Waliokaa kimya hoja ya wagombea binafsi- Ndiyo imekula kwao! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliokaa kimya hoja ya wagombea binafsi- Ndiyo imekula kwao!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 12, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Umaana wa kuwa na wagombea huru/binafsi ndio unaonekana sasa. Wengine tulipopiga kelele watu wakatuona kama "hamnazo". Sasa waliokaa kimya wanatamani kubebwa wakati kama kungekuwa na wagombea huru au binafsi mtu unawanyoshea kidole cha kati tu halafu huyo unaenda kugombea kama mtu huru.. lakini waathirika wakubwa wenye...we hawakutaka hata kunyosha mkono kuonesha kuhesabiwa! Imekula kwenu hiyo!


  Leo, wananikera wana CCM ambao wanatishia kurudisha kadi, sijui kukata rufaa huku wengine wanaandama na machozi yakiwatoka. Ninawaangalia na ninacheka. Sasa ndio wanajua kwanini kulazimisha watu wote katika nafasi zote kugombea hadi wawe na chama ndio matokeo yake haya. Na mtindo huu ndio unalazimisha rushwa kwa sababu kama watu wangekuwa na wagombea binafsi/huru nani angehangaika kuhoja wajumbe wa mkutano gani sijui wa kipuuzi ili jina "lipitishwe!"

  Tumejenga hoja kwa miaka minne kuwa haki ya kugombea ni haki ya msingi kama ile ya kupiga kura lakini hatukuwasikia wana CCM wakionesha kuwa wanaelewa dhana hii. Sasa wametupwa nje, wamegaragazwa, wamefanywa kihoja wamebaki wanapiga ramli na wengine wanakufuru kuibembeleza CCM iwabebe!

  Mioyo yao inawadunda kwa sababu wanaombea tarehe 14 August ije upesi ili wajue kama waanze tambiko au ndio mgonjwa kaokolewa sekunde za mwisho kama yule "aliyeonja pepo".

  Nasema, na ninarudia tena. Wana CCM msilalamike kuenguliwa, na wa wale wa upinzani ambao nao wamekopy na kupaste mtindo na mfumo mbovu wa CCM nao wasilalamike. Huwa tunavuna tulichopanda. Wakati wenzao tunahangaika kupanda hoja ya wagombea huru/binafsi wao walituambia ati "Tanzania haiko tayari"; Sasa leo waiona ngondo wafunga milango?

  Next time, mjue ni wakati gani wa kutetea mambo ya msingi na wakati gani kufanya mambo ya siasa!

  Ndio maana Nyerere alisema wazi kuwa uamuzi wa kufuta haki ya wagombea huru ni uamuzi wa Kipumbavu!!! Nakubaliana naye. Na nina uhakika hakuna mwana CCM hata mmoja ambaye analielewa hili kwani sasa wanajipanga tena kwa 2015 huku wakiombea labda "chama" next time kitawakumbuka!!

  Wanasema, "imekula kwao".
   
 2. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2010
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35


  Mzee hiyo nyekundu vipi tena...you just kidding right?..
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  The lips of the righteous teaches many; But fools die for want of wisdom

  Proverbs 10:21 sung by Peter Tosh.

  Amandla........
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naungana na wewe kuna kipiti hutakiwi kukumbatia ushabiki wa ki chama na kisiasa bali unatakiwa kufanya mambo ya msingi kwa demekrasia ya nchi.
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Wabunge maamuzi yao ni mzaha mzaha

  Mahakama maamuzi yake ni ya mzaha mzaha

  Rais utawala wake ni mzaha mzaha

  Tanzania ni lazima sasa tupate sulushisho, na tuondokane na maamuzi ya mzaha mzaha.
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  CCM kiboko, hata baada ya baba yao Nyerere kuwapaka live on this May 1-1995 Mbeya wamekomaa kichwa mpaka leo.

  Halafu hawaishi kumuimba na kumtaja kama ndiye "dira" yao.

  http://www.dailynews.co.tz/columnist/?n=11323&cat=columnist


  Thursday August 12, 2010
  Columnist
  Why the issue of Independent Candidates was at the heart of Mwl. Nyerere


  Makwaia wa Kuhenga, 1st July 2010 @ 16:00, Total Comments: 2, Hits: 993

  LANDMARK news in the last three weeks has been the suspension of the decision by the Tanzania High Court to allow private candidates to vie for parliamentary and presidential positions in the forthcoming General Elections.

