Uchaguzi 2020 Waliojiandikisha kupiga kura ni milioni 29, waliopiga kura ni milioni 15 tu. Wananchi tumewapa CCM ushindi wa mezani

Raia Mtata

JF-Expert Member
Feb 4, 2017
315
592
Habari wanajamvi,

Katika Taarifa iliyotoka jana kuna taasisi moja walitoa majumuisho ya Uchaguzi 2020, na Takwimu yao wamesema watanzania waliojiandikisha katika daftari ni milioni 29 na waliopiga kura ni milioni 15 tu hii ina maana gani?

Wao wenyewe wamesema watanzania wengi wameogopa kwenda vituoni kwa kuogopa polisi ila hii ni sababu dhaifu sana.

Mimi kwa muono wangu hawa watakuwa ni wafuasi wa upinzani tu, wamesusia kwenda kupiga kura kwa sababu wamekatishwa tamaa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019.

Swali langu, kama wote hawa wangempigia kura Lissu hamuoni kwamba Dkt. Magufuli tungemuacha kwa mbali? Hata kama wangeiba wangefika sehemu aibu ingewashika.
 
Kwa taarifa yako hiyo 29m+ ni idadi ya kupika, na wapiga kura hawajavuka 10m. Hiyo 15m imetokana na kura za Magufuli za kuchakachua. Kama unadhani wanaona aibu hilo sio kweli maana wangeona aibu uchaguzi wa SM.

Magufuli ndio anayeagiza box la kura kunajisiwa ili kuhadaa umma kuwa anapendwa. Watu wengi wanaojitambua hawakuwa na muda wa kwenda kupiga kura, maana haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Kwa taarifa yako hiyo 29m+ ni idadi ya kupika, na wapiga kura hawajavuka 10m. Hiyo 15m imetokana na kura za Magufuli za kuchakachua. Kama unadhani wanaona aibu hilo sio kweli maana wangeona aibu uchaguzi wa SM. Magufuli ndio anayeagiza box la kura kunajisiwa ili kuhadaa umma kuwa anapendwa. Watu wengi wanaojitambua hawakuwa na muda wa kwenda kupiga kura, maana haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Aliyekwambia 29million ni ya kupika nani????

Jinga kabisa.
 
Jamani eee uchaguzi umekwisha. Hatuna muda na propaganda za kutafuta mchawi. Tuko bize na marekani sasa hivi.
 
Aliyekwambia 29million ni ya kupika nani????

Jinga kabisa.

Nasema hivi 29m+ Ni idadi ya kupika. Watanzania tupo 59m+, hiyo ina maana 29m+ ni nusu ya watanzania wote. Inatakiwa mtu kuwa mjinga wa kiwango chako, ili kuamini kuwa watu wazima yaani 18yrs+ ni sawa kabisa ya walio chini ya umri huo. Halafu mbali ya utata huo wote 29m wajiandikishe, halafu wapiga kura wawe 1/3 ya waliostahili kupiga kura.
 
Kwa taarifa yako hiyo 29m+ ni idadi ya kupika, na wapiga kura hawajavuka 10m. Hiyo 15m imetokana na kura za Magufuli za kuchakachua. Kama unadhani wanaona aibu hilo sio kweli maana wangeona aibu uchaguzi wa SM. Magufuli ndio anayeagiza box la kura kunajisiwa ili kuhadaa umma kuwa anapendwa. Watu wengi wanaojitambua hawakuwa na muda wa kwenda kupiga kura, maana haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Wala msitafute mchawi wakati wachawi ni nyinyi wenyewe,ukiombwa ushhidi wa haya uliyobwabwaja wala hutokuwa nao,uchaguzi umeisha tujenge nchi sasa kwani Rais ni JPM.
 
Anaandika Dr. Christopher Cyrilo

Ulichofundishwa kwenye somo la uraia sio kweli.

Ulikuwa mwanafunzi bora darasani kuliko wengine, walimu wakakuita 'jiniasi'. Na wewe ukakenua meno na kuchekelea...utafikiri 'jiniasi' kweli!
Ulisoma kwa bidii zote, usiku na mchana - si kwa lengo la kuvuna maarifa bali kufaulu mitihani, ukafaulu bila maarifa. Sio kosa lako, ni mfumo wa elimu yetu unaomfanya mwanafunzi kuogopa mitihani zaidi kuliko kupenda kujifunza, anasema Mwl. Mabala.

