya katiba mbali na ile ya Warioba itakayowaweka pembeni wanasiasa lakini Kama itawapendeza wachukue yale maoni ya tume ya Warioba Kama Kuna cha kuboresha waboreshe Kama Kuna haja ya kuongezea watajua wenyewe
Kamati hiyo iongozwe na majaji wa mahakama kuu na wastaafu waliowahi kuwa majaji wa mahakama kuu pamoja na mawakili wabobezi
Wajumbe wengine watoke vyombo vya ulinzi na usalama wenye uzoefu wa kutosha. Hawa watasaidia kuweka vipengere vitavyodhibiti vyombo vya ulinzi na usalama.
Inaaminika taasisi uliyoitumikia Kuna mapungufu unayaona wazi lakini unashindwa kuyaziba kwasababu huna uwezo.
Wakiwepo hawa wataunda vifungu vitakavyosaidia polisi, magereza, Jwtz na TISS wasioonee watu, viongozi na watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuweka vipengere vitakavyolinda maslahi na weledi wa vyombo hivi
Wajumbe wengine watoke miongoni mwa waliowahi kuwa washauri wa Rais katika vipindi vyote.
Hawa watakuwa na nafasi nzuri ya kutoa uzoefu wao pale walipojaribu kushauri kitu either cha kuvunja katiba au kujaribu kuzuia katiba isivunjwe. Hawa watatoa uzoefu wa nini kinafanya Rais avunje katiba na nini kiwekwe kuzuia
Wajumbe wengine watoke ndani ya bunge. Hapa simaanishi wabunge. Wachukuliwe wale waliowahi kuwa makatibu wa bunge na waliowahi kuwa Maspika wa bunge au kuhudumu ndani ya ofisi ya Spika. Hawa watakuwa na nafasi nzuri ya kutoa mawazo yao wabunge wawe na sifa gani ili bunge liwe imara kusimamia serikali na vifungu gani viwekwe kulisuka bunge ki uweledi zaidi kuliko ilivyosasa ambapo limekuwa jukwaa la kuzogoana
3. Mwisho kabisa vifungu vya katiba viwe topics kwenye somo la URAIA/CIVICS/GS. Leo watu wanaambiwa katiba mpya ila ni ajabu wengi hata waliopata bahati ya kupata elimu ya darasani hawaijui hii katiba iliyopo.
Wengi wanasikia kutoka kwa wanasiasa ila wao Kama wao hawajui udhaifu au umadhubuti wa katiba iliyopo. Si ajabu leo msomi wa chuo kikuu hajui kilichomo ndani ya katiba
Ikiwa sehemu ya somo mashuleni na ikawa somo la lazima kwa ngazi fulani ya elimu itaweza kusaidia Raia wengi kutambua haki zao za kikatiba na kuzipigania kuliko ilivyosasa
Kwa Sasa wanasiasa hawana nafasi nzuri ya kuleta katiba bora Tanzania kwa maslahi mapana ya Taifa. Wengi wana focus uchaguzi wa 2025 ndiomaana agenda kuu imekuwa kutoshiriki uchaguzi bila katiba mpya
Katiba haitakiwi ku focus uchaguzi tu! Katiba ni zaidi ya uchaguzi, ni zaidi ya CCM, CHADEMA na nk. Katiba ni zaidi ya Mbowe na Samia! Katiba inatakiwa iandaliwe bila pressure na kwa focus iliyohuru itakayojali Tanzania na watanzania waliopo na wajao!