  The suspension by the Tanzania Court of Appeal presided by the Chief Justice at the head of a seven-judge bench has raised a number of questions most of which centre on the efficacy of the present day Constitution of the United Republic of Tanzania, in the context that it is the President of the day who virtually appoints all persons in senior positions in governance without recourse to checks and balances or an alternative authority of appointment of independent of the Executive.

  This will be the well-considered view of the author of this perspective at its conclusion, having heard the ruling of one of the estates of the State, the Judiciary. But before then, let us revisit the highlights of the decision by the Court of Appeal overruling an earlier decision by the High Court to allow private candidates, independent of political parties in place.

  I have a copy of this newspaper, the Daily News, before me. Its June 18 lead story whose heading reads – No private Candidates in October - says, inter alia, quoting the Chief Justice who also heads the Court of Appeal: "The issue of independent candidates has to be settled by Parliament because it is a political matter and not a legal one. Each party should bear its cross."

  The newspaper quoted the Chief Justice as saying in his ruling that the issue of independent candidates depended on the social needs of each country, based on the historical realities. "Tanzanian courts should exercise calculated restraint to avoid meddling with constituencies of the other two pillars of the state," the newspaper quoted the Chief Justice as saying.

  Fair enough. But what had been a fundamental issue that was being contested all the way from the High Court to the Court of Appeal? When does politics start and end? How does one separate a legal issue from a political one? Isn't the wish to stand for elective office independent of political parties an indispensable basic right of a given citizen anywhere?

  I have been consulting the views of other fellow citizens following the ruling of Court of Appeal to overrule the High Court allowing independent candidates. According to one citizen; quoting Article 107:1 of the Constitution of the United Republic of Tanzania (1977), "The Judiciary within the United Republic of Tanzania and the Judiciary in Zanzibar will be expected to dispense justice to whomsoever…"


  And the quest for justice, according to this fellow citizen cannot be relegated to Parliament and the Presidency. Logically, therefore it is the responsibility of the Courts to dispense justice where there is a political tussle.

  Otherwise, why have we, in the past, seen erstwhile candidates in an election petitioning at the courts the outcome of a given vote? We will come back to this point at the last leg of this perspective when we come to address the phenomenon of the immense powers bestowed on the Executive of this country, that is the presidency by the present day Constitution, which powers are devoid of oversight or checks and balances or alternative organs to nominate individuals to head offices of the pillars of state power such as the Judiciary.

  For now, let me also add one person who could have been utterly dismayed if not surprised, had he been alive by the decision of the Court of the Appeal to overrule the High Court which had earlier seen justice in the participation of independent candidates for elective office.

  This is no other than the Father of this Nation, Mwalimu Julius Nyerere. Intermittently in his lifetime and especially after his retirement in the last days of his life, Mwalimu Nyerere spoke of the need and imperative for independent or private candidates away from established political parties to vie for elective office.

  Mwalimu Nyerere used to argue and convincingly that independent candidates would not only be helpful in widening democratic space but it would be a welcome relief to free the respective consciences of those individuals who see something fundamentally wrong with established political parties and cannot associate themselves with those parties.

  To deny them the right to stand for elective office just because they are not associated with a political party would be to inflict an injustice on them and to deny the country of the visions subscribed by these individuals.

  Clearly, even from the perspective of a non-legal counsel like me, to subscribe to this just stated view by Mwalimu, by any of our courts would be the right stance to take, even taken from a purely moral premise. So what could have been the constraint of the Court of Appeal to uphold an earlier stance by the High Court, in this context a lower court?

  It is my well considered view, taken with all due respect to the members of the seven person bench headed by the Chief Justice himself that the real constraint is the present day Constitution which bestows unlimited powers to the Executive, that is the president of the day, who appoints practically everybody senior in the three pillars of state power.

  So I really agree with those people who have been calling for a new Constitution that will take into account the needs for the present and future of this country. If the language of a new constitution altogether sounds far fetched, then there is need for more constitutional reforms that will impose checks and balances on the presidency.

  Those reforms may subject the President's appointees to parliamentary oversight committees for instance. And where the Head of the Judiciary is concerned, the Constitution should give nomination powers to another pillar of the state, such as the Legislature (parliament) as is the case with the position of the Speaker who is not the prerogative appointee of the President of the day.