Na sasa umekuwa mtu mzima, unashangaashangaa tu. Unachokishuhudia ni tofauti na kile ulichojaza kwenye mtihani wa Uraia uliyofaulu vema kuliko marafiki zako wengi. Ulifundishwa eti Taifa linaundwa na mihimili mitatu, Serikali, Bunge na Mahakama, Uongo. Taifa linaundwa na Serikali, Serikali na Serikali. Spika wa bunge na jaji mkuu wote wanasujudu kwa kiongozi wa serikali, na wanaelekezwa cha kufanya na wao wanafuata bila hiyana. Wakikataa watakiona Cha mtemakuni. Kile ulichofundishwa eti mihimili mitatu inayojitegemea ni uongo mtupu.

Ukaambiwa eti viongozi wanachaguliwa na wapiga kura, Uongo.

Viongozi wanachaguliwa na wanaojumuisha mahesabu ya kura. Unapoacha shughuli zako kwenda kupanga foleni ya kupiga kura, sio kwamba ndio unachagua kiongozi - no - no - no, pale unawaongezea kazi wanaohesabu kura tu. Kura zikiwa nyingi ujue watachelewa kumtangaza mtu wanaomtaka wao. Hilo ulikuwa hujui? Wewe kweli ni pimbi.

Ukaambiwa Polisi ni walinzi wa raia na mali zao, na wewe ulivyo kilaza ukaamini kabisa! Kilaza mkubwa wewe!

Polisi ni walinzi wa viongozi wa nchi na matajiri dhidi ya masikini wasumbufu wanaojifanya kudai haki wakati hawana haki. Polisi ni ukuta unaotenganisha wananchi na 'WENYENCHI'. Na Kama hujui basi kuanzia leo ujue - masikini aliyekwapua kuku wa jirani anastahili adhabu kubwa hata kifo wakati tajiri aliyeibia serikali milioni 7 kwa kila dakika anasamehewa. Unakodoa macho?

Unasubiri mkuu mmoja wa mkoa atekwe - apotee uone jeshi la polisi litakavyohangaika? Sasa potea wewe! Watasema umejiteka au umekwenda kutembelea ndugu.

Halafu kuna lile suala la binadamu wote ni sawa! Na wewe uliamini kabisa?

Sikiliza, hata waasisi wa Taifa la Marekani, akina George Washington waliandika hivyo kwenye katiba yao, wakati huohuo wakiwa na mashamba makubwa yenye watumwa kibao wakiwafanyisha kazi za kitumwa. Bado unaamini binadamu wote ni sawa? Muone! wapo binadamu wengine ni sawa zaidi ya wengine - usipoelewa hapo sio tatizo langu.

Ndio maana kuna watu wanakunywa na kupikia tope huko Lindi kwa kukosa kisima cha Milioni 5, huku wengine wanapiga vigeregere mbele ya Dreamliner la Bilioni 500, na baadhi yao hawatalipanda hadi wazeeke wafe. Si binadamu wote ni sawa. Umeelewa we tumbili?

Elimu ni ufunguo wa maisha eti? He hee! Daah. Ungejua! Kuna profesa aliwahi kujizolewa umaarufu na kuonekana moja wa watu muhimu katika kuamua mustakabali wa nchi, leo ni mpumbavu mbele ya mtu aliyeghushi vyeti vya PhD! Unatoa macho? Jichunge na vumbi.

Elimu haiondoi ujinga, bali inampa mtu uwezo wa kuujua zaidi ujinga wake ili ajichunge, na hiyo haimaanishi kuwa elimu ni ufunguo wa maisha. Ujinga ndio ufunguo wa maisha na kadiri unavyokuwa mjinga ndivyo unavyofanikiwa zaidi- kama alivyosema mwandishi nguli wa zamani Mark Twain; "Ili ufanikiwe maishani unahitaji vitu viwili, Ujinga na kujiamini". Wajinga wengi wanaojiamini wametoka kwenye maisha kuliko wanaojifanya werevu... Ujinga ndio ufunguo wa maisha. Wewe endelea kujifanya mwerevu kwa sababu eti ulifaulu darasani! Faulu na maisha sasa! Ha haaa.

