Waliojitokeza kupiga kura ni kina mama zaidi, vipi mwakani?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Ule usemi kwamba vijana wengi ndio wanaofaham maana ya upinzani na ndio wenye mwamko zaidi kwenye chaguzi mbalimbali, lakini kinyume chake wengi wao katika uchaguzi huu hawakujiandikisha kupiga kura hasa mijini, hii ilikua ni kwasababu ya ubize wa kujitaftia riziki, na pia muda mfupi uliotolewa na serikali. Lakini je, kwa dalili ya matokeo haya ambao wengi wao walikua wamama na wazee, mwakani ambapo wengi macho yao ni kwenye madiwani na wabunge pamoja uraisi hali itakuaje? Ikumbukwe kua hawa wenyeviti walipita sasa ndio wahamasishaji wa maandalizi ya uchaguzi mkuu mwakani. 
na akina mama na wazee hupigia kura sana ccm...ningekuwa mtu waorganization wa cdm/ukawa kazi kubwa ingekuwa kuhamasisha na kutoa elimu ya uchaguzi tu na umuhimu wa kura kwa miezi iliyobaki
 
Wakina mama wanaopigia kura CCM hata sijui huwa wanatumia viungo kufikiria.........Wao ndio huwa wanalalamikia huduma duni kwenye vituo vya afya.....hao hao ndio wanaogombana na waume zao kuhusu kodi za meza kuwa hazitoshi...hao hao ndio wanaolalamika kuhusu kupanda kwa bei za vitu madukani........sasa wanasahau vipi mateso yote kwa miaka mitano kwa doti ya kanga na pilau.....???..............
 
Back
Top Bottom