  This way, the hands and feet of the Head of the Judiciary as they would appear today will be untied and freed to dispense justice without any constraint. And for another thing, if the supreme law of the land, that is the Constitution, streamlines roles and responsibilities clearly in so far as the pillars of state power are concerned, then we will have put in place a mechanism that will take care of human factors related to undue misinterpretation and misunderstandings.

  Every estate of state power, that is, the Executive, the Legislature and the Judiciary will be able to dispense its respective role unconstrained for the simple reason that there is politics everywhere! And the country will have ensured for itself of sustained justice, short of which, ‘hatufiki" (We won't make it!) – to borrow from my weekly TV Show – Je, Tutafika? /Shall We Make?

  Makwaia wa Kuhenga is a senior journalist E-mail: makwaia@bol.co.tz
   
 7. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Ni kweli imekula kwao. Ila binafsi kwa issue hii ya ugombea binafsi kinachonisononesha moyo zaidi na kujuta kuzaliwa Tanzania ni ile hukumu ya mahakama ya rufaa. Mahakama ya juu kabisa nchini kujivua jukumu la kuitetea haki ya raia wake na kuivisha kazi hii wanasiasa. Ee Mungu utaturejeshea je hii haki iliyokwepwa na chombo cha kuirafsiri na kuitoa? Jamani naomba kuuliza hauwezekani jaji mkuu na mahakama yake ya rufaa kushitakiwa kwenye mahakama za kimataifa, na hasa katika kitengo cha haki za binadamu? MMJ tusaidiane hapa tafadhali
   
 8. GY

  GY JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Umenena wakijiji...kama ni mtarimbo basi umelela doro!
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Aug 12, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Wale waliosoma hadithi za Esopo wanakumbuka hadithi hii

  Wakati mmoja Nyumbu alikuwa akinywa maji kwenye kisima na kufurahia taswila yake iliyokuwa ikitoka kwenye kisima kile. Akajisemea. "Ah, ni wapi ambapo unaweza kuona mnyama mwenye pembe nzuri kama zangu hizi! natamani ningekuwa na miguu mizuri zaidi kuweza kubeba hili taji la pembe zangu; nina bahati mbaya sana kuwa miguu yangu hii ni myembamba na myepesi sana, inaniudhi sana".

  Wakati huo huo kulikuwa na mwindaji aliyekuwa akimneyemelea na alipokaribia akamrushia mshale ambao uliapitia karibu sana miguu ya yule nyumbu lakini haukumdhuru. Kutokana na wepesi wa miguu yake aliyokuwa akidharau, nyumbu yule aliweza kukimbia kwa kasi sana kutoka kisimani na kumwacha mbali yule mwindaji, ila kwa vile alikuwa na hofu, alikimbia bila kuangalia anakwenda wapi. Basi akapita katika kichaka ambacho matawi yake walikuwa yamening'inia chini sana, hivyo pembe zake alizokuwa akijivunia zikanaswa kwenye tawi mojawapo na akashindwa kuondoka. Ndipo yule mwindaji alipomkaribia vizuri zaid na kumwua papo hapo.


  Mwanakijiji, watu unaowaongelea walifurahia sana uzuri wa pembe zao na kudharau wembamba wa miguu yao. Ingawa miguu hiyo myembamba ingewaeza kuwaokoa, sasa wanajikuta wanauwawa kutokana na pembe zao walizokuwa akijivunia.

   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ule msemo kuwa "mkuki kwa nguruwe mtamu, kwa binadamu mchungu" unaweza kuwa ni wa kweli; sijui wa Kiingereza unaofanana nao ni upi.
   
 11. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  The arrow to the pig is sweet, to the human is bitter.Joke.

  The closest thing I can think of is 'People who live in glass houses should not throw stones.". The same essence but not exactly the same thing.

  But surely I can't expect a replication of proverbs in these distinct languages, it rarely happens.

  In terms of idioms we could say "the shoe is on the other foot". And you know when that happens, it hardly fits.
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ngoja nivute hii Album kutoka kabatini maana siku nyingi saana sijaisikiliza na asante kwa kunikumbusha.