Tuache sisi wajinga tukomae na mapambio ya kusifu - kusifu - kusifu na kuabudu...na tukishateuliwa -nakwambia mtakoma. Mlijifanya sana kufaulu darasani sisi tukawa tunawachora tu... Eti wataalamu, utaalamu bongo!!! mapimbi wakubwa!
#JingaMimi
 
wala mim sijasusa ila siamini tume iliyopo sasa kuna faida gan mim niache mambo yangu nikajianike siku nzima...coz nipige nisipige watashinda sasa wewe endelea nao ushindi wa kishindo unless niko safe hio sio changamoto kwangu
hii tabia ya kususa naona mmeambukizwa na kamanda wa anga

"Raha Sana kuvushwa na MAGUFULI mitano mingine"
 
Nasema hivi 29m+ Ni idadi ya kupika. Watanzania tupo 59m+, hiyo ina maana 29m+ ni nusu ya watanzania wote. Inatakiwa mtu kuwa mjinga wa kiwango chako, ili kuamini kuwa watu wazima yaani 18yrs+ ni sawa kabisa ya walio chini ya umri huo. Halafu mbali ya utata huo wote 29m wajiandikishe, halafu wapiga kura wawe 1/3 ya waliostahili kupiga kura.
Huna ushahidi hebu tutokee uko.....
 
nice comment
Anaandika Dr. Christopher Cyrilo

Ulichofundishwa kwenye somo la uraia sio kweli. Kenge wewe!

Ulikuwa mwanafunzi bora darasani kuliko wengine, walimu wakakuita 'jiniasi'. Na wewe ukakenua meno na kuchekelea...utafikiri 'jiniasi' kweli!
Ulisoma kwa bidii zote, usiku na mchana - si kwa lengo la kuvuna maarifa bali kufaulu mitihani, ukafaulu bila maarifa. Sio kosa lako, ni mfumo wa elimu yetu unaomfanya mwanafunzi kuogopa mitihani zaidi kuliko kupenda kujifunza, anasema Mwl. Mabala.

Na sasa umekuwa mtu mzima, unashangaashangaa tu. Unachokishuhudia ni tofauti na kile ulichojaza kwenye mtihani wa Uraia uliyofaulu vema kuliko marafiki zako wengi.
Ulifundishwa eti Taifa linaundwa na mihimili mitatu, Serikali, Bunge na Mahakama, Uongo. Taifa linaundwa na Serikali, Serikali na Serikali. Spika wa bunge na jaji mkuu wote wanasujudu kwa kiongozi wa serikali, na wanaelekezwa cha kufanya na wao wanafuata bila hiyana. Wakikataa watakiona Cha mtemakuni. Kile ulichofundishwa eti mihimili mitatu inayojitegemea ni uongo mtupu.

Ukaambiwa eti viongozi wanachaguliwa na wapiga kura, Uongo.

Viongozi wanachaguliwa na wanaojumuisha mahesabu ya kura. Unapoacha shughuli zako kwenda kupanga foleni ya kupiga kura, sio kwamba ndio unachagua kiongozi - no - no - no, pale unawaongezea kazi wanaohesabu kura tu. Kura zikiwa nyingi ujue watachelewa kumtangaza mtu wanaomtaka wao. Hilo ulikuwa hujui? Wewe kweli ni pimbi.

Ukaambiwa Polisi ni walinzi wa raia na mali zao, na wewe ulivyo kilaza ukaamini kabisa! Kilaza mkubwa wewe!

Polisi ni walinzi wa viongozi wa nchi na matajiri dhidi ya masikini wasumbufu wanaojifanya kudai haki wakati hawana haki. Polisi ni ukuta unaotenganisha wananchi na 'WENYENCHI'. Na Kama hujui basi kuanzia leo ujue - masikini aliyekwapua kuku wa jirani anastahili adhabu kubwa hata kifo wakati tajiri aliyeibia serikali milioni 7 kwa kila dakika anasamehewa. Unakodoa macho?
Unasubiri mkuu mmoja wa mkoa atekwe - apotee uone jeshi la polisi litakavyohangaika? Sasa potea wewe! Watasema umejiteka au umekwenda kutembelea ndugu.

