Waliokaidi agizo la EWURA watozwa faini mil 10/-

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Waliokaidi agizo la EWURA watozwa faini mil 10/-


na Happiness Katabazi



MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es salaam, imewahukumu kifungo cha miezi sita nje na kulipa faini ya sh milioni 10 wafanyabiashara wawili wa vituo vya mafuta baada ya kupatikana na hatia ya kukaidi amri ya Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ya kufunga vituo vyao vilivyokuwa vikiuza mafuta yaliyochachuka.
Wafanyabiashara hao ni Mohamed Twalib Nahdi na ndugu yake Abdulatif Twalib Nahdi ambao wote ni wakazi wa Morogoro.
Akitoa hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Jaji Thomas Mihayo, alisema amekubaliana na hoja zilizowasilishwa na Wakili wa Ewura, James Kabakama, kwamba amri iliyotolewa na mamlaka hiyo Septemba 19, 2008 inapaswa kuheshimiwa.
Jaji Mihayo alisema yeyote atakayekiuka amri ya mamlaka hiyo atachukuliwa hatua kali za kisheria na kwamba ametoa adhabu nafuu kwa wafanyabiashara hao, ili waweze kujirekebisha.
Kufuatia uamuzi huo, Jaji Mihayo amewataka wafanyabiashara hao kutotenda kosa kama hilo ndani ya miezi sita na akawapa wiki mbili wawe wameshalipa faini ya sh milioni tano kila mmoja. Vituo vya mafuta anavyomiliki Abdulatif Twalib Nahdi ambavyo vimefungiwa ni Kobil Msamvu Petrol Station na Abdulatif Petrol Station.
Aidha, Mohamed Twalib Nahdi naye anamiliki vituo vya Mohamed Twalib Petrol Station, Oilciom Kihenda Petrol Station na Mohamed Twalib Oilcom Petrol Station. Ilidaiwa kuwa EWURA walifanya ukaguzi wa vituo vyote vya mafuta mkoani Morogoro kati ya Septemba 13 na 14 mwaka jana na kubaini vituo vya wafanyabiashara hao kuwa vilikuwa vinauza mafuta yaliyochakachuliwa. Kutoka na hali hiyo, EWURA, iliwataka wafanyabiashara hao kufunga vituo vyao na kujieleza kwa nini wasichuliwe hatua kwa kuuza mafuta yaliyochakachuliwa. Hata hivyo, wafanyabiashara hao walikiuka amri hiyo na kuendelea na shughuli zao.
 
Pdidy,

..mbona nilishakuwahi na habari hii.

..MODS naomba muunganishe hoja yangu na hii ya Pdidy.
 
huu ni uhuni mtupu.............sasa hiyo million 5 wanayotoa inasadia nini....wamearibu magari ya sh ngapi..???????na zimewagarimu watu sh ngapi kutengeneza ??????
HII NI JUDGMENT YA KIJINGA KABISA
 
Re: Waliokaidi agizo la EWURA watozwa faini mil 10/-
Pdidy,

..mbona nilishakuwahi na habari hii.

..MODS naomba muunganishe hoja yangu na hii ya Pdidy. KUMRDHI MKUU NAOMBA MOD UNGANISHA SIKUONA MKUU
 
Pdidy,

..nadhani walitozwa milioni 60 na EWURA.

..inabidi adhabu ziwe kali kiasi kwamba wahuni hawa waone ni hasara kufanya upuuzi wao.
 
Wapumbavu hawa mkuu.......mi nilikuwa mwathirika wa ile shell ya pale madafu...washenzi wale walikaataa kunilipamkabisa siku ya siku wakafungiwa sasa hivi wanatanua................hawa ewura wanakula mlungula awana lolote.......kama si uhuuni mtupu
we unasema ati petrol ni 1400----------1580......kwa nini usiseme petrol mwezi huu sh kadhaa badala yake bp wanauza wanavyotaka wanangalia kisa tu.........watu wa ewura wana shell zao....blaal pdidy

na walaaaniwe milele hawa hata kama awatachukuliwa adhabu zaidi
 
Back
Top Bottom