  Album hii kwa ujumla ina nyimbo nzuri sana kwa watu wengi Tanzania. Ukiongeza na ule wa "Guide me from my friend", "That's the way they will do" na nyingine nyingi ambazo ni vizuri kuzipitia. Sikufahamu kuwa ni maneno ya Zaburi. Asante kwa kuni/tujuza.

  YouTube - Peter Tosh - Fools Die (For Want Of Wisdom)
   
 13. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Basi mimi nawafurahia kweli wanavyoparangana hivi. Maana hawa jamaa ukiwakosoa wanakushambulia kweli. Watasema una wivu wa kike, huna nia njema na nchi yetu, umeishiwa au umefilisika kisiasa. Haya yanapowatokea, mimi nafarijika sana maana huu ni mtaji mhimu sana kwetu kisiasa. Naomba sana Mungu ili hawa bwana waendelee kuparulana hivyohivyo wakati sisi tukiendelea kujijenga, tayari kwa kuchukua nchi. Nadhani mnanielewa hapo, kwamba kukataa kwao mgombea binafsi kwa kudhani atawabania, limekuwa ni jambo jema kwetu, hakuna kuwahurumia wala kuwasikitikia kwa wanachokumbana nacho. Aluta continua, hadi kieleweke.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Aug 12, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu,
  Kukosa kura za maoni kwa wana CCM hakuwezi kuhalalisha kuwepo kwa wagombea binafsi. Na hakika mkitumia sababu hii ndio mnaharibu kabisa matumizi ya nafasi hizo.

  Kama mgombea wa CCM ambaye kiimani anafuata itikadi za chama na amekataliwa na wananchi tu kwa sababu haaminiki mtu huyo hawezi kusimama kuwakilisha wananchi ktk njia yoyote ile hata ikiwa mgombea Binafsi..Ifike wakati wananchi tufahamu kwamba mgombea binafsi ni yule asiyefungamana na itikadi au sera za vyama vilivyosimamisha wagombea wake.

  Huyu mgombea anakuwa na mtazamo tofauti na wawakilishi wa vyama hivi vingine na huwezi kumkuta ati mgombea akinadi sera sawa na za CCM hali akijiita yeye ni mgombea binafsi. Hivyo wakuu zangu tusije poteza maana ya wagombea binafsi kama tulivyokwisha poteza maana ya vyama vingi. Uchaguzi Tanzania umekuwa swala la wewe mwananchi unamuaminia nani zaidi na sii swala la kuzikubali sera na ilani.

  Ila kitu kimoja tu ambacho sintawaonea huruma hawa wapiganaji kwa sababu tuliwaambia yaliyoandaliwa kwao wakapinga na kukiita kijiwe cha JF kuwa ni kijiwe cha uongo, chuki na uzushi lakini ajabu ni kwamba mengi yaliyozungumzwa hapa yamewatokea kweli sasa kilio chao kinakuja baada ya kutupwa nje?
   
 15. K

  Keil JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkandara,

  Siyo wote wanaoshinda kura za maoni wanakuwa wameshinda kihalali na siyo wote wanaokuwa wameshindwa kwenye kura za maoni wanakataliwa kihalali.

  Pili, wako wengine ambao ambao wanashinda kihalali, lakini majina yao hayarudi au kwa maneno mengine majina yao yanakatwa. Hawa hawakatiliwa na wananchi/wanachama bali wanakataliwa na "wenye chama".

  Kuna wengi sana wanaongoza kura za maoni kwa njia za rushwa na hawafanywi chochote na kuna wengine wanashinda kwa njia halali lakini majina yao yanakatwa.

  CCM kwa kuogopa hiyo double standard ndio maana serikali yao imepambana mpaka dakika ya mwisho kupinga swala la mgombea binafsi. Maana walijua kwa sababu ya hizo double standard zao, wangetoa mwanya wa exodus ya wanachama walioshinda kihalali na wakaenguliwa na hivyo kuongeza threat ya kupoteza majimbo. Maana kama mtu ameongoza kwenye kura za maoni ndani ya chama chake na bado akakatwa jina, akienda kwenye general election na akapambanishwa na independent candidate aliyemshinda kwenye ngazi ya chama, unategemea ataambua kitu?

  Hilo ndio ambalo CCM imekuwa ikiliogopa siku zote, lakini nina hakika come 2015, tutakuwa na wagombea huru/binfasi.
   