Halafu kuna lile suala la binadamu wote ni sawa! Na wewe uliamini kabisa?

Sikiliza, hata waasisi wa Taifa la Marekani, akina George Washington waliandika hivyo kwenye katiba yao, wakati huohuo wakiwa na mashamba makubwa yenye watumwa kibao wakiwafanyisha kazi za kitumwa. Bado unaamini binadamu wote ni sawa? Muone! wapo binadamu wengine ni sawa zaidi ya wengine - usipoelewa hapo sio tatizo langu.
Ndio maana kuna watu wanakunywa na kupikia tope huko Lindi kwa kukosa kisima cha Milioni 5, huku wengine wanapiga vigeregere mbele ya Dreamliner la Bilioni 500, na baadhi yao hawatalipanda hadi wazeeke wafe. Si binadamu wote ni sawa. Umeelewa we tumbili?

Elimu ni ufunguo wa maisha eti? He hee! Daah. Ungejua! Kuna profesa aliwahi kujizolewa umaarufu na kuonekana moja wa watu muhimu katika kuamua mustakabali wa nchi, leo ni mpumbavu mbele ya mtu aliyeghushi vyeti vya PhD! Unatoa macho? Jichunge na vumbi.

Elimu haiondoi ujinga, bali inampa mtu uwezo wa kuujua zaidi ujinga wake ili ajichunge, na hiyo haimaanishi kuwa elimu ni ufunguo wa maisha. Ujinga ndio ufunguo wa maisha na kadiri unavyokuwa mjinga ndivyo unavyofanikiwa zaidi- kama alivyosema mwandishi nguli wa zamani Mark Twain; "Ili ufanikiwe maishani unahitaji vitu viwili, Ujinga na kujiamini". Wajinga wengi wanaojiamini wametoka kwenye maisha kuliko wanaojifanya werevu... Ujinga ndio ufunguo wa maisha. Wewe endelea kujifanya mwerevu kwa sababu eti ulifaulu darasani! Faulu na maisha sasa! Ha haaa.
Tuache sisi wajinga tukomae na mapambio ya kusifu - kusifu - kusifu na kuabudu...na tukishateuliwa -nakwambia mtakoma. Mlijifanya sana kufaulu darasani sisi tukawa tunawachora tu... Eti wataalamu, utaalamu bongo!!! mapimbi wakubwa!
#JingaMimi
 
Habari wanajamvi,

Katika Taarifa iliyotoka jana kuna taasisi moja walitoa majumuisho ya Uchaguzi 2020, na Takwimu yao wamesema watanzania waliojiandikisha katika daftari ni milioni 29 na waliopiga kura ni milioni 15 tu hii ina maana gani?

Wao wenyewe wamesema watanzania wengi wameogopa kwenda vituoni kwa kuogopa polisi ila hii ni sababu dhaifu sana.

Mimi kwa muono wangu hawa watakuwa ni wafuasi wa upinzani tu, wamesusia kwenda kupiga kura kwa sababu wamekatishwa tamaa na uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019.

Swali langu, kama wote hawa wangempigia kura Lissu hamuoni kwamba Dkt. Magufuli tungemuacha kwa mbali? Hata kama wangeiba wangefika sehemu aibu ingewashika.

Waliokwenda kupiga kura ni hawa wasimamizi wa uchaguzi kutoka CCM na wanazipiga kura hapa

Kwa taarifa yako hiyo 29m+ ni idadi ya kupika, na wapiga kura hawajavuka 10m. Hiyo 15m imetokana na kura za Magufuli za kuchakachua. Kama unadhani wanaona aibu hilo sio kweli maana wangeona aibu uchaguzi wa SM. Magufuli ndio anayeagiza box la kura kunajisiwa ili kuhadaa umma kuwa anapendwa. Watu wengi wanaojitambua hawakuwa na muda wa kwenda kupiga kura, maana haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Tulikuambia mapema ukashupaaza, shingo wanaCcm mil 12+ ndio wamemchagua JPM. Na hili la wafuasi wa upinzani kutojitokeza ni ukweli hayo mengine unaleta uongo tu.
Screenshot_20201104-094823.png
 
Back
Top Bottom