 16. Tindikali

  Tindikali JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 765
  Likes Received: 550
  Trophy Points: 180
  Yeye Nyerere aliruhusu wagombea wa aina gani?
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu kama ndivyo basi dawa ni kurekebisha mfumo mzima wa Upigani kura za maoni na sio kupachika kiraka nje ya tobo kama style ya nguo tukidai tunaziba pengo hilo.

  Mimi sitazami wagombea Binafsi kwa kuitazama CCM au kwa nini CCM hawataki wagombea binafsi isipokuwa natazama utaratibu wa kisiasa (demokrasia) ktk kuwepo wagombea binafsi. Hawa wote wanaodai kuwa wagombea binafsi wanachukua nafasi hiyo kwa sababu wanajua hawawezi kupita ktk uchaguzi wa ndani CCM. Sasa kwa nini wanabakia CCM hali wanaweza kwenda vyama vingine wakapita uchaguzi ikiwa wananchi wanawakubali?..Au onyesha utofauti wako na CCM kiitikadi bila shaka tutakuwa nyuma yako kukubali kama alivyojitangaza Rev. Kishoka.

  Kama unataka kugombea Ubunge au kiti chochote cha kisasa ni lazima uwe na mtazamo tofauti na mpinzani wako kiitikadi laa sivyo tunapelekea kuamini kwamba Ni mtu anayeweza kutuwakilisha na sio sera za mtu huyo. Yale yale ya kitumwa kuamini wazungu (watu weupe) ndio wanajua kuliko weusi pasipo hata kueleza tofauti ya uwezo wao. Tukumbuke tu kwamba siasa na itikadi ni Ubunifu wa mirengo ya kuboresha maisha ya jamii zetu, sasa ikiwa tuna watu 10 wenye itikadi sawa na tuwape nafasi za wagombea binafsi hali mchango wao hauna tofauti na ule wa mgombea wa CCM tunakuwa tunapoteza muda na fedha za wananchi.
  Ni sawa na utaratibu wa Taxi kuchukua abiria, kama unalo gari na unataka kulifanya Taxi nenda kasajili ktk jumuiya ya wana taxi kisha fanya biashara zako lakini sio kuomba haki ya kila mwenye gari aruhusiwe kusanya anapopenda kwa sababu tu kuna matatizo ktk mfumo wa jumuiya ya wanaTaxi. Hutaki Taxi ingia kwenye Daladala hutaki pia jaribu kufikiria kuanzisha njia usafiri mwingine utakao pingana na jumuiya zilizopo na sio kuomba kibali cha kusanya.

  Wonna be a Politiacian, be a Politician kwa kujiunga na chama unachokubali sera zao au pingana na itikadi za vyama vilivyopo.Leo hii tuna vyama zaidi ya 20 tena chini ya sheria kama hii tukiachia hapo unafikiria tutakuwa na wagombea wangapi?..

  Uchaguzi wa CCM tu umetuonyesha jinsi gani watu walijitokeza kugombea hali nimegundua kwamba CCM yenyewe haina hata wananchama zaidi ya millioni moja kutokana na hesabu ya wapiga kura. Matokeo yote ya kura za maoni za CCM ni ishara nzuri kwetu kutonyesha jinsi watu tulivyokuwa walafi wa madaraka badala ya uwakilishi wa wananchi kupitia chama.
   
 18. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nasikia mkuu umehamia 'CCK',vipi hutaki kuungana na wanaotaka kujitenga?
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji hoja hii inafahamika wazi, na ndio iliyoondoka na Profesa Mwaikusa. Si siri kuwa wakati wa uhai wake Mwalimu alisema wazi kabisa hii ni haki ya mtanzania kikatiba, na alitoa mfano wazi kuwa Sarawat alitumia haki hiyo kulinda maslahi ya wanajimbo wake. Lakini sasa tuko kwenye mazingira tofauti kabisa, mhimili wa CCM leo uko kwenye kulazimisha watu kugombea kwa niaba ya CCM au upinzani, ni rahisi zaidi kuwadhibiti wakiwa kwenye makundi hayo mawili.

  Ajabu ni kuwa wanaopinga hoja hiyo huwa wanaumia sana wanaposhindwa kwenye kura za maoni, wanaogopa kula matapishi yao.
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  CCK ndio madudu gani tena?
   
Loading...